Kwanini Mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi ya HIV Tanzania?

Unajua mtu akienda kutibiwa dar basi ni lazima iwe muhimbili au lugalo na lazima anaenda kutibiwa tatizo lililoonekana kushindikana sehemu zingine zote ndo akapelekwa huko... Ukifikiri utaelewa
Hapo unaongelea rufaa.
Angalia idadi ya watu waliopo Dar.
Chunguza idadi ya watu wanoingia na kutoka Dar.
Je, nisawa na njombe?
Nasio kila anaenda muhimbili anaenda kwa rufaa, wapo wanaoenda bila rufaa.
SABABU IPO, ILA SIO HIYO ULIOSEMA.
 
Hapo unaongelea rufaa.
Angalia idadi ya watu waliopo Dar.
Chunguza idadi ya watu wanoingia na kutoka Dar.
Je, nisawa na njombe?
Nasio kila anaenda muhimbili anaenda kwa rufaa, wapo wanaoenda bila rufaa.
SABABU IPO, ILA SIO HIYO ULIOSEMA.
Uko njema
 
Niliwahi kumuuliza daktari flani wa njombe hili swali nilichoambiwa ni kuwa njombe kuna hospital kubwa kama ikonda hosp, bulongwa hosp, kibena hosp, ikelu hosp lugarawa na ilembula hosp. Zote ni hosptali kubwa sana hivyo watu wengi wanafika kupata matibabu huko kutoka sehemu mbalimbali na wakipimwa vvu takwimu zinasoma njombe kwakuwa watu wengi hawatoi taarifa sahihi wanatoka wapi... Ila sijui kama ndo uhalisia wenyewe

Kwamba mtu anatoka dar anaenda kupimia waya njombe?
 
Mimi nnachokijua ni kwamba Njombe inaongoza kwa maambukizi,lakini ukiwa ndani ya Njombe,MAKETE ndio inaongoza kwa maambukizi,na makete ndio wilaya pekee namba moja yenye baridi kuliko sehemu yeyote ndani ya Tanzania,nadhani kwa tahmini hiyo jibu litakuwa limepatikana kuwa kwanini njombe ndio iongoze kwa hilo tatizo,na maeneo mengine yanayofuatia lazima yana hali ya hewa inayoshahabiana na Makete...
 
Mimi nnachokijua ni kwamba Njombe inaongoza kwa maambukizi,lakini ukiwa ndani ya Njombe,MAKETE ndio inaongoza kwa maambukizi,na makete ndio wilaya pekee namba moja yenye baridi kuliko sehemu yeyote ndani ya Tanzania,nadhani kwa tahmini hiyo jibu litakuwa limepatikana kuwa kwanini njombe ndio iongoze kwa hilo tatizo,na maeneo mengine yanayofuatia lazima yana hali ya hewa inayoshahabiana na Makete...
Usijidanganye, mkoa Wote taabani, si Mkinga wa Makete, wala Mbena, wote hoi. Sisi tupo huku, kila Nyumba ina huzuni yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulia usome taratibu then ukielewa nilichoandika ndio urudi tena,unaweza ukawa umeni`crash lakini kumbe tunabishana wakati wote tupo upande mmoja..
Haya boss, Makete baridi ni ya kawaida, October hadi April Hakuna Baridi, kama Baridi ndio Ukimwi basi Russia, Canada, Norway pia na zingine, zingekua zinaongoza. Kiufupi ufupi wetu wa mawazo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baridi nazani ni chanzo kikuu
kikwete-20181025-0001.jpeg
 
View attachment 461162

Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia takwimu mbali mbali kupitia vyombo mbali mbali kuwa mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi na waathirika wa UKIMWI.

Swali langu ni la kidadisi(curiosity). Napenda kusikia toka kwa wataalamu na watafiti(kama tafiti zipo), kwanini isiwe majiji na mikoa mikubwa kama Dar, Mwanza, Mbeya n.k? Kama awali ilikuwa mkoa wa Kagera ndiyo ulioripotiwa mgonjwa wa kwanza na baadaye kuwa na waathirika wengi, ilikuwaje HIV iliruka mikoa ya hapo kati(Shinyanga, Tabora, Dodoma, Singida...) na kuufanya mkoa wa Njombe kuongoza?

Kama ni tohara kwa wanaume je, ni mikoa mingapi Tanzania hii walichelea kufanya tohara? Kwanini mikoa hiyo haijaathirika kiasi hicho? Japo kwa zamani(ninavyokumbuka) wilaya ya Makete(Njombe) ndiyo iliyokuwa ikiongoza na kwa sasa sina taarifa rasmi, bado ni jambo ambalo sina majibu yake, ilikuwaje mkoa wa Njombe uongoze kwa maambukizi?

Naomba wenye kufahamu majibu ya swali langu la msingi wanisaidie.

Kwanini Njombe?
Achana na hizo % Dar ndo inawathirika wengi kuliko mkoa wowote hapa TZ, idadi ya watu mkoa wa njombe ni tarafa moja tu ya Dar
 
Back
Top Bottom