Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2015

Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2015

Pamoja na Uchama na nini ila huyu mama kashindwa kuongoza Bunge coz kuna Hoja pia ilitoka kwa Zambi ikaungwa mkono na Jenista Muhagama afu hoja hiyo hiyo ikarekebishwa kidogo na Mnyika ikilenga kubalance upande wa Serikali pamoja na Wabunge ambao ndo wanatunga Sheria huku ikilinda Maslahi ya Umma ikapata Sapoti ya Simbachawene ambae pia ni mwenyekiti wa bunge ila shida inakuja huyu Mama alivyoendesha mjadala hadi kufikia muafaka yaani ni kama Sheria anatunga ye mwenyewe nakuipitisha coz hata angekuwa Bias ingekuwa afadhali sasa kazi ya Bunge nini?
 
kauli ya kinafiki na kupandikiza hiyo balile unajulikana wewe kwa unafiki wako endelea kuwa tetea mabosi zako ila iko siku damu ta WAtz itakuangukia.
 
Kwa sasa mama hana comfu. vijana wame mchanganya hasa baada ya siku ya alhamis iliyopita kwenye maswali ya papo kwa papo kwa pinda. Mimi nadhan aseme tu, yamenishinda.
 
Alianza na jazba toka day 1 akijua atawanyamazisha wabunge machachari, lakini bahati mbaya amegundua kuwa haiwezekani, anachofanya sasa ni kuzuia au kulimit miongozo ya spika, na kumsaidia waziwazi waziri mkuu kwa kuyakataa baadhi ya maswali asiulizwe.
PM naye angekuwa makini angemzuwia Spika asiwakataze wabunge kumuuliza maswali...lakini hata PM ni walewale!
 
Hivi tunakaa kujadili ukali au Upole wa Spika hapa?Itatusaidia nini?Spika ni cheo na si mtu na kipo kwa mujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,kama anatekeleza majukumu yake kinyume na taratibu zilizopo basi tutumie taratibu hizo kumwajibisha.

Tuache JAMII FORUM iwe Furum ya kujadili mambo ya maana kwa mustakabali wa Taifa letu na si MAJUNGU na kuzungumzia Maisha ya watu binafsi!
 
Edward Ngoyai ndie anaeijua CCM ndani nje, ndio anajua falsafa ya CCM (Uliza ni ipi), Ndio safi kuliko viongozi wote wa CCM kwa kigezo cha itikadi halisi ya CCM. Atagombea tu. Ila sijui kama atashinda.
 
Wapendwa.

Ni mara yangu ya kwanza kuchangia kwenye wavuti hii. Suala la lowasa kufaa au kutofaa kusema ukweli kunategemea utashi wa mtu. Kwa upande wangu unawaza ni kiongozi siyo mtawala " a leader is the one who shows the way and to be a leader is to be accepted" ni ukweli usiopingika kwamba c.c.m bila lowasa inapwaya. Ni lowasa pekee anaethubutu kufanya maamuzi hata yasiyowezekana katika hali ya kawaida ( kama 1. Kukandamiza mawingu tupate mvua 2. Kupita upande wa pili wa barabara ili kupunguza msongamano dar. Mimi naamini angekuwa bado waziri mkuu fly overs zingekuwa zimeshajengwa).


Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Mambo yote ambayo c.c.m inajitangaza kama mafanikio yako yote ni msukumo wa lowasa. Baada ya yeye kuondoka uwaziri mkuu hatuoni chochote tangible kama taifa.


1. Ni lowasa aliyesimamia kwa nguvu zote mradi wa maji kutoka ziwa victoria mpaka shinyanga na kahama;


2. Ni lowasa aliyesimamia kwa ujasiri ujenzi wa chuo kikuu dodoma ndani ya muda mfupi wanafunzi wakaanza masomo.


3. Ni lowasa pamoja na udhaifu wake aliyesimamia uanzishwaji wa shule za sekondari za kata.


He is a man of actions not word, na hicho ndicho kinamponza. Hakuna c.c.m bila lowasa kama huamini subiri kama c.c.m itaweza kumfukuza. Thubutu!



Pamoja na udhaifu wangu nawasilisha.
 
Naunga mkono hoja asilimia 100% kwa mia,mimi nakubalina na mawazo wanayotoa wengine kwamba wana haki ya kufikiria tofauti lakini umesema ukweli,Sisiemu imeapwaya sana toka kuondoka kwa huyu jamaa!Heshima ya chama imeporomoka sana miongoni mwa wanachi wengi,hao waliomundia tume ili wamalize wamesababisha wanachi wakichukie chama ndio maana kimepoteza Majimbo mengi tena kwenye miji mikubwa Tanzania.

