Kwanini Mahotelini hakuna nyama ya Bata?

Kwanini Mahotelini hakuna nyama ya Bata?

lukelo sakafu

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2015
Posts
2,938
Reaction score
517
Kuna kitu kinanichanganya sana.Nimetembea katika hoteli ni migahawa mbalimbali ndani na nje ya nchi lakini sijawahi kukuta nyama ya bata inauzwa. mfano - CHIPS BATA,WALI BATA UGALI BATA, lakini zimejaa nyama za kuku tu. Je, kwanini hatupendi kula nyama ya bata kama kuku?

Je, siyo tamu,ni gharama?

Jamani karibuni tujuzane.
 
Bata mbona wapo wengi tu, sema beiyao ndio iko juu ukilinganisha na kuku, minikiwa na hamu nae navunja kibubu namnunua namchinja namuandaa vizuuuuri kisha namtafuna nyama lainiiiiii.
 
Bata bei ni ghali sana pia wanahitaji maandalizi ya umakini mkubwa wakati Wa kumuanda LA sivyo utawatapisha watu
 
kuna kitu kinanichanganya sana jamani nimetembea katika hoteli ni migahawa mbalimbali ndani na nje ya nchi lakini sijawahi kukuta nyama ya bata inauzwa mfano. CHIPS BATA,WALI BATA UGALI BATA, lakini zimejaa nyama za kuku tu. je kwa nini hatupendi kula nyama ya bata kama kuku? je siyo tamu,ni gharama? jamani karibuni tujuzane
Sema umetembelea vijiwe vyote vya mama ntilie.... na usitudanganye kuwa wewe ni mtu wa ''hoteli za ndani na nje ya nchi''.
 
Mbona kila siku watu wanakula Bata. Hujawahi kusikia mtu anakwambia nipo sehemu fulani nakula Bata
 
Mkuu bata ni mtamu sana ila ujue kumuandaa tena kwa utulivu snaa
Alafu bata ana nyama nyingi tofauti na kuku

Ni kweli kama hajaandaliwa unaweza usitamani kumla maishani maana ana shombo la samaki mtoto
 
Back
Top Bottom