Kwanini mke wangu hataki kunisamehe?

Kwanini mke wangu hataki kunisamehe?

bobby dolat

Senior Member
Joined
May 18, 2015
Posts
167
Reaction score
263
Wakuu habari ya ujenzi wa taifa,

Kwa kweli hadi leo sijui nini kilinipata hadi nikatembea na shemeji yangu mdogo wa mke wangu wa ukoo.Kama si yule binti kunirubuni nisingefikia hatua ya kufanya kitendo hicho.

Historia ya tatizo:
Mwanzoni mwa mwaka jana wife aliniomba nimuombee kazi au nimpe kazi mdogo wake mtoto wa babake mkubwa ambae amemaliza chuo mwaka juzi. Hapo ninapofanya kazi mimi ni Administrative Officer ni kiwanda cha wahindi, hivyo haikua shida nikapigana kiume akaanza kazi ingawa sio ya mshahara mkubwa maana wahindi mnawajua walivyo. Miezi 4 mbele akaniambia ana zawadi yangu niifute alipopanga maana hawezi kuibeba kuja nayo kazini, ni shukrani kwa kazi niliyompa,ikawa kila nikifika kazini asubuhi huja ofisini kwangu kuniuliza kwa nn Jana yake sikweenda kwake

Siku moja nikamwambia basi leo tuongozane nina nafasi tulipofika pale akanipa shati jipya nikamshukuru akaniuliza haujaribishi nikufanyie na massage ya mgongo?Kwa kweli sijui nilikua nawaza nn nikajibu sawa akaaenda duka La dawa akanunua olive oil akaja nayo chumba ni kimoja tu hivyo akaanza kunifanyia masage huku tunapiga story mbalimbali Ilifika pahala nikawa sina nguvu hata ya kuongea tena hasa alipoanza kifuani kushuka chini, nilihisi ni shoti ya Umeme imenipiga.

Zoezi zima likawa limekamilika na ukawa ni mchezo wetu kila mara, na hatukuwahi kwenda guest tulikua tukifanyia hapo hadi siku moja ambayo tulisikia hodi ikigongwa na binti kwenda kufungua na kukutana uso kwa uso na dada yake yaani mke wangu mimi.Mimi nilikua ndani ya shuka kitandani kama nilivyozaliwa.Mke wangu akaingia akaanza kulia mbele yangu, walikuepo na kaka zake wawili na ndugu wengine watatu wanawake kumbe walitufuatilia kutoka kazini hadi hapo baada kutuchunguza kwa muda mrefu

Matokeo:
Wife alibeba vitu vyake vyote akaondoka na watoto akarudi kwao baadae akaenda kupanga sehemu ambapo anaishi hadi sasa. Nimemuomba msamaha katika ngazi zote za familia na hata ngazi ya kanisa na hadi kwa paroko bado amekataa kunisamehe.Nimetuma marafiki zake na watu Wa heshima na hata bosi wake kazini anisaidie kuzungumza nae ndio kwanza akanitukana kwa nn nimeenda ofisini kwake.Hataki hata niende kuwaona watoto wangu pale anapoishi.

Wakuu nimefanya kosa gani kubwa la kustahili haya yote? Umeshakatika mwaka tangu aondoke home kwa tatizo hili sioni dalili njema siku za usoni na mimi nampenda mke wangu nahitaji turudiane cha kushangaza nyumbani kwao wanaona kama mimi ndio niliemrubuni yule shemeji yangu kwa aijili ya kumpa kazi wakati yeye ndio alinirubuni mimi.

Kwanini anakua na roho mbaya kiasi cha kushindwa kumsamehe mtu? Akina dada ukikosewa kiasi hiki unaweza kutaka kufanyiwa nini ili usamehe? Kwa ujumla napaswa kufanya kitu gani hasa kuweza kumu win tena wife? Maana kuna wanaomshawishi akadai talaka mahakamani sinajua a awaza nn kwa sasa.Nimekuja kwenu kwa Mara ya kwanza as a last resort to this problem.

Wana JF nifanye lipi liliobaki ili mke wangu arudi?

