Kwanini majina ya Mjimwema, Gezaulole na Majengo yanapatikana katika mikoa mingi hapa Tanzania?

Brightg

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
373
660
Wadau haya majina kama MAJENGO, GEZAULOLE, MJIMWEMA yapo karibia mikoa mingi.

Historia ya nchi kuamua kutoa haya majina ikoje na kwa sababu gani? Inamaana hakukuwepo na majina mengine? Mikoa ambayo yana majina hayo ni Mwanza, Kigoma, Wilaya ya Hai. Utakuta mkoa au wilaya ina majina yote 3 au 2 au 1.

Wenye historia watujuze
 
Ni kweli ila binafsi hamna jina nalipenda kama MAJENGO. Yaani sehemu ikiitwa Majengo huwa naipenda sana sijui kwa nini. Kule Babati Manyara karibu na mahakama ya wilaya kuna mtaa unaitwa Old Majengo na kuna mwingine huko mbele unaitwa Majengo. Yaani Majengo kila mahali nchi hii.

Kuna sehemu nina kiwanja hakujajengeka badonataka nifanye kila namna niwashawishi watu waukubali mtaa wetu uitwe Majengo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kigoma majengo ni mtaa mkogwe uliojaa malaya na tabia za hovyo

Mjimwema huku ni pakishua

Gezaulole huku wanakaa walalahoi

Note
Nimetumia experience ya mkoa wa kigoma
MAJENGO-kuna baadhi ya mitaa huwa na majengo mengi na mazuri kuliko mingine
MJI MWEMA-ni jina tu la waswahili ku describe kwamba huo mtaa una usalama au umetulia
GEZA ULOLE-hii niliikuta Songea tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Geita kuna kariakoo na manzese, posta bado sijasikia.Ila mtaa uitwao Songambele na Kilimahewa.
Hiyo mitaa ipo mikoa lukuki.
 
Geita kuna kariakoo na manzese, posta bado sijasikia.Ila mtaa uitwao Songambele na Kilimahewa.
Hiyo mitaa ipo mikoa lukuki.
Watanzania tunarudia majina ya mitaa,wazungu wao kuna mtaa walikaa kujadili jina la kuupa muafaka ukakosekana,mmoja akasema why not name it why not,basi mtaa ukaitwa WHY NOT mpaka leo
 
Kwa kuongezea Mji mpya Soweto, Mabatini
Mji Mpya - Morogoro
Mji Mpya - Mpwapwa
Kaloleni - Morogoro
Kaloleni - Arusha
Chamwino -Morogoro
Chamwino - Dodoma
Manzese - Dsm
Manzese - Morogoro
Boma Rd - Morogoro, Ilala Boma - Dsm, Bomani - Ifakara!
 
now day ukiwa na kazi ya kuingiza buku tano kwa siku mademu wa ujiji wanakufata muishi wote kama mke na mume

ujiji kujenga national housing hapana kuna uswahili saaana
dah!!ujiji nakumbuka mida ya jioni ka giza giza watu wanatafutana kuchakatana,lakini ujiji nadhani inge boreshwa pajengwe majengo ya serikali ya National Housing

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom