Kwanini maheadmaster/ headmistress hawafundishi darasni? ijue sababu

makwaru

Member
Joined
Jun 11, 2013
Posts
6
Reaction score
1
tatizo kubwa hapa wakuu wa shule wanajihita managers/wakurugenzi na si walimu. na wamesahau kuwa wanalipwa mishahara kwa cheo cha ualimu na si utawala. wanashindwa kufundisha na ndio maana wanashindwa kusimamia ufundishaji mashuleni.
na ndio maana elimu inashuka nchini.
 
hv wewe nani kakwambia head masterz/minstres huwa hawafundish nani? Alafu jua kuwa co wakuu wote wa shule wamesoma education wengne wamesoma administration kama ulikua hujui kaa humo.
Then laiti ungejua kaz za hawa wakuu wa shule ungewaonea huruma.

Swali? Je wajua ni kwa nn wale wa primary wanaitwa Head teaches-(walmu wakuu) na wale wa secondary wanaitwa head-masters/mistres wakuu wa shule?
 
Sio wote wasiofundisha,wengi wanafundisha tena masomo yao waliyosomea na sio civics.
 
mpale steve, acha uongo na upuuzi, wengi wa wakuu wa shule lazima watokane na walimu, si kweli kwamba wale wakuu hawafundishi eti kwa kuwa wamesomea administration. wakuu wa shule wengi ni uamuzi wao kuamua kutofundisha, na ni makosa wanayoyafanya...
 
tatizo kubwa hapa wakuu wa shule wanajihita managers/wakurugenzi na si walimu. na wamesahau kuwa wanalipwa mishahara kwa cheo cha ualimu na si utawala. wanashindwa kufundisha na ndio maana wanashindwa kusimamia ufundishaji mashuleni.
na ndio maana elimu inashuka nchini.

Hivi unafikiri kazi wanazofanya Ofisini ni ndogo, amini nakwambia wanatamani sana kupiga story na wanafunzi darasani, tatizo majukumu ni mengi mno. Nakumbuka wakati tuko O-Level tulikuwa tunafundishwa na Headmaster, somo la Biology; Yule mzee alikuwa vizuri mno lakini huwezi amini tulipeleka maombi kwa mwalimu wa Taaluma tubadilishiwe mwalimu, tatizo ilikuwa akiwa darasani somo limekolea mara anakuja kuitwa kuna wageni wa muhimu ofisini, akienda anakaa mpaka muda wa kipindi unakwisha! Pia kutokana na majukumu yao wanakuwa na safari nyingi mno kiasi kwamba mkifundishwa na HM atahudhuria darasani chini ya asilimia 30 ya muda anotakiwa kufundisha, hapo ni kufeli tu! Mara nyingi wanafunzi wanaona ni kama hafanyi kazi vile "amekaa tu ofisini", jaribu tu kufuatilia idadi ya wageni anaopokea na kuhudumia ndani ya siku utashangaa! Utamkuta mpaka saa6 yuko ofisini wakati huo waalimu wa kawaida wamelala na wake zao!
Hebu jaribu kudadisi kwa watu walio ndani ya mfumo wa Elimu, iwe Afisa ELimu au watu wengine watakufafanulia MAJUKUMU YA HEADMASTER!!

Binafsi wakati niko shuleni nilikuwa nawaogoopa na kuwachukia sana hawa HEADMASTERS, lakini baada ya kukua nawaheshimu sana hawa wazee, na najua mengi waliyokuwa wananifanyia ambayo mimi niliona kama wananinyanyasa walikuwa wananitakia mema. Shukrani sana zimwendee HM wangu wa O-Level Mr M, na A-Level Mzee wa Miwani aka Shetani, without you i wouldnt be here now! Nakumbuka Nilifanya ukorofi na kukaa nyumbani kama miezi sita hivi nilivyokuja kufanya paper Master aliniita na kuniambia niahirishe mwaka, and i said NO, TRUST ME, I WONT LET YOU DOWN!..kweli skumlet down, i did wonders mpaka nikawa subject for years hapo shuleni.
I LOVE YOU TEACHERS, THOUGH I WONT LET MY SON BE A TEACHER....HE'D BETTER BE A FARMER!
 
umetoa maelezo mazuri sn,wakuu wa shule sio kweli kwamba wote hawafundishi!,sasa km shule yake ina walimu wa kutosha kwanini na yeye ajitese kufundisha?

Wakuu wa shule wana majukumu mengi sn km ulivyoainisha ndugu yangu,na ni kweli endapo wanakua na masomo ya kufundisha basi hawawez kumaliza topics zote kwa wakati muafaka kwakua wana safari nyingi na vikao vya utendaji vingi mno!

Mwisho,umesema hutoruhusu wanao wawe walim ni bora wawe wakulima,je kila mmoja akiwa na mtazamo hasi juu ya fani ya ualim km ulivyo ww,watoto wetu watafundishwa na nani????
 
Tatizo serikali haijaipa kipaumbele fani ya ualimu, sitafurahi kijana wangu akifundisha kwa juhudi kubwa bila maendeleo yoyote binafsi! Seikali itimize wajibu wake, mambo ya ualimu ni wito yalishapitwa na wakati!
 
mpale steve, acha uongo na upuuzi, wengi wa wakuu wa shule lazima watokane na walimu, si kweli kwamba wale wakuu hawafundishi eti kwa kuwa wamesomea administration. wakuu wa shule wengi ni uamuzi wao kuamua kutofundisha, na ni makosa wanayoyafanya...

mimi ni mwalimu na headmaster wetu hafundishi kwa kuwa amesoma uongoz katika masuala ya elmu upo hapo??
 
Tatizo serikali haijaipa kipaumbele fani ya ualimu, sitafurahi kijana wangu akifundisha kwa juhudi kubwa bila maendeleo yoyote binafsi! Seikali itimize wajibu wake, mambo ya ualimu ni wito yalishapitwa na wakati!
"Ualimu ni wito" hayajapitwa na wakati ndugu yangu. Msemo huo unahitajika sasa kuliko wakati mwingine wowote kwa Tz. Tatizo watu wengi wanaunasibisha msemo huo na ualimu bila malipo/malipo madogo, noooooo. "WITO" ni ile hali ya kusukumwa ndani yako kufanya jambo fulani (ualimu kwa mjadala wetu) kwa kujali mahitaji ya wateja (wanafunzi katika mjadala huu). Ishu ni je walimu wa sasa wanawito?
 
hakuna maelezo yakutosha hapo!
mi Mwalimu
ualimu sio wito kama wengi wanavyodhan,ualimu nikazi kama kazi nyingine na mshahara kiasi fulan unakidh mahitaji kulingana na sehem fulani tatizo walimu wengi wanaifananisha mishahara yao na sekta nyingine flani flan ndo kama vile benk ndo wanakuja najibu kuwa ualimu unamshahara mdogo! ujasiliamali nikitu muhm kwa mwalimu ili kujikomoa na umaskini! nahasa serikali yetu inapoziba masikio kwa kilio cha walimu!, Istoshe zamani ualimu ulikuwa laisi sana kuupata kwan watu walikuwa hawautaki na ndo jina la ualimu wito lilianzia hapo! kipindi hiki vijana wengi wanalilia na hawaupati ushahidi ninao pale CHUO CHA UALIMU MOROGORO
 
Ualimu ni Taaluma bana!
 
Ndugu yangu, kujuwa kwetu kunatofautiana katika kupokea taarifa na katika kuwasilisha. Ninakubaliana na wewe kuwa ualimu ni kazi kama kazi nyingine (soma tene maelezo yangu). Hata udaktari ni "wito", vivyo hivyo uaskari, uuguzi, uandishi wa habari, n.k. Ukiwa na WITO katika taaluma yako utafanya zaidi ya job description. Vinginevyo tunakuwa na walimu wa tuition na udanganyifu katika mitihani na mapenzi na wanafunzi wao. Bila wito tunapata polisi majambazi na wafanya magendo. Bila wito tunapata wanahabari wa bahasha na wapakaziaji. Bila wito tunapata bankers wezi na wefanya madili haramu.
Suala la kipato silipingi, hata mishahara ikipanda vipi au walimu wawe wajasiliamali kama Mengi, bila wito tutapata form four leavers wasiojua kusoma na kuandika. Polisi bila wito ndiyo maana hakuna upelelezi wa kina katika case zenye manufaa kwa umma. Muuguzi bila wito wagonjwa wanajigonga kwenye vitanda wakijikongoja kwenda chooni huku wauuguzi wakipiga soga mbele yao.
WITO ni msingi wa weledi kwenye kazi/taaluma zetu
 
Suala la Mkuu wa shule kufundisha lipo pamoja na majukumu mengine wanayokuwa nayo mathalani kiongozi cha mkuu wa shule kinaonesha kutaka mkuu wa shule afundishe vipindi vichache mno kwa wiki (4)ili apate muda wa kutosha kufanya shughuli nyingine za kiutawala akiwa shuleni na kama Mkuu hafundishi kabisa huyo atakuwa amesomea utawala tu kama mchangiaji wa awali alivyosema au ni aina ya wakuu wapuuzi wanaoona ukuu wa shule ni ahera
 
Back
Top Bottom