bigmind
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 12,457
- 12,668
Una proof wapi kwamba shetani au Mungi alikosea mpakq pahitajike marekebisho....?Habari ya jumapili.
Dini inasema shetani aliasi huko juu mbunguni mahala palipotukuka na palipoinuka juu anapoishi mungu. Baada ya shetani kuasi mungu akamtimua na kumshusha huku Duniani.
Dini inasema baadae mungu akamuumba mwanadamu na kumuweka Duniani, maana yake mwanadamu alipowekwa duniani tayari shetani alikua duniani muda mrefu tu anakula zake maisha.
Hadithi ya shetani kuasi iko one sided, yaani inaelezwa kutoka upande wa mungu, hakuna aliewahi kusikia upande wa shetani(tayari binadam wanamshutumu shetani kwa habari ya kuambiwa, one sided story, hivyo shetani anahukumiwa kua ni mbaya bila kusikilizwa).
Dini haisemi kwa nini shetani aliasi na ilikuaje akaasi. Dini inasema mungu anajua kila kitu, all knowing lakini haisemi mungu alishindwaje kujua kua shetani atakuja kuasi ili asimuumbe. Na kama alijua shetani atakuja kuasi kwa nini alimuacha aasi. Mbaya zaidi huo mgogoro wao umetuingiza na sisi binadam ambao hatujui chanzo cha mgogoro. Yaani mungu anarecruit binadam washirikiane nae mwenye mgogoro wake na shetani huku binadam hawajui chanzo cha mgogoro wao. Na mungu anatishia kua yoyote ambae hatashirikiana nae kwenye mgogoro huo atampanish vikali. Unajiuliza hakuaje involved kwenye mgogoro nisioujua chanzo chake na natishiwa adhabu kali kama sitashiriki huo mgogoro, hivyo watu waoga na wajinga wanalazimika kushiriki mgogoro blindly ili kuogopa adhabu.
Kama mungu anawapenda wanadamu kama dini inavyosema alipaswa kurekebisha kasoro zilizojitokeza kabla ya kumuumba mwanadam, lakini pia alipaswa kujua in the first hand kua shetani atakuja kuasi kabla hajamuumba, vinginevyo hajui kila kitu kinyume na inavyosemekana kua anajua kila kitu.
Tukubali tukatae, maovu yote duniani kama mauaji, wivu, kifo, husda, wizi, matetemeko ya ardhi, tsunami, vimbunga, ukame, magonjwa yote chanzo chake ni mungu. Mbaya zaidi ameyatengeneza alafu ameshindwa kuyaondoa.
Hii mada inaendelea.
Pili una reference/ushahidi ipi kuonesha uasi mwingine umetokea mbinguni..???
Sent using Jamii Forums mobile app