Kwanini Marais wengine wastaafu kama Mwl. Nyerere na wengine hawasifiwi kwa kujenga miundombinu?

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,806
4,370
Hivi kwanini Marais wengine wastaafu kama vile Mwl. Nyerere na wenzake waliomtangulia Rais Magufuli wao hawasifi kwa kujenga miundo mbinu?

Swali ni je Marais wastaafu wakiongozwa na Mwl. Nyerere wao hawakujenga miundo mbinu kama Rais wetu mpendwa wa awamu ya 5?

Kila mara anaposifia Rais wetu mpendwa wa awamu ya 5 Rais Magufuli watu wengi wanajikita katika ujenzi wa miundo mbinu.

Swali linalokuja kwa wananchi walio wengi ni je, mbona marais wengine waliopita wao hawasifiwi kwa kujenga miundo mbinu?
Mwenye jibu tafadhali tunaomba atusaidie.
 
Rais anapogombea huwa ana ilani ya Chama chake inayoonyesha nini atafanya akipata u-Rais. Na wananchi wanampa kura kwa kushindanisha ilani yake na ya washindani wengine.

Yule anaueshinda anajuwa ameajiriwa na wananchi kwa miaka 5 mpaka uchaguzi mwingine. Anapojenga madaraja, barabara anakuwa anatekeleza ilani kwa tafsiri nyingine anafanya kazi aliyotumwa na Mwajiri wake.

Rais mshamba na limbukeni ndiyo tu atafurahi kusifiwa lakini mwenye akili timamu hatopenda sifa.

Akina Nyerere, Mwinyi, Mkapa hata KIKWETE wamefanya mambo mengi makubwa Ila wanatambua ilikuwa ni wajibu wao. Ndiyo maana hawajawahi kubabaika na misifa.

Huyo Rais Mwendazake pamoja na kuwa Waziri miaka 20 na Rais miaka 5 ushamba haukuwahi kumtoka na amezikwa Chato na ushamba wake.
 
Baba wa Taifa alifanya mengi makubwa lakini husikii kokote kutaka sifa za kipuuzi za kujitapa wakati alikuwa anajua fika kwamba kama Rais alikuwa na wajibu wa kuleta umoja na mshikamano, kujenga uchumi bora hadi pale uchumi wa dunia ulipotetereka kwa bei ya mafuta kupanda sana, ukame uliosababisha njaa kubwa sana nchini na pia vita ya Kagera ambayo ilitumia akiba ya forex nyingi sana ili kumuondoa nduli madarakani. Pia alikuwa na mapenzi ya kweli kwa Tanzania na Watanzania na kuvijua vipaumbele vya Tanzania siyo kama huyo mtu wa chato.

Tatizo kuna wanasiasa hasa vijana wasiojua vyema historia ya Tanzania na watu wazima walioamua kujitoa ufahamu tu. Matokeo yake wanaishia kudemka tu badala ya kujadili mambo ya msingi.

Hayati Nyerere siyo tu alijenga reli ya uhuru, ya kisasa kabisa kwa wakati huo, toka Dar es salaam mpaka Kapirimposhi, bali pia alijenga mabwawa kadhaa ya kuzalisha umeme na gridi ya kuweka miundombinu ya kuusambaza umeme huo nchini. Hapo hatujaongelea viwanda mbalimbali ya kati vilivyojengwa sehemu mbalimbali nchini vikiongozwa na vile vya nguo. Lakini kubwa kuliko yote ni umoja wa kitaifa alioujenga na kuusimamia kwa nguvu zake zote. Na pia alikuwa kielelezo cha uadilifu kwa maraisi waliomfuatia na marais wa Afrika. Hapo hatujaongelea uongozi wake katika vita ya kuzikomboa nchi za kusini mwa Afrika zilizokuwa chini ya utawala wa kikoloni na kuifanya Tanzania kituo kikuu cha harakati za ukombozi. Ni yeye pekee ndiye mwenye sifa za kuitwa SHUJAA WA AFRIKA.

