Kwanini Lowassa anatolewa Sadaka?

Kikwete kuwa fisadi hakumfanyi Lowassa msafi. Hivyo anastahili anachofanyiwa. Ikifika zamu ya JK naye afanywe vivyo hivyo. Period.

Dada/Kaka Ukifata badiko langu sijasema Lowassa ni msafi, lakini ufisadi wa Lowassa unamuhusu JK, na matunda ya huo ufisadi JK kayaona na kuyatumia, Swali liko palepale kwa nini Lowassa anatolewa sadaka
 
Lowassa hawezi kuwa Raisi hata siku moj,jina lake limeshachafuka mno,Ninachomuomba ni kwamba asikubali kuchafuka mwenyewe kwa sababu alikuwa anachora michoro ya kuiba fedha EPA na DOWANS,RICHMOND ili kumsaidia rafiki yake Jakaya ahakikishe akinq'oka anaq'oka na Jakaya ili kuhakikisha nchi inakuwa salama badala ya kuendesha mambo chini chini wakimkabidhi barua aitishe press conference kuomba wenyekiti wa CCM ajiuzulu
 
kuna jambo moja muhimu la kuelewa hapa .mtu anaweza kuwa maarufu kwa mambo mazuri au mabaya!! na haiwezekani yote yakajitokeza kwa pamoja. hapa hoja ni kupata kiongozi mwenye maadili atakayejali maslahi ya watanzania si ya cdm,cuf,nccr,ccm nk nchi kwanza! kuna umuhimu wa kuwafahamu mapema hao wanaoonyesha nia ya kuwania hiyo nafasi ya juu nchini.tuchambue sifa na maadili yao na pia utayari wao wa kuwatumikia watanzania na kuwaneemesha.suala la tuhuma ni dosari kubwa kwa mtu anayewania uongozi wa juu wa nchi.watanzania wenye uwezo na wasio na dosari wapo na hakuna sababu ya kuendelea kuwajadili kina edward. kuna fursa nyingi ikiwemo kuwa mfanyibiashara mkubwa kwa vile huko ndiko ameelemea toka ujana wake.
 
nikisema JK anamwandaa Hussein Mwinyi sidhani kama ntakuwa nakosea
 
we sadak unazijua kwanza??au mbabeli
kuna sadaka za

1)UJENZI
2)HIARI
3)EMERGENCY
4)ZAKA

LOWASA ANATUMIKIA YA NGAPI
 
Rostam Aziz, Andrew Chenge na Edward Lowasa mapacha watatu kwa kifupi RACHEL msikilizeni kijana wenu wa UVCCM sisi huku CHADEMA tulishasema toka pale Mwembe Yanga, Temeke jijini Dar-es-Salaam:
 
Last edited by a moderator:
Mafisadi 17 wameshatajwa na Dr. Wilbroad Slaa. Kwa nini wasitimuliwe wote 17 ndani ya CCM na ndani ya serikali kwa ujumla na mali zao zitaifishwe?
 
Mafisadi 17 wameshatajwa na Dr. Wilbroad Slaa. Kwa nini wasitimuliwe wote 17 ndani ya CCM na ndani ya serikali kwa ujumla na mali zao zitaifishwe?

uamuzi mwingine serikali waombe wanamaombi wawaombeee ukitaifisha mali za lowasa umetaifisha mitaa ya UPANGA yote sasa uoni unarudi kwenye ubinfsishaji..ni kweli lazima maamuzi magumu yajirudie
 
Ameondolewa kwenye chama si kwasababu ya ufisadi epa, richmond et...hiyo adhabu yake ilikuwa kujiuzulu na wanachama tungemwacha apumzike kama tulivymfanya malecela..ok

Anaondolewa kwasababu amewapa chadema (in particular Mbowe) milion 200...ili kuchafua chama chet kwa ajili ya umaarufu binafsi

Chadema kama mnataka mchukueni ...naona Mbowe na Slaa wameshaanza mikakati ya kumtetea ok.
 
JK na Lowasa hawakukutana barabarani..ila tatizo la Lowassa ni kula tunda la mti wa katikati ndiyo maana wanamtosa!
 
afadhali aachiliwe Baraba kuliko Lowassa
 
 
Huo kweli ulikuwa mtazamo wako ambao hauna tofauti na wacheza kamari wa sport pesa! Kumbe kweli nimeamini ndoto za mchana zina bundi nyuma yake!
 
Clinton hakusoma Havard, wacha kulisha watu matango pori hapa!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…