muonamambo
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 875
- 545
Wanabodi kuuliza si ujinga nataka kupata kufahamu tu. Najua kuna Mihimili mitatu kwa Maana ya Bunge , Mahakama na Serikali.
Na naambiwa mihimili hii ina Nguvu sawa na kujitegemea.
Nimeona wateule wa Serikali wanateuliwa na Rais na kuapa kwa Rais.
Naona Wabunge wanaochaguliwa na wananchi wanaapa kwa Spika wa Bunge.
Swali sasa kwa nini majaji wateuliwe na Rais? Je kwa nini waape kwa Rais, wakati wapo kwenye Muhimili wa Mahakama?
Je huku si kusema kuwa ni Bunge pekee ambalo labda liko huru kidogo maana wabunge hawapaswi kuapa mbele ya Rais.?
Je, huku ni kusema kuwa Mahakama haiko huru maana Watendaji wake wanateuliwa na Rais na kuapa kwa Rais?
Nauliza tu waungwana maana hii inanichanganya?
Michango ya Wadau

Naomba nikujibu kwa msingi ya utawala na sio kisheria.
Tanzania kama ilivyo Marekani, Rais ana-play role ya mkuu wa nchi. Kwa kofia ya Ukuu wa nchi, anakua na madaraka ya kuteua na kuongoza kiapo cha utii kwa majaji.
Uingereza (The United Kingdom) majaji wanateuliwa na Malkia au Mfalime. Waziri mkuu (amabe ni mkuu wa serikali) anawajibika kumshauri Malkia nani wa kumteua akishirikiana na tume ya utumishi wa mahakama.
Ujerumani, jaji mkuu anakula kiapo mbela ya Rais wa Germany Federation (na sio Chancellor ambae ni mkuu wa serikali)
Israeli pia, majina ya majaji wanapendekezwa na tume ya kijaji (Judicial Nomination Committee). Anaewateua na Rais wa Israel ambae ni mkuu wa nchi.
Kwa kifupi sana, Tanzania, Rais kwa kofia yake ya Ukuu wa Nchi, katiba inampa nguvu ya kisheria na kiutawala kuchagua/kuteua majaji na kuwaongoza kula kiapo cha utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Niko tarari kukosolewa na kupata ufahamu zaidi toka kwa "wasomi na mawakili"