Pulchra Animo
Platinum Member
- Jun 16, 2016
- 8,392
- 14,677
Inaonekana Waswahili tunaujua vizuri udhaifu wetu! Sasa tumeshindwaje kujirekebisha? Who bewitched us?
Muhindi muaminifu kabisa ni Goa ! Na ndo walikuwa wahasibu wa kuaminika tokea enzi za Sultan Sayyid Said.Eneo la Uhasibu Reginald Mengi aliajiri Wahindi ambao wanasifika kusimamia kwa uaminifu mkubwa finances...
Mfano mmoja wapo ni Mhasibu wa IPP FM Srinivas Chitanturi na wengine ambao wapo kwenye chain ya IPP kama wahasibu wakiwemo kule kwenye kampuni ya Maji na viwanda vyake...
Mengi sio tajiri wa kwanza kuwatumia watu wa asili ya Asia/India kusimamia kampuni zao...miongoni mwa matajiri wengine wanaotumia
sana raia hawa wa kigeni ni pamoja na Aliko Dangote ambae amekuwa akiweka Chief Finacial Officers kuwa wageni akiwemo Brian Egan aliehudumu kwa weledi wa hali ya juu na kwa uaminifu na kuiwezesha empire ya Dangote kuendelea kuchanja mbuga kama kinara cha uwekezaji Afrika...
Mwafrika mwingine tajiri ambae amekuwa akitumia wageni eneo la finances ni Mzimbabwe Strive Masiyiwa ambae ni miongoni mwa matajiri wakubwa Afrika ambae hapa Tanzania anamiliki TV1/Kwese,Raha nk na huko kwingineko ana makampuni lukuki unaweza kumtafuta wiki utamuona..... Huyu tajiri pia pamoja kwamba Chief Group Finance Officer wake ni mwanamama mwafrika lakini hajaacha kuwatumia wahindi ambapo msaidizi wa Finances za group ni Muhindi aitwae Minnesh Ajoodha....
Ukija kwa mzee wetu tajiri Bakhresa utagundua kwenye Finances pia kaweka Wahindi pale...Mfano Mkaguzi wa Hesabu wa ndani wakati fulani aliitwa Suraj Khandelwal sina uhakika kama bado yupo... lakini huyu ndo anakagua kuona usalama wa mapesa hapo Bakhresani...Lakini pia hapo hapo Bakhresa Mhindi mwingine kwa jina CA. AMAN VOHRA yeye ameshahudumu kwenye Idara ya Mapesa kama Mdhibiti Mkuu wa Rasilimali za kampuni.
MTAZAMO WANGU: Naamini kabisa kwa utafiti huu mdogo kwamba inaonekana kabisa kwamba Indians/Wahindi ni watu waaminifu na watu mahiri katika kupangilia expenditure na income kwenye kampuni...kwa hiyo niamini kwamba kama una plan ya kuibukia kwenye mega business hawa jamaa naamini ukiwaajiri kwenye eneo la finances unaweza kutoboa...Nina wasiwasi kwamba kwenye eneo la Uhasibu huenda sie ngozi nyeusi tunakosa uaminifu au tunashindwa kusaidia ukuaji wa businesses!
I stand to be corrected.