Kwanini Marais wengine wastaafu kama Mwl. Nyerere na wengine hawasifiwi kwa kujenga miundombinu?

Radio mbovu ndio huwa ina makelele!!! Hakuna cha maana alicho fanya kwa wanadamu huyo magu aliye oza udongini muda huu. alidhani maisha ni kujemga madaraja tu bila kujali utu wa watu. wengine walijenga lakini tunawakumbuka kwa utu wao.
magufuli amelaaniwa.
 
Nyerere na wengine mengi wamefanya lakini hivi karibuni limezuka genge la wahuni wachache hawaoni yaliyofanyika na viongozi waliopita sijui labda walitaka na wao wawe madhulumati?
Hilo 'genge la wahuni' nadhani lilikuwa na nguvu kubwa sana hata kuishinda nguvu ya 'umma' vinginevyo umeandika ukiwa na kinyongo sana.
 
Radio mbovu ndio huwa ina makelele!!! Hakuna cha maana alicho fanya kwa wanadamu huyo magu aliye oza udongini muda huu. alidhani maisha ni kujemga madaraja tu bila kujali utu wa watu. wengine walijenga lakini tunawakumbuka kwa utu wao.
magufuli amelaaniwa.
Hiyo chuki uliyonayo brother achana nayo huwa siyo nzuri kwa afya.
Mwache apumzike na hukumu yake itakuwa ya haki kwa kadiri ya matendo yake wakati wa uhai wake, na kwako maisha lazima yaendelee, usiruhusu nyongo ianze kukuathiri mapema kiasi hiki.
 
Hiyo chuki uliyonayo brother achana nayo huwa siyo nzuri kwa afya.
Mwache apumzike na hukumu yake itakuwa ya haki kwa kadiri ya matendo yake wakati wa uhai wake, na kwako maisha lazima yaendelee, usiruhusu nyongo ianze kukuathiri mapema kiasi hiki.
you can go to hell.
 
Hivi kwanini Marais wengine wastaafu kama vile Mwl. Nyerere na wenzake waliomtangulia Rais Magufuli wao hawasifi kwa kujenga miundo mbinu?

Swali ni je Marais wastaafu wakiongozwa na Mwl. Nyerere wao hawakujenga miundo mbinu kama Rais wetu mpendwa wa awamu ya 5?

Kila mara anaposifia Rais wetu mpendwa wa awamu ya 5 Rais Magufuli watu wengi wanajikita katika ujenzi wa miundo mbinu.

Swali linalokuja kwa wananchi walio wengi ni je, mbona marais wengine waliopita wao hawasifiwi kwa kujenga miundo mbinu?
Mwenye jibu tafadhali tunaomba atusaidie.
Hili ndio jambo la ajabu sana
 
Sababu kuu ni kwamba JIWE alikuwa dictator na kawaida ya madictator ni kupromote majina yao kuliko wengine.

Kwa ufupi Magufuli anatajwa sana na watu wake kwa sababu alihakikisha kila alitendalo linaoneshwa,kusifiwa na kuenziwa.Serikali za nyuma hazikuwa mfano wa serikali ya awamu ya tano ya misifa na ndo maana yaliyofanywa yanapotezewa japo yapo mengi na yaliyoshiba.

Jamaa alifanikiwa kuirudisha Tanzania kipindi cha ujima na ashukuriwe M/Mungu kwa kutenda jambo lake kabla mambo kuwa mabaya zaidi (Astaghafirullah)
 
Unauliza swali na jibu unalofahamu.Jibu ni NDIYO.hakuna hata mmoja hapo aliyefanya kazi kubwa kama Magufuli katika ujenzi
 
Hivi kwanini Marais wengine wastaafu kama vile Mwl. Nyerere na wenzake waliomtangulia Rais Magufuli wao hawasifi kwa kujenga miundo mbinu?
Nyerere ana sifa lukuki kwa alioyafanya mpaka vitabu ametungiwa
 
you can go to hell.
Ungefikiria kwanza lugha yako ya taifa maana naamini kwamba hauna uhakika kama ujumbe wako umefika, by the way( na Mimi nisibaki nyuma ktk kizungu) unazidi kuonesha jinsi gani unavyoumia sana! kwani umebanwa sana?
 