Mzee Mwinyi naye amefanya mambo makubwa ikiwemo uamuzi mgumu wa kuruhusu mfumo wa soko huria na kuuondoa mfumo wa uchumi wa dola uliojengwa wakati wa siasa ya Ujamaa na Kujitegemea kama ilivyoainishwa kwenye Azimio la Arusha. Kupitia azimio la Zanzibar Tanzania ilipitia mabadiliko makubwa ya kiuchumi yaliyowezesha mitaji binafsi kuingia nchini na kubadili mwelekeo wa nchi kiuchumi. Mzee Mwinyi pia ndiye aliyekuwa muasisi wa siasa za ushindani wa vyama vingi.

Hayati Mzee Mkapa kimsingi ndiye chief architect aliyesuka mikakati ya kutufikisha kwenye uchumi wa kati na alifanya maboresho mbali mbali ya kimfumo na kiutendaji ili kuwezesha Ndoto ya kufikia uchumi wa kati 2025 ifikiwe. Katika utawala wake ndiyo ile ndoto ya kuunganisha nchi kwa barabara za lami ilianza kutekelezwa na ninakumbuka vyema alipotoa ahadi ya kuunganisha Bukoba na mtwara kwa lami jinsi ilivyofanyika kazi kwa vitendo.

JK akiendeleza alipoishia Hayati Mzee Mkapa alisimamia miradi mingi sana ya ujenzi wa uchumi ambayo mingi imezinduliwa wakati wa Hayati Mzee Magufuli. Pengine Mzee JK ndiye Rais aliyeanzisha miradi ya ujenzi wa bararaba za lami zenye urefu mkubwa zaidi kuliko raisi mwingine yeyote kwenye historia ya nchi yetu. Miradi ambayo JK aliianzisha na kuisimamia ni pamoja na:
(i) Chuo Kikuu cha Dodoma
(ii) Jakaya Kikwete Cardiac Center Muhimbili
(iii) Ujenzi wa airport Terminal III
(iv) Kutekeleza mradi wa BRT ulioasisiwa na Hayati Mkapa
(v) Mradi wa Bomba la Gesi ya Asili toka Mtwara Mpaka Dar es salaam
(vi) Ujenzi wa shule za sekondari kila kata
(vii) Ujenzi wa barabara ya lami toka Tunduma - Katavi
(viii) Ujenzi wa barabara ya lami toka Ruvuma Mpaka Lindi
(ix) Ujenzi wa barabara ya lami toka Dodoma mpaka Babati
(x) Ujenzi wa daraja la Mfugale
(xi) Ujenzi wa ringroads kupunguza msongamano wa magari DSM
etc. to mentiom a few.

Anayesema hakuna kilichofanyika kabla ya Mwendazake ama haijui vyema historia ya nchi yetu au ni mjinga tu anayehitaji kuelimishwa kwa busara na upole.

Tata said!
 
Nyerere madarakani zaidi ya 20 years miundo mbinu aliorithi kwa wakoloni aliharibu ... Hana sifa nzuri zaidi ya mbaya kwa hiyo bora tukanyamaza
 
Aisee 🤔
Baba wa Taifa alifanya mengi makubwa lakini husikii kokote kutaka sifa za kipuuzi za kujitapa wakati alikuwa anajua fika kwamba kama Rais alikuwa na wajibu wa kuleta umoja na mshikamano, kujenga uchumi bora hadi pale uchumi wa dunia ulipotetereka kwa bei ya mafuta kupanda sana, ukame uliosababisha njaa kubwa sana nchini na pia vita ya Kagera ambayo ilitumia akiba ya forex nyingi sana ili kumuondoa nduli madarakani. Pia alikuwa na mapenzi ya kweli kwa Tanzania na Watanzania na kuvijua vipaumbele vya Tanzania siyo kama huyo mtu wa chato.

Hivi kwanini Marais wengine wastaafu kama vile Mwl. Nyerere na wenzake waliomtangulia Rais Magufuli wao hawasifi kwa kujenga miundo mbinu?

Swali ni je Marais wastaafu wakiongozwa na Mwl. Nyerere wao hawakujenga miundo mbinu kama Rais wetu mpendwa wa awamu ya 5?

Kila mara anaposifia Rais wetu mpendwa wa awamu ya 5 Rais Magufuli watu wengi wanajikita katika ujenzi wa miundo mbinu.

Swali linalokuja kwa wananchi walio wengi ni je, mbona marais wengine waliopita wao hawasifiwi kwa kujenga miundo mbinu?
Mwenye jibu tafadhali tunaomba atusaidie.
Tumetoka kwenye nchi ya wazandiki mda mfupi ulipita kazi ya kusifu na kuabudu ilikuwa kubwa kwhy upepo utajituliza wenyewe tu.
 
Aliyewabatiza Chadema nyumbu aliona mbali ni mijitu mijinga isiyojitambua kabisa
Nenda kwenye kaburi lake Mwendazake ukaendelee kuimba mapambio huku ukitajataja majina yake na kuendelea kulia kwa nguvu, waweza nawe ukamfuata huko 'anakotawala' malaika.
Hapa utakonda bure kwa kumkosa ulieaminishwa atatawala milele.
 
Nyerere madarakani zaidi ya 20 years miundo mbinu aliorithi kwa wakoloni aliharibu ... Hana sifa nzuri zaidi ya mbaya kwa hiyo bora tukanyamaza
Utoto unakusumbua au lack of information!

Hujui kwamba hujui au unajitoa ufahamu?

Nyerere alijenga reli ya Tazara.
Alijenga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Alijenga hospitali ya Muhimbiri.
Alijenga Mzumbe.
Alijenga vyuo vingi sana ambavyo leo vimebadilishwa kuwa vyuo vikuu.
Alinunua ndege nyingi tu.
Alijenga shule za sekondari nyingi ikiwemo Sengerema na ile ya Singida mjini,nimesahau jina lake.
Alijenga zaidi ya viwanda 400!

The list is endless!
 
Nyerere madarakani zaidi ya 20 years miundo mbinu aliorithi kwa wakoloni aliharibu ... Hana sifa nzuri zaidi ya mbaya kwa hiyo bora tukanyamaza
Au humjui Nyerere unasimuliwaga kwenye kahawa?

Nyerere alikuwa habari nyingine!

Alitoa huduma za afya bure.
Alitoa elimu bure kuanzia msingi mpaka chuo kikuu. ELIMU BURE, kwa uzito wake,kuanzia pen,daftari,vitabu na hata nauli ya kwenda na kurudi shule/chuo.
 
Hivi kwanini Marais wengine wastaafu kama vile Mwl. Nyerere na wenzake waliomtangulia Rais Magufuli wao hawasifi kwa kujenga miundo mbinu?

Swali ni je Marais wastaafu wakiongozwa na Mwl. Nyerere wao hawakujenga miundo mbinu kama Rais wetu mpendwa wa awamu ya 5?

Kila mara anaposifia Rais wetu mpendwa wa awamu ya 5 Rais Magufuli watu wengi wanajikita katika ujenzi wa miundo mbinu.

Swali linalokuja kwa wananchi walio wengi ni je, mbona marais wengine waliopita wao hawasifiwi kwa kujenga miundo mbinu?
Mwenye jibu tafadhali tunaomba atusaidie.
Simple...

Kwasababu hao wengine hawakuwa wasukuma....
 
Utoto unakusumbua au lack of information!

Hujui kwamba hujui au unajitoa ufahamu?

Nyerere alijenga reli ya Tazara.
Alijenga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Alijenga hospitali ya Muhimbiri.
Alijenga Mzumbe.
Alijenga vyuo vingi sana ambavyo leo vimebadilishwa kuwa vyuo vikuu.
Alinunua ndege nyingi tu.
Alijenga shule za sekondari nyingi ikiwemo Sengerema na ile ya Singida mjini,nimesahau jina lake.
Alijenga zaidi ya viwanda 400!

The list is endless!
Mitoto ya usukumani iliyozaliwa miaka ya 90 haioni aibu kumlinganisha mwizi Meko na mzalendo Nyerere...
 
Back
Top Bottom