Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,121
- 35,130
Mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM umekamilika na tayari John Magufuli ameibuka mshindi.
Jambo la ajabu kabisa ni kuwa mchakato huo umeacha machungu makubwa kwa baadhi ya wagombea na pia umeacha maswali makubwa juu ya mazingaombwe ya siasa za ndani ya CCM.
Familia ya Rais Kikwete ilikuwa tayari na mgombea wake Benard Membe huku akisindikizwa na January Makamba. Hizi ni kambi kubwa kabisa ndani ya CCM baada ya Edward Lowassa.
Jambo la ajabu kabisa ni namna Jina la Membe na Makamba lilivyoshindwa kufurukuta ndani ya Halmashauri kuu kiasi cha kuona wagombea dhaifu kabisa kama Amina Salum na Asharose Migiro wakipita.
Inawezekana kabisa nguvu ya kambi ya Lowassa iliwatengua kwenye Halmashauri kuu, lakini pia mwisho wa mchakato wa kumpata Mgombea urais katika mkutano mkuu ilipelekea John Magufuli kushinda kwa kishindo (87%) Je ni kura za kambi ipi zilizombeba Magufuli?