Kwanini msibani wanawake ndio wanalia lakini wanaume hawalii?

Kwanini msibani wanawake ndio wanalia lakini wanaume hawalii?

Chizi Msomi

Senior Member
Joined
Jun 23, 2026
Posts
129
Reaction score
219
1. Kwanini msibani wanaume hawalii ni wakamili sana au kujikaza tu ?

2. Kwanini wanawake ndo huwa wanalia msibani ni udhaifu au ni mazoea?

3. Ni mara chache sana kukuta mwanaume msibani analia hebu nipeni" ufafanuzi,, wa jambo! hili wakuu

MJADALA:
 
Mwanaume tokea mdogo anaambiwa we unaliaje mtoto wa kiume kaza
Yaan anatengenezewa mazingira kwamba akionyesha hisia zake ni udhaifu

Acha sisi wanawake tulie tutoe sumu tupone

nyie mnalinda brand ya uanaume
so mnalia ndani kwa ndani

Au pengine ukiacha malezi labda ni swala la maumbile ngoja waje wajuzi
 
1 Kwa nini msibani wanaume hawalii ni wakamili sana au kujikaza tu ?

2 Kwanini wanawake ndo huwa wanalia msibani ni udhaifu au ni mazoea?

3 ni mara chache sana kukuta mwanaume msibani analia hebu nipeni" ufafanuzi,, wa jambo! hili wakuu

MJADALA:
KILIO ni hisia.
1. Mwanaume analia pale anahisi kulia hata kama amefiwa na mtu wa karibu..unaweza usione amelia wakati wa tukio la kifo lkn akalia baada ya mazishi.
2. Mwanamke analia Kwa hisia halafu Kuna wanaolia Kwa kuigiza. Nimewahi shuhudia Mwanamke anasemwa na wenzie kuwa Kwa nn hakulia alipofika msibani.
 
Utalia saa ngap wakati inatakiwa uende mortuary ukahakikishe marehemu hajaibiwa (ameogeshwa), watu msibani wamekula, jeneza/sanda imenunuliwa, umetafuta pesa za kusafirisha marehemu.
Uanaume ni mateso
 
Back
Top Bottom