Kwanini Magazeti ya kenya?

Kwanini Magazeti ya kenya?

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,292
Reaction score
6,768
Yana matangazo mengi ya biashara kuliko haya ya kwetu?

FIKRA ZANGU:
  1. Makampuni mengi ya Kenya yanalipa kodi hivyo hayaogopi kujitangaza.
  2. Makampuni yetu yanakwepa kodi. Naombeni mawazo yenu.
 
Wao wenzetu wanatangaza bidhaa zao wanaweka bei.Na wana bei ya punguzo baada ya mda kupita na vitu vyao vina garantee ya mwaka na kulenndelea sisi kwetu ukinunua bidhaa kwenye risti chini ukakutana na neno Mali ikishanunuli harudiswi huu ni unyanyashaji kwa vile wanajua vitu wanavyouza havina ubora.Magazeti yetu yamejaa matangazo ya waganga wa kienyeji.
 
Kuna mada humu jukwaani ilikua inaelezea jambo la ukitaka kuijua nchi vizuri na raia wake, Sikiliza redio zao na Soma magazeti yao utawajua ni watu wa aina gani. WATANZANIA, ni vichwa vya habari tu hatusomi kilichomo ndani ya Gazeti sasa sidhani kama kuna biashara ingependa ijitangaze ndani ya gazeti linalosomwa ukurasa wa mwanzo tu. Labda habari iwe inahusu mchawi aliyekamatwa akiwanga uchi.
 
pia magazeti yao yanasomwa sana na watu,huku kwetu kiwango cha watu kusoma ni kidogo sana na hiii inasababishwa na mambo mengi ,baadhi ni uwezo wa kifedha wa watanzania kununua magazeti kila siku,baadhi ya watanzania hawajui kusoma na kuandika,ubora wa magazeti yenyewe ni mdogo mfano gazeti linaandika habari ya uongo ukurasa wa mbele kama Tyson abadili jinsia kwa vyovyote mtu huwezi kupoteza fedha yako kununua gazeti kama hilo,kwa kifupi magazeti mengi ya Tanzania ubora wa kile kinachoandikwa ni mdogo.

Watangazaji wa matangazo nao wanaangalia vitu vingi mojawapo ni watu wangapi wanasoma magazeti.
 
Wenzetu wameendelea kuliko sisi. Period! Nashauri tuendelee na porojo siasa na maneno mengi LABDA tunaweza kutoka kwa style hiyo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Magazeti mengi ya tz ni kama vipeperushi maana mengi ya kurasa chache sana, alafu pia kwa ubora bado tuko nyuma.

Simaanishi kuwa magazeti yote bali maana yapo magazeti yenye viwango, pia pamoja na kipato cha watanzania kuwa kidogo lakini tukubaliane kwamba watz tulio wengi hatuna tabia ya kusoma magazeti hata vitabu, kwa mwenye tabia ya kusoma kama budget yake imekaa vibaya anaweza asinywe chai au lunch ili mradi apate gazeti.

Wakenya ni watu tu kama sisi ni suala la kubadilika tu.
 
Magazeti mengi pamoja na vyombo vingine vya habari vya tz viko biased, vinafanya kazi kulingana na matakwa ya mmiliki ndo maana hata km habari ni nzuri haiwezi kuandikwa km inakinzana na matakwa ya mmiliki. Hata tangazo litatafuta gazeti lenye mlengo mmoja na mtoa tangazo!!
 
Dah, michango yenu ni mizuri sana.
 
Magezeti mengi ya Tanzania hayana maana,yamejaa uwongo na propaganda.Kuna facts nyingi lakini wao hawataki kuandika.Pia waandishi wanaendekeza njaa wananunuliwa hovyohovyo.Mwandishi yuko tayari kuandika habari ya kumchafua mtu kisa kapewa pesa.Taalum ni yakwako lakini mwandishi wa kitanzania kwa maksudi anakubali kutumiwa,ni ujinga mtupu.Watalalamika siku zote,vinginevyo wajirekebishe.Binafsi naishia tu kusoma na kusikiliza vichwa vya habari na kuwaenjoy waandishi uchwara kama mkapa alivyokuwa akiwaita

Halafu ukichunguza kwa umakini magezeti mengi uandishi wake unaweza ukasema yana haririwa na mtu mmoja.Yes,huo ndiyo ukweli.Huwa nachunguza kwa umakini sana magezeti mengi yanarudi.Si kweli kwamba watu hawana hela,angalia kwenye kumbi za starehe,angalia watu wanavyochangamkia bidhaa zingine.Mtu hawezi kutoa 500 au 1000 yake kisha asome habari iliyopikwa.Haya unapeleka sehemu copy 100,hata haziishi hakuna kitu hapa,watu wanaona bora wanunue magazeti ya udaku na michezo kuliko haya yanayojita ya siasa na uchambuzi.
.Kwa maksudi niliamua ninunue pc yangu ili nijitafutie mwenyewe habari,siko tayari kulishwa -----.
 
Mkuu we ushangai kiu ijumaa risasi (magazeti ya maudaku) ndo yanaongoza kwa mauzo. Kenya Hakuna kitu hicho. Yaani ukute mkenya aache kununua nation, standard anunue kiu au ijumaa??

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Yana matangazo mengi ya biashara kuliko haya ya kwetu?

FIKRA ZANGU:
  1. Makampuni mengi ya Kenya yanalipa kodi hivyo hayaogopi kujitangaza.
  2. Makampuni yetu yanakwepa kodi. Naombeni mawazo yenu.

Unampango wa kuanzisha Gazeti???? usirogwe ukidhani wafanyabiashara watakuja tangaza biashara zao humo. Ukitaka likulipe we jikite kwenye UMBEYA KAMILI. Watanzania wamechoshwa na umaskini hivyo huona bora wasome UDAKU wajiburudishe. Suala la makampuni kukwepa kodi hilo pigia mstari na ujiulize hayo makampuni ni ya akina nani!
 
Watanzania mna mambo kweli, the grass is always greener at the other side of the fence but not until you get to see the water bills.
 
matangazo yaliyopo kwenye magazeti yetu ni ya kuongeza nguvu za kiume,na ya uganga uganga,mara kujiunga na free===son,lakin magazeti ya kenya na uganda kuna matangazo ya kila aina na yako mengi sana,
 
matangazo yaliyopo kwenye magazeti yetu ni ya kuongeza nguvu za kiume,na ya uganga uganga,mara kujiunga na free===son,lakin magazeti ya kenya na uganda kuna matangazo ya kila aina na yako mengi sana,

Redpaper

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Magazeti ya KENYA yako kibiashara zaidi ilhali haya ya TANZANIA yako kisiasa, kimbea na kishirikina zaidi
 
...michango ya wadau iko sawa kabisa..ila pia Kenya wameanza ushindani wa kibiashara siku nyingi sana..na wana Advertsing Agency nyingi sana....
 
Back
Top Bottom