Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2015

lowasa ni mzuri tu kwa kumlinganisha na chekibobu lakini hafai kuwa kiongozi wa serikali bado, ni mwizi bwana unataka nini ili uamini?

Mkuu povu lote hilo la nini? Nakushauri usubiri Oktoba upige kura against him. Au ndio tuseme hii post yako ni kura yako? Haisaidii sana.
 
EDWARD LOWASA ni kiongozi mtendaji si mchekeshaji.
Na nchi ya Tanzania ilipo imahitaji kiongozi kama yeye.
Wapinzani wake juu ya sakata la RICHMOND hawajui uhalisia wa jambo .
Mpeni Lowasa Urais Tanzania 2015 asafishe mazingira ya utendaji katika ofisi za serikali hapa nchini.!
Ikishindikana Lowasa CCM jipangeni kuwa Wapinzani kwa mvurugano utakaotokea ndani ya chama kuanzia July hadi Septemba, 2015!!
 
ImageUploadedByJamiiForums1425789904.745218.jpg

Lowasa ajadiliwe in all dimensions..
 
Ya Mwalimu Nyerere, Lowassa na hali ilivyo CCM

Julius Kambarage Nyerere ni jina zito na lenye maana kubwa nchini. Uzito wake unatoka na kujitoa kwake dhidi harakati zake ambapo aliamua kuiacha kazi yake ya ualimu iliyokuwa ikimpatia mshahara na kuamua kujitosa kwenye siasa na kuanza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika na hatimaye kufanikiwa kuupata rasmi Disemba 9, 1961.

Mara baada ya kufanikiwa kuupata uhuru wa Tanganyika alifanya harakati za kuiunganisha Tanganyika na Zanzibar na hivyo kuzaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Aprili 26, 1964.

Mwalimu Nyerere hakuishia hapo bali aliendelea kuijenga Tanzania katika mikondo ya haki, usawa, amani, umoja na mshikamano. Mwalimu alikuwa na maadui wake wakuu watano ambao ni ujinga, maradhi, umaskini, udini na ukabila ambapo alipigana nao vikali. Hali hii ilimjengea heshima.

Heshima ya Mwalimu ilizidi kupaa zaidi pale alipoamua kuzisaidia nchi nyinginezo za kiafrika kupata uhuru ambapo alitumia akili, hali na mali katika kuzisaidia na hatimaye alifanikiwa katika dhamira yake hiyo ambayo ilimfanya aijengee heshima kubwa jina la Tanzania.

Kutokana na mambo makubwa ambayo aliyafanyia Taifa hili alipewa heshima kubwa ya kuwa Baba wa Taifa letu na kila ambacho alichokuwa akikisema ama akilitenda lilikuwa likionekana la maana hata kama lilikuwa lina mtelezo na chembechembe za kiupuuzi hazikuweza kuonekana. Hakuna mtu yeyote aliyekuwa juu ya Mwalimu hata baada ya kung'atuka madarakani, marais wote waliofuatia wote walikuwa watiifu na hawakohoi dhidi ya Mwalimu.

Licha ya uzito na umaana wa Mwalimu Nyerere aliokuwa nao lakini kuna baadhi alikuwa akiyafanya yalikuwa na maswali tele lakini alikosekana wa kuuliza wala kuhoji maana halisia ya hali hizo. Isipokuwa ni kwa sababu ni Mwalimu aliyaamua hakukuwa na ubishi.

Mathalani mara baada ya kuzaliwa kwa Tanzania, Mwalimu aligombana na swahiba wake karibu sana Ndugu Oscar Kambona hadi kuamua kuikimbia nchi katika mazingira yasiyo eleweka na mpaka leo amekosekana jasiri ama mtu mwenye kuelezea hali ile kwa uwazi kabisa.

Mnamo mwaka 1968, Mwalimu Nyerere aliingia sintofahamu ya migogoro na--viongozi wazito wa TANU wa kipindi hicho ambao ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa TANU na wa pekee, Oscar Kambona ; aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza wa UWT, Bibi Titi Mohammed; Katibu Mwenezi wa TANU,--na Mbunge wa Geita Mashariki, Fortunatus L.Masha; Katibu Mkuu wa TANU Youth League "TYL" na Mbunge wa Rungwe , Elli Anangisye walifukuzwa ndani ya chama na Mwalimu Nyerere katika hali ya sintofahamu nay a uwazi zaidi ambayo iliishia kupewa mwavuli wa--utovu wa nidhamu .

