Ameacha legacy ambayo siyo ya kulazimisha "eti ooh legacy legacy ya mwendazake". Huyu kaacha legacy ambayo ipo tu. Halafu akatokea mtu mmoja akaviua viwanda vyote kwa decision ya ajabu!!!! Naumia sana nikikumbuka viwanda vilivyokuwepo halafu vikauliwa overnight kwa kisingizio cha ubinafsishaji!!! Kuna mashirika kama NBC, TBL, TTCL nk. hayakuwahi kuregister hasara lakini hesabu zikapikwa kuonyesha yana hasara ili yachukuliwe na so called investors!!! Hao investors kwanini wasianzishe vitu vyao? Nakumbuka eulogy ya Madeline Albright kwa late J.K. Nyerere ilivyokuwa nzuri sana!!!Nyerere ndiye kiongozi pekee aliyetoa elimu bure kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.
Alijenga viwanda vingi sana mfano ;
Urafiki, Mwatex, kilitex, musoma textiles Sunguratex Moroccans ,moproco mgololo paper mills Mbeya textiles, Twiga cement, Tanga cement na vingine vingi tu
Lakini kubwa zaidi anakumbukwa kama shujaa wa Afrika kwa kuitangazia dunia tulipovamiwa na Nduli IDD Amini, kuwa atampiga.
Akasema, sababu, uwezo na nia anayo na akampiga kweli kweli na kumwondoa madarakani.
Haijawahi kutokea katika historia ya Afrika Rais wa nchi kupigwa na nchi Jirani na kukimbia nchi.Huyu aliwaua RAIA wake zaidi ya 500000 na akavamia Ardhi yetu akaua wananchi wetu, akaharibu na kupora Mali.
Mwl.Nyerere aliwaomba OAU walaani uvamizi huo uliofanywa na nduli Amin waliposhindwa kufanya hivyo, kwa uongozi wake mahili, aliwaunganisha watanzania wote, waliokuwa mstari wa mbele vitani na waliokuwa wakiendelea na shughuri za kiuchumi kupambana kila mtu kwa nafasi yake, na akasema; vita hiyo lele mama,watanzania pambaneni kila MTU kadri ya nafasi yake.
na hatimae tukashinda vita hiyo ya kihistoria na kulejesha utu na heshima ya mtanzania kwenye sura ya dunia.