Kwanini mnaficha jinsia Zenu.??

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,641
11,956
Habari za mwisho wa wiki wandugu.
Ashukuliwe Mungu kutupa tena pumzi ya uzima hadi tunakutana tena hapa jukwaani.

Kuna hili swali naomba nilielekeze kwenu.
Hivi ni kwanini baadhi ya member hapa JF ukiangalia profile zao utakuta hazielezi Jinsia zao?
Hivi sababu ni nini hasa hadi kuficha jinsia yako.?
Ni kuto kujiamini ama huipendi jinsia yako?

Inashangaza sana na inaleta tabu mtu anapochangia mada fulani hadi unapata utata kuwa huyu me ama ke mana anacho ongea hakieleweki.

Utakuta dume zima nalo limeficha jinsia.
Kuna wale walio funga PM zao, hawa hatuwalaumu labda hawataki usumbufu.
Lakini pia wengine ni kwasababu ya kutokujiamini hasa kwa wanawake wasio na msimamo.
Sasa hawa nao wanawake wanaume na wanaume wanawake ndo vipi sasa??

Karibuni.
 
Kila MTU Anaishi Apendavyo kikubwa havunji katiba kwani lengo lako hasa ni nini?? Kama MTU katoa mchango wake na una mantiki kuna haja gani ya kufuatilia jinsia yake?? Au umetumwa??
 
Kama tunaficha majina na sura zetu,kwanini tusifiche jinsia na umri wetu? Wanaoficha wako sahihi.
 
Back
Top Bottom