Tatizo kuna wanasiasa hasa vijana wasiojua vyema historia ya Tanzania na watu wazima walioamua kujitoa ufahamu tu. Matokeo yake wanaishia kudemka tu badala ya kujadili mambo ya msingi.

Hayati Nyerere siyo tu alijenga reli ya uhuru, ya kisasa kabisa kwa wakati huo, toka Dar es salaam mpaka Kapirimposhi, bali pia alijenga mabwawa kadhaa ya kuzalisha umeme na gridi ya kuweka miundombinu ya kuusambaza umeme huo nchini. Hapo hatujaongelea viwanda mbalimbali ya kati vilivyojengwa sehemu mbalimbali nchini vikiongozwa na vile vya nguo. Lakini kubwa kuliko yote ni umoja wa kitaifa alioujenga na kuusimamia kwa nguvu zake zote. Na pia alikuwa kielelezo cha uadilifu kwa maraisi waliomfuatia na marais wa Afrika. Hapo hatujaongelea uongozi wake katika vita ya kuzikomboa nchi za kusini mwa Afrika zilizokuwa chini ya utawala wa kikoloni na kuifanya Tanzania kituo kikuu cha harakati za ukombozi. Ni yeye pekee ndiye mwenye sifa za kuitwa SHUJAA WA AFRIKA.

Mzee Mwinyi naye amefanya mambo makubwa ikiwemo uamuzi mgumu wa kuruhusu mfumo wa soko huria na kuuondoa mfumo wa uchumi wa dola uliojengwa wakati wa siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kama ilivyoainishwa kwenye Azimio la Arusha. Kupitia azimio la Zanzibar Tanzania ilipitia mabadiliko makubwa ya kiuchumi yaliyowezesha mitaji binafsi kuingia nchini na kubadili mwelekeo wa nchi kiuchumi. Mzee Mwinyi pia ndiye aliyekuwa muasisi wa siasa za ushindani wa vyama vingi.

Hayati Mzee Mkapa kimsingi ndiye chief architect aliyesuka mikakati ya kutufikisha kwenye uchumi wa kati na alifanya maboresho mbali mbali ya kimfumo na kiutendaji ili kuwezesha Ndoto ya kufikia uchumi wa kati 2025 ifikiwe. Katika utawala wake ndiyo ile ndoto ya kuunganisha nchi kwa barabara za lami ilianza kutekelezwa na ninakumbuka vyema alipotoa ahadi ya kuunganisha Bukoba na mtwara kwa lami jinsi ilivyofanyika kazi kwa vitendo.

JK akiendeleza alipoishia Hayati Mzee Mkapa alisimamia miradi mingi sana ya ujenzi wa uchumi ambayo mingi imezinduliwa wakati wa Hayati Mzee Magufuli. Pengine Mzee JK ndiye Rais aliyeanzisha miradi ya ujenzi wa bararaba za lami zenye urefu mkubwa zaidi kuliko raisi mwingine yeyote kwenye historia ya nchi yetu. Miradi ambayo JK aliianzisha na kuisimamia ni pamoja na:
(i) Chuo Kikuu cha Dodoma
(ii) Jakaya Kikwete Cardiac Center Muhimbili
(iii) Ujenzi wa airport Terminal III
(iv) Kutekeleza mradi wa BRT ulioasisiwa na Hayati Mkapa
(v) Mradi wa Bomba la Gesi ya Asili toka Mtwara Mpaka Dar es salaam
(vi) Ujenzi wa shule za sekondari kila kata
(vii) Ujenzi wa barabara ya lami toka Tunduma - Katavi
(viii) Ujenzi wa barabara ya lami toka Ruvuma Mpaka Lindi
(ix) Ujenzi wa barabara ya lami toka Dodoma mpaka Babati
(x) Ujenzi wa daraja la Mfugale
(xi) Ujenzi wa ringroads kupunguza msongamano wa magari DSM
etc. to mentiom a few.

Anayesema hakuna kilichofanyika kabla ya Mwendazake ama haijui vyema historia ya nchi yetu au ni mjinga tu anayehitaji kuelimishwa kwa busara na upole.

Tata said!
Asante kwa Elimu nzuri
 
Hivi kwanini Marais wengine wastaafu kama vile Mwl. Nyerere na wenzake waliomtangulia Rais Magufuli wao hawasifi kwa kujenga miundo mbinu?

Swali ni je Marais wastaafu wakiongozwa na Mwl. Nyerere wao hawakujenga miundo mbinu kama Rais wetu mpendwa wa awamu ya 5?

Kila mara anaposifia Rais wetu mpendwa wa awamu ya 5 Rais Magufuli watu wengi wanajikita katika ujenzi wa miundo mbinu.

Swali linalokuja kwa wananchi walio wengi ni je, mbona marais wengine waliopita wao hawasifiwi kwa kujenga miundo mbinu?
Mwenye jibu tafadhali tunaomba atusaidie.
Tena Nyerere alifanya vitu vingi sana vya maendeleo.
 
Nyerere madarakani zaidi ya 20 years miundo mbinu aliorithi kwa wakoloni aliharibu ... Hana sifa nzuri zaidi ya mbaya kwa hiyo bora tukanyamaza
Kwa uhalo huu tu nimeshahisi una elimu gani na umri wako!!pole, hiyo miaka 20, aliyoongoza Nyerere, kulikuwa na madini gani yanayochimbwa hapa TZ, zaidi ya alimasi tu?hilo deni la taifa lilikuwa kiasi gani?!!tatizo la jiwe alijuwa kuwa watu wengi wanaakili kama zako, yaani awadanganye kwa kujenga vitu vigeni vigeni, (vidaraja hivyo)kwani hatuwezi viita fly overs , vindege hivyo, mala daraja la juu ya maji!!tayari akawashika akili!!kuna watu wamefanya kazi nchi hii ila hawakupenda promo!!MUNGU FUNDI
 
Au humjui Nyerere unasimuliwaga kwenye kahawa?

Nyerere alikuwa habari nyingine!

Alitoa huduma za afya bure.
Alitoa elimu bure kuanzia msingi mpaka chuo kikuu. ELIMU BURE, kwa uzito wake,kuanzia pen,daftari,vitabu na hata nauli ya kwenda na kurudi shule/chuo.
Siyo elimu bure hi ya Sasa,unachangia chakula,mtoto anaenda na makande,na maharage shule,na maji na michango mingine kibao...THEN TUNAAMBIWA ETI ELIMU BURE

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Tena Nyerere alifanya vitu vingi sana vya maendeleo.
Nyerere ndiye kiongozi pekee aliyetoa elimu bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.
Alijenga viwanda vingi sana mfano ;
Urafiki, Mwatex, kilitex, musoma textiles Sunguratex Moroccans ,moproco mgololo paper mills Mbeya textiles, Twiga cement, Tanga cement na vingine vingi tu

Lakini kubwa zaidi anakumbukwa kama shujaa wa Afrika kwa kuitangazia dunia tulipovamiwa na Nduli IDD Amini, kuwa atampiga.
Akasema, sababu, uwezo na nia anayo na akampiga kweli kweli na kumwondoa madarakani.
Haijawahi kutokea katika historia ya Afrika Rais wa nchi kupigwa na nchi Jirani na kukimbia nchi.Huyu aliwaua RAIA wake zaidi ya 500000 na akavamia Ardhi yetu akaua wananchi wetu, akaharibu na kupora Mali.
Mwl.Nyerere aliwaomba OAU walaani uvamizi huo uliofanywa na nduli Amin waliposhindwa kufanya hivyo, kwa uongozi wake mahili, aliwaunganisha watanzania wote, waliokuwa mstari wa mbele vitani na waliokuwa wakiendelea na shughuri za kiuchumi kupambana kila mtu kwa nafasi yake, na akasema; vita hiyo lele mama,watanzania pambaneni kila MTU kadri ya nafasi yake.
na hatimae tukashinda vita hiyo ya kihistoria na kulejesha utu na heshima ya mtanzania kwenye sura ya dunia.
 
Back
Top Bottom