Kwanini mimi sipati wangu...!

Kwanini mimi sipati wangu...!

Man Ngosha

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2012
Posts
219
Reaction score
69
Habari zenu Wana JF ,

Mimi ni kijana wa kiume, kwa muda sasa nimekuwa nikitafuta rafiki wa kike ambaye hapo baadae atakuwa mwenza wangu!

Ninachoumia ni kwamba sifanikiwi pamoja na kumshirikisha Mungu pia, najiuliza Maswali mengi!

Kama Mungu amenijaalia elimu, kazi na afya njema kwanini katika hili maombi yangu hayatimii? Nisaidieni wadau, wapi nakosea? Nimechoka na upweke, na umri nao unasogea!
 
pole mkuu punguza upole jitahidi kutongoza na uwe unadanganya kidogo.....una miaka mingapi?

ila wakati ukifika Mungu atakupa mwenzi tu
 
Usihofu Mungu ameshasikia maombi yako sasa anakuandalia huyo wa kufanana na wewe mimi ilinichukua miaka kadhaa nikimgojea Bwana anipe wa kufanana na mimi kumbe kilikuwa bado kitoto kidogo, Mungu alikuwa ansubiri kikomae komae anikutanishe na hiki kibinti.Kwa kweli ni kama tupo paradiso haleluya.
 
Unapoona umechoka ushindi wako ndo umekaribia, usikatee tamaa.Huo umri usikutishe bado sana.
 
Duh! Huwa ukimuomba Mungu anakujibu isipokuwa anakujibu kwa wakati autakae yeye kwa kukujibu mapema au kwakuchelewa cha msingi usikate tamaa endelea kumuomba ipo siku utampata tena mwenyemapenzi ya dhati kwako
 
usijali mkuu Mungu atakupa aliye wako. jichanganye kwny makundi km vile kanisan/msikitini jitokeze kwny shughuli mbalimbali km harus send off etc. bila hivyo km unafanya kazi za kutoka asubhi na kurudi usiku utapata chngamoto. kila kheri mkuu ktk mchakato huo
 
usijali mkuu mungu atakupa aliye wako. Jichanganye kwny makundi km vile kanisan/msikitini jitokeze kwny shughuli mbalimbali km harus send off etc. Bila hivyo km unafanya kazi za kutoka asubhi na kurudi usiku utapata chngamoto. Kila kheri mkuu ktk mchakato huo

pia kama ana gari siku moja moja panda daladala na treni mchanganyiko uko pia ni mkubwa.
 
Pia unaweza kuwa na matatizo mawili, either una aibu kwa hawa bidadas au unachagua mno yaani ukumuona unamtafakari sana then unapotezea unaona km si yy yupo mwnywe. Kwn hata umuombe Mungu hawezi kktongozea, ila amekupa akili na utashi wa kutambua na kuchagua, just do it!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom