Kwanini mtanzania akifikiri sana/tofuti na watawala anaambiwa sio raia wa tanzania. Je, watanzania ni mambumbumbu?

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Hivi karibuni kumezuka hii tabia ya kuonekana mtu sio raia ikiwa ana mawazo tofauti na watawala.

Sasa je watanzania ni mambumbu, maana kila wakimuona mtu anafikiri Zaidi/tofauti wanashuku kuwa sio mtanzania.

Yaani inaonyesha watanzania wana aina Fulani ya kufikiri, sanasana ni kufuata tu, ukianza kufikiri tofauti na uraia wako unakoma. Niambieni watanzania wenzangu isije kuwa na mimi sio mtanzania.

Enzi za mwalimu nyerere ilikuwa ukiwa na mawazo tofauti unafukuzwa nchini, ilikuwa hivyo kwa Kambona, Kezilahabi nk.
 
Mbumbumbu, ata wewe ni mbumbumbu tu, Vipi umejisikiaje kuitwa mbumbumbu?

Vitu vingine vinachekesha sana sijui aliyebuni huu msemo mzee meko pale jangwani Alifikiria nini.
 
Mbumbumbu, ata wewe ni mbumbumbu tu, Vipi umejisikiaje kuitwa mbumbumbu?

Vitu vingine vinachekesha sana sijui aliyebuni huu msemo mzee meko pale jangwani Alifikiria nini.
Sio shida, lakini kwa nini mtu ukiwa unafikiri tufauti uonekane sio raia?
 
Ulitaka wote wawe kama mtume Paulo?
Acts 23:2-3
[2]
Kuhani Mkuu Anania akawaamuru wale waliosimama karibu naye wampige kinywa chake.
[3]
Ndipo Paulo akamwambia, Mungu atakupiga wewe, ukuta uliopakwa chokaa. Wewe umeketi kunihukumu sawasawa na sheria, nawe unaamuru nipigwe kinyume cha sheria?
 
Jibu rahisi mkuu. Shauri/Toa mawazo yako mbadala kisha achana na hao wanaotoa uraia. Kama mawazo ni mazuri yatafanyiwa kazi na wenye akili. Mawazo ya mtu yanaishi.
 
Ukiwa una mipango yako na kuna mtu anataka kukuondolea focus na una resources nyingi at your disposal kumuondoa yeye kama kizuizi hautatumia hizo resources?

Vipi kama miongoni mwa resources ni Ofisi ya Uhamiaji? Au jeshi? Au bunduki? Hautatumia?

NB: Mipango ni yoyote iwe ya nia njema au ovu.
 
Back
Top Bottom