Kwanini Lowassa anawapoteza vijana CHADEMA?

Ufisadi ufisadi pesa zinazoliwa kupitia ufisadi zingeweza kununua dawa
Kwahiyo Lowassa amekula fedha za kununulia madawa maana hakuna dawa mahospitalini? Kuna mahali sisi wananchi tumeruhusu kuchezewa akili. Hivi wewe Mkuu Technically, unaamini kwamba ajenda kuu ya taifa hili ni ufisadi na fisadi ni Lowassa? Huyu Mzee alijiuzulu kwa kashfa ya Richmond toka mwaka 2008. Sasa kama wewe na mimi tuna uchungu kweli na tunapiga vita ufisadi, hebu tupeane muda halafu turudi hapa tukiwa na orodha ya kashfa za ufisadi toka mwaka huo hadi leo tunapohadili. Halafu kashfa hizo tuone kama zinamhusisha nani. Na mwisho tuje na majibu ya ni kwanini serikali inayochukia ufisadi haimpeleki Lowassa mahakamani kwa ufisadi.

Napendekeza hivyo kwa sababu nimekuwa nikitafakari na kupata wazo kuwa, serikali na CCM zinalitumia vibaya jina la Lowassa, na kadri nyie akina Technically mnaponasa katika propaganda zao ndipo serikali na CCM wanapopata fursa ya kufunika ufisadi mkubwa zaidi ambao unaendelea kulitafuna taifa hili zaidi ya miaka minane tangu Lowassa aondoke serikalini. Nimeona asubuhi umeandika "kutopelekwa mahakamani kwa Lowassa hakumfanyi awe msafi", come on..sasa kwa hoja hiyo hiyo wewe unapata wapi msukumo wa kuendelea kumwita Lowassa kuwa ni fisadi wakati chombo pekee kinachopaswa kuthibitisha ufisadi wake ni mahakama, ambako serikali ya CCM inashindwa kumpeleka?

Jiulize jambo hili: CCM sasa hivi hawamwiti Lowassa kuwa ni fisadi, umemsoma mzee Kinana akisisitiza tu kuwa Lowassa ni rafiki yake, huwasikii akina Mwakyembe wakisema kuwa Lowassa ni fisadi. Lakini subiri mwaka 2020! Sasa kwanini unakubali kuingia mkenge wa kutumika kwa gharama ya kulinda ufisadi mkubwa unaoendelea?
 
Mi uwa nashaanga eti kwanini ajapelekwa mahakamani.....

Kutopelekwa mahakamani sio kigezo pekee cha kukufanya uwe msafi........

Vijana wanaumia wanashindwa hata jinsi ya kutetea chama Kwa sababu ya mtu
Kigezo ni nini?
 
Mpaka kuwafunika wapigania chama kama wakina Mwalimu.

Mpaka kuwapoteza wakina Wenje wamekosa nguvu ya kupambana na kutetea wananchi.

Baada chadema impe cheo mtu kama Vincent Nyerere wao wanaangaika na mtu ambaye ana makando kando ya ufisadi.

Timu ya vijana kama Vincent Nyerere,Wenje,Kiwia wangeweza kujenga chama maana hawapo bungeni lakini sio Lowassa huyo ninayemjua.

Hivi toka lini Lowassa na &com aliowaacha ccm wameacha ufisadi?

Lowassa apumzike na yeye asiwe muongo na mtu wa kubadilika alituhaidi mwenyewe kuwa akishindwa uchaguzi ataenda kuchunga ngombe .

Sasa mtu ambaye anashindwa kutimiza tu ahadi ndogo kama hii anawezaje kuaminiwa kupewa nchi?..

Lazima tuambiane ukweli kuwa mtu kutopelekwa mahakamani sio kigezo cha kutokuwa fisadi.

Acha vijana wanaoaminika wafanye Kazi .
Angeacha siasa Leo wewe ungeandika nini?
 
Kwani suala la kujenga chama ni la viongozi tu! Lowasa ni Mjumbe tu wa Kamati kuu ya chama, lakini ana haki ya kukijenga chama kama Mwanachadema yeyote yule.
 
Kwahiyo Lowassa amekula fedha za kununulia madawa maana hakuna dawa mahospitalini? Kuna mahali sisi wananchi tumeruhusu kuchezewa akili. Hivi wewe Mkuu Technically, unaamini kwamba ajenda kuu ya taifa hili ni ufisadi na fisadi ni Lowassa? Huyu Mzee alijiuzulu kwa kashfa ya Richmond toka mwaka 2008. Sasa kama wewe na mimi tuna uchungu kweli na tunapiga vita ufisadi, hebu tupeane muda halafu turudi hapa tukiwa na orodha ya kashfa za ufisadi toka mwaka huo hadi leo tunapohadili. Halafu kashfa hizo tuone kama zinamhusisha nani. Na mwisho tuje na majibu ya ni kwanini serikali inayochukia ufisadi haimpeleki Lowassa mahakamani kwa ufisadi.

Napendekeza hivyo kwa sababu nimekuwa nikitafakari na kupata wazo kuwa, serikali na CCM zinalitumia vibaya jina la Lowassa, na kadri nyie akina Technically mnaponasa katika propaganda zao ndipo serikali na CCM wanapopata fursa ya kufunika ufisadi mkubwa zaidi ambao unaendelea kulitafuna taifa hili zaidi ya miaka minane tangu Lowassa aondoke serikalini. Nimeona asubuhi umeandika "kutopelekwa mahakamani kwa Lowassa hakumfanyi awe msafi", come on..sasa kwa hoja hiyo hiyo wewe unapata wapi msukumo wa kuendelea kumwita Lowassa kuwa ni fisadi wakati chombo pekee kinachopaswa kuthibitisha ufisadi wake ni mahakama, ambako serikali ya CCM inashindwa kumpeleka?

Jiulize jambo hili: CCM sasa hivi hawamwiti Lowassa kuwa ni fisadi, umemsoma mzee Kinana akisisitiza tu kuwa Lowassa ni rafiki yake, huwasikii akina Mwakyembe wakisema kuwa Lowassa ni fisadi. Lakini subiri mwaka 2020! Sasa kwanini unakubali kuingia mkenge wa kutumika kwa gharama ya kulinda ufisadi mkubwa unaoendelea?
Tatizo lililopo ni kuwa Chenge,Kikwete, Mkapa na Lowassa,Karamagi na yule aliyestaafu siasa Tabora ndio mafisadi wakubwa wa nchi hii.

Tatizo kubwa ni kuwa uwezi uwezi shugulikia mtu mmoja ukaacha wengine lazima washugulikiwe wote....

Na ukitaka kuwashuguliki wao katiba inawalinda wawili.....

Swali linakuja je kwanini mtu tuliyemuita fisadi miaka 8 Leo kawa msafi?......

Kwanini tumeondoa List of shame kwenye website ya chama?......

Kwanini mtu aliyekataa katiba bora ya Warioba ndiye leo awe mwana mabadiliko wakati alikataa katiba ya kuondoa kinga ya kushitakiwa kwa marais wastaafu?.............

Kama ndio huyu ambaye tunampigania....

Very shame.....
 
Nashanga bado unamawazo kama hayo sijawahi sikia mtu anashinda urais lakini anasambaratishwa kwa wabunge (67%ccm ) na kwa madiwani ( zaidi 70% ccm) .
Na hiyo ndio sababu ya kushindwa kwenyewe lakini kwa kura alishinda vizuri tuu alikosa uungwaji mkono wa wabunge wengi waliokuwa bado wanakubalika majimboni kupitia ccm naamini 2020 pengo hilo litazibika tuu.
 
Msitegemee kuwa LOWASSA atakuja kuwa Rais wa nchi hii. Tafuteni mtu mwingine atakayeweza kukiwakilisha vyema chama. Akisimama Lowassa, mjue wazi kuwa mtashindwa. Lowassa tayari ameshaanza kutoa pongezi nyingi kwa mh.Rais Magufuli. Kwa hiyo image ya Chadema ndiyo hivyo inaondoka. Msemaji wa chama amebaki mtu mmoja tu Lowassa wakati kweli chama kilikuwa na vijana na wazee wengi tu wenye uwezo wa kujenga hoja na ambao walipambana hadi kuijenga Chadema kuwa imara. Tuliondoka ndani ya Chadema kutokana na ujanjaujanja wa mwenyekiti kubadiri gia angani. Tuliondoka tukiwa tumesononeka sana kutokana na ujio wa Lowassa ndani ya chama.
Ulistahili kuondoka maana huelewi maaana ya taasisi unafikiri cdm ni mtu mmoja tuu lakini unasahau kuna kura zaidi ya six millions hiyo ndio taasisi na majina yote yatakuja yatapita lakini cdm itabaki, na uchaguzi uliopita mgombea wetu alikuwa Lowassa na alifanya vizuri sana! Na bado tunasonga mbele kuonyesha uwezo wa kuiondoa sisiem madarakani tuifanye nchi isiyo na mfumo wa kifisadi wala isobagua wakupambana na kuwachukulia hatua.
 
Back
Top Bottom