Kama hiyo haitoshi, mwaka 1984 aliyekuwa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Makamu Mwenyekiti--wa CCM (kipindi hicho), Alhaji Abood Jumbe alivyolazimishwa na Mwalimu Nyerere kujiuzulu nyadhifa zake zote alizokuwa nazo pasipo kujua mazingira wala sababu za kufukuzwa kwake na hakuna aliyehoji uamuzi huu wa Mwalimu Nyerere.

Hapa sipo kwa ajili ya kumsimanga mtu bali ni kuweka kumbukumbu sawa juu ya historia ya matukio yalivyokuwa. Mnamo mwaka 1995, Mwalimu Nyerere alitumia mabavu ya hali ya juu yaliyotokana na uzito na heshima ya nafasi yake--kuwaengua John Samwel Malecela na Edward Ngoyai Lowassa katika kuwania nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi.

Kwa upande wa John Samwel Malecela alienguliwa kutokana na tuhuma za kushindwa kuwadhibiti wabunge wa CCM almaarufu G55 waliokuwa wanadai Serikali ya Tanganyika ndani ya Bunge mwaka 1993 na hivyo kushindwa kutetea sera mama ya CCM kuhusu Muungano wa Serikali mbili ambayo Mwalimu ndio alikuwa akisimamia hoja hiyo. Tuhuma hizi za Malecela zimeainishwa vizuri katika kitabu cha Mwalimu kinachoitwa " Uongozi wetu na hatma ya Tanzania".

Naye Lowassa alienguliwa kwa tuhuma za kuwa na ukwasi mkubwa wa pesa na hivyo kujenga taswira ya ufisadi ambapo Mwalimu Nyerere alisema ingekipa wakati mgumu CCM kumnadi mgombea wake kwa wapiga kura.

-Mwalimu Nyerere alizalisha hoja dhidi ya Malecela na Lowassa na kutumia hoja mficho mbili. Mosi, Mwalimu alitambua nguvu kubwa ya kisiasa waliyokuwa nayo Malecela na Lowassa ambao walikuwa ni miongoni mwa wagombea 17 na hivyo kuweza kuhatarisha malengo ya Mwalimu dhidi ya aliokuwa akimtaka. Pili; Mwalimu aliyafanya haya mapema ili kutokurudia makosa ya mwaka 1985 ya kushindwa kumpitisha Dk. Salim Ahmed Salim kuwa Rais ambaye alikuwa ni chaguo la kwanza la Mwalimu Nyerere.

Kwa wale ambao watakuwa na kumbukumbu sawa Mwalimu Nyerere alifanya kosa kubwa la kuchezea shilingi baharini kwani alikuwa akimuhitaji Dk. Salim Ahmed Salim awe Rais lakini akamtegeshea Mzee Ali Hassan Mwinyi kumuomba kugombea urais Mzee Mwinyi akitarajia Mwinyi angekataa na hivyo kumchukua pendekezo la pili ambalo ni Dk. Salim kiulaini lakini alikuja kupigwa na butwaa pale ambapo jaribio (Mzee Mwinyi)--lilipofanya kweli ya kukubali kugombea urais na hivyo mchezo wake dhidi ya Dk. Salim uligonga mwamba.

Chanzo cha tuhuma za ukwasi ama kujilimbikizia mali kwa Lowassa ulianikwa kwenye ripoti ya siri ambapo pamoja na mali nyinginezo Lowassa alikuwa akimiliki nyumba ya kisasa huko Masaki.

Kwa Mwalimu hii ilikuwa ni kishikilio chake pasipo kujua historia ya utajiri wa ukoo anaotoka Lowassa wala kujua historia ya ujenzi wa nyumba hiyo licha ya Lowassa kujieleza vizuri kwenye kikao na mbele ya wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa--kwa undani hatua kwa hatua juu ya nyumba hiyo alivyoijenga na kuanika (kwa mchanganuo) hatua kwa hatua ya alivyoupata utajiri wake.

