Desire Dizaya
JF-Expert Member
- Feb 16, 2015
- 6,476
- 11,672
Habari wanajukwaa
Mimi leo napenda kushea nanyi hili suala linalonitatiza. Kwanini katika jamii zetu za sasa kama mtu ni wa kipato cha chini anadharauliwa ilhali mwenye pesa au tajiri anaheshimiwa na kuogopwa??
Je aina hii ya maisha iliwahi kuwepo tangu enzi za mababu zetu?
Utakuta mtu na pesa zake anafanya jambo sio zuri bali watu wanamchekea tu "oooh hamna tatizo." Sasa ukute ni maskini muokota makopo ama msukuma guta hapo uone hiyo mitusi.
Hata katika koo zetu za sasa, familia yenye pesa ndo wanapewa kipaumbele wale wa kubangaiza wanaachwa nyuma; kwanini? Jiangalie leo huna kitu umepanga Tandale kijumba kinakaribia kuanguka unavaa nguo za mia tano Manzese dharau utazopata na mitusi kwa walimwengu halafu fikiria Mungu akajibu maombi yako ukajenga mansion Mbezi unatembelea gari la bei mbaya, nguo zako sijui Uturuki uone watakujaje kwako.
Kwanini binadamu tu wanafki hivi? Katika maisha yangu mimi kamwe siwezi kumsimanga mtu sababu ya umaskini ama hali duni. Nanyi nawaasa muwe hivi kwani maskini na matajiri wameumbwa na Mungu mmoja.
Katika kitabu cha mithali 14;20 imeandikwa:- Maskini huchukiwa hata na jirani yake bali tajiri ana rafiki wengi! Sijui kwenye Quran wameandikaje anayejua aweke.
Mpende mtu kwa utu wake sio hali yake. Love u all JF members