Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 745
- 1,470
Kabla ya yote, kwanza pita katika Thread 'Diamond Platnumz: Fanyeni kazi, acheni lawama, kila awamu, kila uongozi mnalalamika' kisha ndo tukae kujadili title ya uzi huu hapo juu “Nikwanini Matajiri (Watu waliofanikiwa) Hudhani Masikini ni Wavivu?”
Si Nasibu na Omari pekee ndio wamekuwa wakwanza kuongea suala hili. Mara nyingi katika mijadala ya kijamii na hata mazungumzo ya kawaida, utakuta wale waliofanikiwa wakiwa na dhana kwamba umasikini ni matokeo ya uvivu na kutofanya kazi kwa bidii. Watu wenye uwezo mkubwa kifedha huamini kuwa kila mtu ana nafasi sawa na wao ya kufanikisha maisha, na kwamba wale waliobaki nyuma hawajitumi vya kutosha. Hii imekuwa kama imani iliyojengeka, ingawa ukweli unaweza kuwa tofauti kabisa.
Wapo matajiri waliofanikiwa kutoka chini na kufanikisha maisha kwa bidii kubwa. Lakini changamoto ni kwamba mara nyingi huchukua safari yao kama kielelezo cha wote. Wanashindwa kuona kwamba mazingira hayafanani kwa kila mtu. Kuna watu wanaokua bila elimu bora, bila mtaji, bila mitandao ya kijamii inayowasaidia, au wakiwa wamezuiliwa na changamoto za kijamii na kiuchumi ambazo ni kubwa kuliko jitihada zao binafsi.
Pia, naona mtazamo huu huwasaidia baadhi ya matajiri kuhalalisha nafasi yao (utajiri). Kukubali kwamba bahati, urithi, au mfumo wenye upendeleo uliwasaidia inaweza kuwa ngumu, hivyo ni rahisi zaidi kulaumu umasikini kama matokeo ya uvivu. Kwa upande mwingine, mitazamo ya kitamaduni na kidini pia imechangia. Katika baadhi ya jamii, utajiri huchukuliwa kama baraka na umasikini kama ishara ya gundu, jambo linalofanya umaskini kuonekana kama kosa la mtu binafsi.
PIA SOMA: Thread 'Hivi kwanini hapa Tanzania matajiri au watu waliofanikiwa kimaisha hupenda kutuongopea kuwa wao wanafanya kazi kwa bidii?'
Lakini tukitazama kwa undani, masikini wengi hufanya kazi ngumu kuliko inavyofikiriwa. Wanalima mashamba kwa jembe la mkono, wanabeba mizigo, wanaendesha bodaboda kwa saa nyingi, au kufanya kazi zisizo na kinga wala maslahi bora. Kazi hizi ni ngumu sana, lakini kwa kuwa hazilipi vizuri, mara nyingi hudharauliwa na kuonekana hazina thamani (sa sijui kazi gani Naseeb na mwenzake wanazungumzia).
Hii limeniacha na maswali mengi sana: je, kweli umasikini unatokana na uvivu na kutofanya kazi kwa bidii, au ni matokeo ya changamoto za kimfumo na kijamii ambazo mara nyingi hazionekani kwa macho ya wale waliofanikiwa? Kwa nini baadhi ya matajiri hupuuza jitihada za masikini? Na je, tunawezaje kujenga mtazamo mpya unaotambua mchango wa kila mtu bila kuwapachika majina yenye kudhalilisha?