Hivi karibuni kumezuka hii tabia ya kuonekana mtu sio raia ikiwa ana mawazo tofauti na watawala.
Sasa je watanzania ni mambumbu, maana kila wakimuona mtu anafikiri Zaidi/tofauti wanashuku kuwa sio mtanzania.
Yaani inaonyesha watanzania wana aina Fulani ya kufikiri, sanasana ni kufuata tu, ukianza kufikiri tofauti na uraia wako unakoma. Niambieni watanzania wenzangu isije kuwa na mimi sio mtanzania.
Enzi za mwalimu nyerere ilikuwa ukiwa na mawazo tofauti unafukuzwa nchini, ilikuwa hivyo kwa Kambona, Kezilahabi nk.
Jibu rahisi mkuu. Shauri/Toa mawazo yako mbadala kisha achana na hao wanaotoa uraia. Kama mawazo ni mazuri yatafanyiwa kazi na wenye akili. Mawazo ya mtu yanaishi.
Ukiwa una mipango yako na kuna mtu anataka kukuondolea focus na una resources nyingi at your disposal kumuondoa yeye kama kizuizi hautatumia hizo resources?
Vipi kama miongoni mwa resources ni Ofisi ya Uhamiaji? Au jeshi? Au bunduki? Hautatumia?