Maelezo ya Lowassa yaligonga mwamba mbele ya Mwalimu ambaye alikuwa na mgombea wake na hakutaka mtu kama Lowassa au Malecela ama Jakaya Kikwete awe Rais wa awamu ya tatu kumrithi Mzee Mwinyi. Na ikumbukwe kuwa kipindi hicho ilikuwa ni ngumu sana kwa mtu yeyote kushinda nafasi ya urais bila ya Mwalimu Nyerere kukuunga mkono kutokana na uzito wake kwa Taifa hili.

Watu ambao ni wabaya wa kisiasa wa Lowassa wanaitumia sana hii hoja ya mwalimu kumkata Lowassa kama fimbo ya kumchapia Lowassa ambaye ameonekana ni tishio na kipenzi cha Watanzania katika nafasi ya mrithi wa Rais Kikwete 2015.

Lakini watu hao hao wanashindwa kutambua ukweli na kuweka kumbukumbu sawa ya ukweli kwamba ni miaka miwili tu ya mara baada ya kuchaguliwa kwa Rais Mkapa mwaka 1997 alimteua Lowassa kuwa Waziri katika serikali yake wakati huo huo Mwalimu akiwa bado yupo hai. Kama Lowassa angekuwa na uchafu wa utajiri wenye mashaka, Mwalimu asingekubali kuruhusu hali ile ya Lowassa kuteuliwa kuwa Rais kwani alikuwa bado ana sauti na nguvu kubwa ya kimaamuzi dhidi ya Rais Mkapa.

Kiukweli mpaka sasa ni ngumu kabisa iwe ni mtu ambaye hajasoma au hata iwe ni kwa Profesa wa chuo kikuu-kukubali moja kwa moja kwamba utajiri wa Lowassa ilikuwa ndiyo sababu ya msingi kabisa ya kuondolewa ama kuenguliwa na Mwalimu Nyerere katika kinyang'anyiro cha urais 1995.

Mbaya zaidi wanaoishupalia hoja ya Nyerere kumkataa Lowassa wengi wao katika uchache uliopo ni viongozi wa CCM na ni viongozi wa kiserikali kwa madai ya kuwa wanamuenzi Mwalimu Nyerere kupitia misingi yake aliyoijenga. Jamani, hii ni sawa kweli?

Mwalimu Nyerere aliamini katika uwepo wa usawa katika jamii na ndio maana akalianzisha Azimio la Arusha la mwaka 1967 lililokuwa na lengo la kuondoa unyonyaji, matabaka na kuleta usawa ndani ya jamii. Lakini viongozi hawa hawa ambao leo hii wanajinasibu kumuenzi Mwalimu ndio waliolivunja Azimio hilo huko Zanzibar mnamo mwaka 1992 na kuanzisha Azimio la Zanzibar ambapo leo hii limezaa na kuongeza kiwango cha hali ya juu cha utabaka kati ya maskini na tajiri; kimeongeza hali ya utabaka unaolihatarisha Taifa letu kati ya walio nacho na wasio nacho.

Watu hawa, utasema kweli ya Mungu, wanamuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo? Iweje suala la kumuenzi Mwalimu Nyerere liwe ni kupitia kumkata na kumchafua Lowassa na si kusimamia suala la kuondoa matabaka sugu yanayoligawa Taifa letu?

Mwalimu Nyerere alipambana vikali dhidi ya maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini. Lakini leo hii kiwango cha ongezeko la ujinga (kutokana na uduni wa elimu yetu) na kiwango cha umaskini wa kipato kwa Watanzania ni cha hali ya juu kupita wakati wowote ule.

Huku jamani ndio kumuenzi Mwalimu na kuisimamia misingi yake? Iweje msingi wa kumkataa Lowassa ndio usimamiwe zaidi kuliko msingi wa kuondoa tatizo la ujinga, maradhi na umaskini?

