GODZILLA
JF-Expert Member
- Dec 26, 2014
- 5,909
- 10,567
Yaani, ni shida sana!swadakta
Yaani, ni shida sana!swadakta
Mswahili huwa haaminiki na Mhindi kwa sababu amekaa kikupiga piga kila muda...ukimpa Lori aendeshe anawaza atakuibiaje mafuta,matairi na kubadilisha vipuri aweke vibovu vizuri akauze Kariakoo Ilala,...sasa mswahili pale hampendi Mhindi kwa sababu tairi likibasti huko barabarani anataka urudi nalo na liwe na namba zilezile...Mhindi auditing ya assets anaifanya kwa kina ukizingua huna kazi...sasa mswahili atampendea wapi Mhindi...matokeo yake atasema Wahindi wabaguzi kumbe ni yeye kakosa maadili ya kazi...Usemalo ni Kweli ila wanawapa tabu wafrika wenzetu [emoji23][emoji23][emoji23]
Sasa Prof. Assad anaingiaje kwenye sledi hii inayomzungumzia Mengi na Uaminifu wa Wahindi/Baniani katika business Management...Hebu dadavua kiyakinifu kabisa tukuelewe kisha tukupe sapoti kama unapaswa!Niambie kwanza kama you stand with Prof Assad maana sie badala ya kuwatia nguvu watu wetu wazidi kufanya vyema tunawafanyia mambo ya hovyo
Kwani fani ya Prof Assad huijui? na utendaji wake uliotukuka hadi ma UN hukoSasa Prof. Assad anaingiaje kwenye sledi hii inayomzungumzia Mengi na Uaminifu wa Wahindi/Baniani katika business Management...Hebu dadavua kiyakinifu kabisa tukuelewe kisha tukupe sapoti kama unapaswa!
Wahindi ni waaminifu sana tofauti na waswahili
Eneo la Uhasibu Reginald Mengi aliajiri Wahindi ambao wanasifika kusimamia kwa uaminifu mkubwa finances...
Mfano mmoja wapo ni Mhasibu wa IPP FM Srinivas Chitanturi na wengine ambao wapo kwenye chain ya IPP kama wahasibu wakiwemo kule kwenye kampuni ya Maji na viwanda vyake...
Mengi sio tajiri wa kwanza kuwatumia watu wa asili ya Asia/India kusimamia kampuni zao...miongoni mwa matajiri wengine wanaotumia
sana raia hawa wa kigeni ni pamoja na Aliko Dangote ambae amekuwa akiweka Chief Finacial Officers kuwa wageni akiwemo Brian Egan aliehudumu kwa weledi wa hali ya juu na kwa uaminifu na kuiwezesha empire ya Dangote kuendelea kuchanja mbuga kama kinara cha uwekezaji Afrika...
Mwafrika mwingine tajiri ambae amekuwa akitumia wageni eneo la finances ni Mzimbabwe Strive Masiyiwa ambae ni miongoni mwa matajiri wakubwa Afrika ambae hapa Tanzania anamiliki TV1/Kwese,Raha nk na huko kwingineko ana makampuni lukuki unaweza kumtafuta wiki utamuona..... Huyu tajiri pia pamoja kwamba Chief Group Finance Officer wake ni mwanamama mwafrika lakini hajaacha kuwatumia wahindi ambapo msaidizi wa Finances za group ni Muhindi aitwae Minnesh Ajoodha....
Ukija kwa mzee wetu tajiri Bakhresa utagundua kwenye Finances pia kaweka Wahindi pale...Mfano Mkaguzi wa Hesabu wa ndani wakati fulani aliitwa Suraj Khandelwal sina uhakika kama bado yupo... lakini huyu ndo anakagua kuona usalama wa mapesa hapo Bakhresani...Lakini pia hapo hapo Bakhresa Mhindi mwingine kwa jina CA. AMAN VOHRA yeye ameshahudumu kwenye Idara ya Mapesa kama Mdhibiti Mkuu wa Rasilimali za kampuni.
MTAZAMO WANGU: Naamini kabisa kwa utafiti huu mdogo kwamba inaonekana kabisa kwamba Indians/Wahindi ni watu waaminifu na watu mahiri katika kupangilia expenditure na income kwenye kampuni...kwa hiyo niamini kwamba kama una plan ya kuibukia kwenye mega business hawa jamaa naamini ukiwaajiri kwenye eneo la finances unaweza kutoboa...Nina wasiwasi kwamba kwenye eneo la Uhasibu huenda sie ngozi nyeusi tunakosa uaminifu au tunashindwa kusaidia ukuaji wa businesses!
I stand to be corrected.
Utajiri hauna siri I disagree...labda ule wa kwenye hadithi za Alfu Lela Ulela za akina Mwajemi Mzuri na Nurdin au zile hadiths za Unyoya wa Kipanga Aziz...Utajiri una kanuni ambazo ziko wazi kabisa...hauji tu ghafla paa!...uchawi ndio unatufanya Africans tuamini utajiri ni mazingaombwe fulani ambayo anayafahamu tajiri husika pekee.Utajiri Wa MTU in siri ya MTU,staff management haina chochote kwenye asili ya utajiri Wa MTU.
Labda ungeweka kichwa cha Uzi wako kuwa staff management hasa ya waeshia imechangia pakubwa kuendeleza utajiri Wa bwana mengi
MD wa bonite bottlers limited nafikiri ni muhindi. Hawa jamaa kwa mahesabu sio wa kuchezewa hata wakinunua peni ya sh 100 wanaandikia kwenye rekodi wana nidhamu ya usimamizi wa ela na mali
Hili nakupa mia mia ni kweli kabisa .....Wahindi ni waaminifu sana tofauti na waswahili