Your regards
 
Duuuuuuu!!! Yy hawez kujua kuwa ww ndo umerubuniwa kwa kuwa ww ni mkubwa!! Lawama zitabak kwako tu endelea 2 kuomba msamaha
 
Pole sana ndugu yangu kwa hilo janga. Kwanza nianze kwa kukushauri kua kwa mujibu na uzito wa kosa lenyewe msamaha sio haki yako na huwezi mlazimisha mkewe akusamehe. Mahusiono especially ya kimapenzi kati ya mke na mme sio kama KANISA au MSIKITI kua ukifanya dhambi hata ya makusudi utaungama na kwa imani unaamini kua umesamehewa. Hili ni swala la feelings/hisia na umemuumiza mke wako kwa kutembea na mdogo wake, yaan umepoteza sifa na heshima sio tu kwa mkeo na wanao bali kwa familia nzima ya mkeo. Just put urself in her shoes eti amekusaliti na mdogo wako wa kiume...si ungemnyonga???????

Here is my take, time is a good healer! mwache mkeo akae peke yake na watoto hata kama ni miaka 4 poa tu. Endapo ataona umuhimu wa kukusamehe basi umshukuru Mungu but ikishindikana kubali kuwajibika kwa uzembe na makosa yako and move on with life. One more thing, usimlaumu shemeji yako/mchepuko wako kwa kukurubuni , blame tamaa zako coz hawa viumbe sometimes wako weak sana. Labda tu umlaumu shetani.
 
Dah pole sana mkuu subiri labda atakusamehe ila hivi vishemeji vina mitego sana, nina kashemeji kamoja kalikuwa kanapenda kuja home halafu kanavaa ki hasara hasara sket fupi kama nini, halafu kazuri nilipata sana shida. nashukuru wajanja waliwahi kukapiga mimba sasa kamekuwa kapole sana.
 
wewe jamaa umenichekesha,eti unajiuliza why hajakusamehe hadi leo..my dear uhusiano wenu sio wa boyfriend and girlfriend, ni mume na mke...aisee umemsaliti na kumuumiza vibaya sana rohoni, tena na mdogo wake! aliyemuombea kazi!...

hiyo hasira na maumivu hayaondoki hivi hivi...ni pale mke wako atakapoamua kuomba msaada kwa Mungu ili amrehemu na amfundishe kusamehe ndio utakapoona mabadiliko, na hiyo talaka hata Biblia inakubaliana nayo kwamba adultery will result to divorce na proof ipo..shetani mbaya jamani,pole ndugu
 
Labda wengine watanisaidia katika hili. Mimi nnachojua unapoomba kitu chochote kile, kuna njia mbili tu za ufumbuzi katika kuomba kwako. Ama upewe, au ukataliwe. Sina hakika kama kuna njia nyingine ya tatu.

Umefumaniwa na mkeo, LIVE bila ya chenga badala ya kuwa mpole unalazimisha msamaha, Kivipi??!! Binafsi naamini ungemkata Matiti mkeo kama sio Puchi puchi kabisa laiti kitendo ulichofanya angefanya mkeo.

Kimsingi Kidume mwenzangu unachemka kulazimisha msamaha ilihali unajua umefanya kosa zito. Kuwa mpole mkuu. Wife kachagua kutokukusamehe kwa kipindi hiki kutokana na MAYAI VIZA uliyopasua. Kuwa mpole mkuu mpaka mkeo atakapoamua vinginevyo.
 
Ama kweli...... Ndoa ndoanooo,kila leo afazali ya janaaa
 
mkeo hana kosa wala ucmlaumu assume yy angetembea na ndg yk ingekuaje???? kilichobaki tubu kwamungu wako na muombe m.mungu alainishe moyo wa mkeo akusamehe.
 
Ingekuwa ww ungemsamehe au unapiga porojo tu...sisi wqnaume tunawatesa sana wanawake kila mtu eti nikajikuta nimefanya asa kwa nn isjikute hukufanya???.....cku iz wanaume wachache tumebak co siri na tatzo mnaoa bado wavulana.

OVER!!!!!!!!!
 
Kama hataki kukusamehe, usinedelee kumbuguz anza upya kwani kuanza upya sio dhambi, endelea na maisha yako na jaribu kumsahau. Kuna siku atakufuata mwenyewe.
 
nashindwa kuelewa mtu unaombwa msamaha unakataa .. jamani hakuna kitu kizuri kama kusamehe ... au kama vipi amfanyie kitu ahalafu amsamehe
 
Mkuu just upgrade that mchepuko to lollipop. Awe wife kabisa
 
Endelea kumpa muda, kama na yeye ana mtu wake jee? kama hajakusamehe usilalamike kosa lako mwenyewe na binaadamu tupo tofauti,alikataa anza maisha kivyako, au laa endelea kusubiri, maybe ipo siku atajirudi, ulivyokuwa unafanyiwa massage uliona raha sio
 
Mwaka mzima ulikuwa unaenjoy na nani? Muoe huyo. Hata akirudi hata kuheshimu tena.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom