Kwanini mabasi ya Kilimanjaro Express hayashushi abiria Ubungo bus terminal?

fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,902
2,396
Wadau,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza.

Nashindwa kuelewa ni utaratibu gani unaotumiwa na kampuni hii ya usafirishaji abiria kutoingia pale stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani Ubungo na badala yake wao wakitokea na mikoani wanapitiliza mpaka eneo la Shekilango ilipo stendi yao.

Ikumbukwe kuwa hili suala linaleta usumbufu kwa abiria mfano anaekaa Buguruni itampasa kutembea kutoka Shekilango mpaka darajani Ubungo kupanda daladala za Buguruni.

Kwa anaefahamu kuhusu huu utaratibu wao naomba atujuze je inakubalika hiyo hali?
 
By the way pole,na kupanga ni kuchagua baada ya hayo mawili kubali matokeo
 
Ni utaratibu wao waliojiwekea kuwa na vituo vyao binafsi, maana hata mikoa wanayotoa huduma kupakia na kushusha abiria huwa wanafanya kwenye vituo vyao mfano Arusha na Moshi, hivyo ukipanda magari yao inabidi ukubaliane na masharti yao pia
 
Vipi kuhusu kupakia abiria, napo hawaingii ubungo bus terminal??
 
Ni utaratibu wao waliojiwekea kuwa na vituo vyao binafsi, maana hata mikoa wanayotoa huduma kupakia na kushusha abiria huwa wanafanya kwenye vituo vyao mfano Arusha na Moshi, hivyo ukipanda magari yao inabidi ukubaliane na masharti yao pia
ushuru wanalipia wapi?
 
Mkuu mtoa mada si ni bora hilo la kilimanjaro kwasababu unachagua meebyeee either kupanda hilo bus au lah. Kuliko mtu ukitokea maeneo ya buguruni ukiwa kwenye daladala kituo cha mwisho ni riverside unatembea na mizigo yako tokea riverside mpaka stand ya mkoa.
 
Hahaaa hlo nalo neno
 
Duuu...sikujua aseee
 
Back
Top Bottom