Hiyo ni mifano michache tu ambayo inatupa kila sababu ya kuhoji dhamira zao kwani hauwezi kuusimamia kigezo cha Lowassa pekee na huku ukiikiuka misingi mikuu aliyoijenga Mwalimu Nyerere. Halikadhalika hauwezi kabisa kabisa kutenganisha taswira ya kile kinachodaiwa ufisadi wa Lowassa na taswira ya CCM. Hii nina maana ya kuwa hauwezi kumkosoa ama kumzomea Lowassa katika eneo la uadilifu bila ya kuikosoa ama kuizomea CCM. Hii ni sawasawa na kunyooshea kidole kimoja mwenzako huko vidole vinne vilivyosalia vikikuhukumu.

Ndani ya CCM na serikali zake tumesikia kila aina ya uchafu, tumesikia kila aina ya ufisadi ukitajwa tajwa na watu. Hii ina maana ya kuwa kigezo cha uadilifu cha kutokuwa fisadi si kigezo wala sifa ya uadilifu kwa mgombea wa CCM kwani kuishupalia hoja hii mbele ya umma ni sawa ni kushupalia CCM isimamishe mgombea yeyote Yule katika uchaguzi wowote ule.

Kinachowatofautisha viongozi wa CCM na serikali ni tofauti ya kiwango na dau wanalolipiga kulingana na nafasi mtu aliyonayo. Kitendo cha kumshupalia Lowassa dhidi ya hoja ya ufisadi kitazua maswali na tafakuri ya siasa maji taka kwa Wananchi na watakachoangalia wao ni historia ya uchapa kazi wake na ndio haswaa kitakacho mbeba Lowassa kuliko wagombea wengineo ndani ya CCM.

Huu ni ushauri wa bure kwa CCM, kuachana na hoja ya kutumia kete ya kinachosemwa ufisadi dhidi ya Lowassa kwani kinaweza kuiporomosha CCM dhidi ya wananchi ambao ni waelewa na wanaijua vyema siasa ilivyo.

Naomba kutoa hoja.
 
[video=youtube_share;-lZTdDotxXY]http://youtu.be/-lZTdDotxXY?t=8m14s[/video]

[video=youtube_share;hQe6kqOw3Ko]http://youtu.be/hQe6kqOw3Ko[/video]
 
CCM yetu safi kamwe haiwezi kumpitisha au kumteua FISADI MKONGWE kupeperusha bendera ya CCM kuongoza nchi. Lowassa ni mwizi kwanini mwizi apewe nchi akiiiuza je, acheni ujinga na mnaomuona Lowassa ndio rais mtakuja kufa kwa presha jina la mgombea litakapotolewa.
 
Habari za asubuh wapambanaji wa mzee Lowassa...ni mara chache na nimara ya kwanza kwa dunia yenye utandawaz,technologia za kimataifa,nchi yenye watu wasomi kwa kiwango cha juu kabisa watu mamia,maelfu elfu kwa makundi mbali mbali..watu wenye vyeo mbali mbali,umri tofauti tofauti kutoka kila pembe ya nchi yetu kwa umoja wao kwa utashi wao kuandamana kifikra,kimaneno na kimatendo kuonyesha nia ya dhati wazi wazi kwa KIPENZI wao wanao mtaka ht kama uchaguz bado kabisa.ni waz watanzania tuna imani kubwa na mzee Lowassa na kwa hili Mungu anadhihirika waz kwani sauti ya wanadam weengi ni sauti ya Mwenyezi Mungu.asubuh njema watanzania.kura yangu moja,tanzania yangu ni moja nampenda Edward Ngoyai Lowassa awe rais wetu 2015-2025.
 
Lowassa ndie mwana ccm pekee anayeweza kuifanya nchi yetu ikastawi angalau kama Kenya, au Uganda au hata Rwanda !
... maana sasa tumekuwa afadhali ya msumbiji
 
Tatızo la viongozi wetu sio tu ufisadi balı naksi ya uweledi,ujasiri na maamzi sahihi.Hata kama kıongozi akawa fısadi lakn agressive mm sıoni shda kuliko na mwadilifu lakn lineant na asiye jasıri.

Siamini kama Rais anaweza kupatikana mzuri anayetumia gharama kubwa kuupata,Najifunza kwa Obama
 
Back
Top Bottom