kauzu12
JF-Expert Member
- Nov 11, 2016
- 868
- 779
Inaongoza kwa waathirika ka sababu ya kupenda kupima pima ukimwiKwa muda mrefu nimekuwa nikisikia takwimu mbali mbali kupitia vyombo mbali mbali kuwa mkoa wa Njombe unaongoza kwa maambukizi na waathirika wa UKIMWI.
Swali langu ni la kidadisi(curiosity). Napenda kusikia toka kwa wataalamu na watafiti(kama tafiti zipo), kwanini isiwe majiji na mikoa mikubwa kama Dar, Mwanza, Mbeya n.k? Kama awali ilikuwa mkoa wa Kagera ndiyo ulioripotiwa mgonjwa wa kwanza na baadaye kuwa na waathirika wengi, ilikuwaje HIV iliruka mikoa ya hapo kati(Shinyanga, Tabora, Dodoma, Singida...) na kuufanya mkoa wa Njombe kuongoza?
Kama ni tohara kwa wanaume je, ni mikoa mingapi Tanzania hii walichelea kufanya tohara? Kwanini mikoa hiyo haijaathirika kiasi hicho? Japo kwa zamani(ninavyokumbuka) wilaya ya Makete(Njombe) ndiyo iliyokuwa ikiongoza na kwa sasa sina taarifa rasmi, bado ni jambo ambalo sina majibu yake, ilikuwaje mkoa wa Njombe uongoze kwa maambukizi?
Naomba wenye kufahamu majibu ya swali langu la msingi wanisaidie.
Kwanini Njombe?