Kwanini mechi za CHAN zimekosa hamasa na mahudhurio mazuri viwanjani Tanzania?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
57,243
Reaction score
90,303
Tanzania hujinasibu kama taifa linalohusudu zaidi mpira na la viwango vya juu vya mpira Africa Mashariki, ajabu ni kwamba mahudhurio katika viwanjani katika CHAN ni haba sana na tunazidiwa hadi na taifa la wanariadha la Kenya!

Nimeshangaa hata mechi za timu ya Ibrah Traore (Burkinafaso) zilikuwa zimelala doro sana hakuna watazamaji kabisa pamoja pamoja na ufuasi mkubwa na hamasa aliyonao Ibrah Traore hapa bongo!
 
Hizo habari kwamba Tanzania ina viwango vya juu kimpira kuwashinda kina Kenya na Uganda umevitoa wapi ?

Pili haya mashindano ya CHAN yenyewe basi tu ila mashindano ya Timu fulani chache kucheza na watu ambao hata kwenye reserves hawamo (kwahio hata uzito wa mashindano yenyewe nao ndio hivyo) hapo ingekuwa wamekuja creme de la creme kutoka nchi nyingine na sio makapi nadhani mambo yangekuwa tofauti...

By the way pale Kenya Ruto alinunua ticket za kutosha na kuzigawa kama njugu....
 
Hehehe
 
Mbona ndondo cup huwa inakuwa na hamasa sana na shamrashamra??
 
Tanzania hujinasibu kama taifa linalohusudu zaidi mpira na la viwango vya juu vya mpira Africa Mashariki, ajabu ni kwamba mahudhurio katika viwanjani katika CHAN ni haba sana na tunazidiwa hadi na taifa la wanariadha la Kenya!

Nimeshangaa hata mechi za timu ya Ibrah Traore (Burkinafaso) zilikuwa zimelala doro sana hakuna watazamaji kabisa pamoja pamoja na ufuasi mkubwa na hamasa aliyonao Ibrah Traore hapa bongo!
Hii mada ndio inazingumzwa azam tv muda huu kupitia sports am,wanasema kuwa:
1.foleni zinakera
2.muda wa usiku ni shida kwa watu wengi
3.ukosefu wa huduma za chakula na vinywaji pembezoni mwa uwanja.
Ni baadhi ya sababu sasa kama kuna mwingine ana hoja aziweke hapa
 
Viwango vya furaha na hamasa vimepungua kwa kiasi kikubwa Sana siku hizi miongoni mwa waTanzania.
Kuna migawanyiko mingi Sana kwenye jamii za waTanzania, kiini Cha kuwepo kwa migawanyiko hiyo hasa ni Siasa chafu Sana zinazoendeshwa na Watawala wa Nchi hii. Chuki kubwa imetamalaki, uhasama umezidi, Watu Wana maumivu makali Sana mioyoni mwao, umaskiini na ufukara uliokithiri na kuvuka Mipaka, matukio maovu ya Utekaji Watu, dhuluma, Utesaji, kubambikia Watu Kesi za uongo, na Mauaji ya makusudi ya raia wema ndio yamekuwa kichocheo kikubwa zaidi kinachoongeza Chuki kubwa kwenye jamii.
Matokeo yake hamasa imepungua Sana kwenye suala hili la Watu kujihusisha na matukio ya kijamii kama hayo.
 
Mbona ndondo cup huwa inakuwa na hamasa sana na shamrashamra??
Mpira it's about competition sasa ndondo ni kwamba wote ni wataalamu nguvu sawa wanapimana nguvu hii ni kama bondia (Matumla) anapigana na Gangwe wa Mtaani (Tena bado anapigwa au kutolewa jasho)
 
Viwango vya furaha na hamasa vimepungua kwa kiasi kikubwa Sana siku hizi miongoni mwa waTanzania. Kuna migawanyiko mingi Sana kwenye jamii za waTanzania, kiini Cha kuwepo kwa migawanyiko hiyo hasa ni Siasa chafu Sana zinazoendeshwa na Watawala wa Nchi hii. Chuki kubwa imetamalaki, uhasama umezidi, Watu Wana maumivu makali Sana mioyoni mwao, umaskiini na ufukara uliokithiri na kuvuka Mipaka, matukio maovu ya Utekaji Watu, dhuluma, Utesaji, kubambikia Watu Kesi za uongo, na Mauaji ya makusudi ya raia wema ndio yamekuwa kichocheo kikubwa zaidi kinachoongeza Chuki kubwa kwenye jamii. Matokeo yake hamasa imepungua Sana kwenye suala hili la Watu kujihusisha na matukio ya kijamii kama hayo.
ok sawa ngoja tuone wengine wanasemaje
 
Hii mada ndio inazingumzwa azam tv muda huu kupitia sports am,wanasema kuwa:
1.foleni zinakera
2.muda wa usiku ni shida kwa watu wengi
3.ukosefu wa huduma za chakula na vinywaji pembezoni mwa uwanja.
Ni baadhi ya sababu sasa kama kuna mwingine ana hoja aziweke hapa
Mbona mechi za Simba na Yanga huwa wanaenda kuangalia muda wowote??
 
Mimi juzi nilikuta foleni ya maana ya malori. Jana nikaghairi kwenda uwanjani "Nia ilikuwepo ya kwenda mwanzoni mwa week".
 
Back
Top Bottom