Bado nina imani kwamba mzee wetu EL akipewa nafasi atauthibitishia umma wa Tanzania kwamba yeye ni nani.Ahsante mkuu kwa kuwakumbusha wanajamii wenzangu jinsi alivyosukuma kukamilika kwa mabo muhimu katika Taifa letu.Hata JK mwenyewe mara kadhaa amemlilia sana EL,anafahamu kwamba wangekuwa pamoja hadi sasa,mambo yangekuwa tofauti na ilivyo sasa.

Narudia tena,kama mwandamu hawezi kukosa mapungufu,but mema nayoweza kufanya na aliyofanya vizuri tuyaseme jamani.

Bado sijajibiwa swali langu?

Mitambo ya Dowans/Richmond haijawashwa?sio huu umeme tunaotumia sasa ?

Kama Sisiemu watamfukuza EL,basi tujue kwamba watakuwa wamejimaliza wenyewe.

Shime wana Sisiem,msidanganyike na wanaompuuza EL,Wanajua wazi huyu ndie mgombea mwenye nguvu anayeweza kuleta upinzani mkali kwenye Uchaguzi,kuweni macho sana!
 
one mistake ahundred goals! Lowassa enough is enough, go! Nikwel Lowassa ni mchapa kazi ila ni fisadi wa kupindukia sikubali tumkabidhi nchi, hata mwl. Nyerere mwaka 79 alituambia 'Ni heri mfanyakazi mzembe kuliko Manager mlevi'
 
Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake kwa mujibu wa mawzo yake kwakuwa ana utashi wake binafsi so naomba nitoa mtizamo wangu na sitatoa maoni ili kumfurahisha mtu humu ndani ya Forum ni maoni yangu na nina haki ya kuwa tofauti au sawa kimawazo na mtu yoyote.EL anaifaa Tanzania kwa sababu zifuatazo:-

Ni Kiongozi huyu shupavu,jasiri na mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama na serikali kwa upande wa serikali hili linadhihirika aliposhika nyazfa mbali mbali kama:-

a.Kusimamia Sekta ya Elimu ambayo ndiyo Uti wa mgongo wa maendeleo ya Taifa lolote hapa Duniani.Alisimamia kwa ukakamavu kutekeleza mpango wa kupanua Elimu ya Sekondari na alihimiza kwa nguvu zake zote ujenzi wa Shule za Kata Nchi nzima ili kuwapa Fursa Mamilioni ya Watanzania wenzetu waishio Vijijini kupata Fursa ya Elimu.

Zoezi hili lilihitaji uwekezaji mkubwa sana na Tukumbuke kwamba Taifa letu ni Maskini sana,changamoto zilizo ikabili Sekta ya Elimu kama Ukosefu wa vifaa vya maabara,Nyumba za Walimu,Madarasa ya Kutosha na upungufu wa Vitabu si kosa la mtu Fulani bali umaskini wa Taifa letu ndio maana WB na IMF hutoa misaada kwa nchi maskini kusaidia maendeleo ya Elimu kwakuwa ni Sekta inayohitaji uwekezaji mkubwa kifedha na Rasilimali zingine.

EL ni mtu anayeamini katika Elimu ndi maana motto wake ni tofauti kidogo na Motto wa Chama chake na anasema ’’ ELIMU KABLA,KILIMO KWANZA’’ Ni kweli kabisa kwamba hakuna linaloweza kufanikiwa bila Elimu,Unaweza kuwaambia watu wasio na Elimu ya kutosha Walime Kilimo cha Kisasa?Me I agree kwamba Elimu KABLA na Kilimo Kwanza.

Mataifa Makubwa yaliondelea leo Duniani yalifanya uwekezaji Mkubwa kwanza katika Elimu,hasa Elimu ya Msingi(Kwa mfano China,Brazil na USA) na Baadaye kufanya Mapinduzi Makubwa ya Kilimo,baadaye Viwanda Vidogo na baadaye Viwanda vikubwa ambavyo vilichochea kukua kwa kasi kwa Sekta za Huduma na kupelekea mfumuko wa nafasi kibao za ajira kwa Vijana!!!

b.Kuwafukuza bila woga hadi kuwasindikiza Airport wawekezaji wababaishaji wa Kampuni ya City Water hadi kuwapandisha ndege uwanja wa
Taifa:

Akiwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo ,EL alitekeleza wajibu wake kwa umahili mkubwa na bila uwoga na moja ya mambo ambayo yatakumbukwa ni kufukuzwa kwa wawekezaji wababaishaji wa Kampuni ya Kitapeli ya City Water ambao walishindwa kutekeleza wajibu wao,aliwatimua na kuwasindikiza hadi Airport!EL ni Kiongozi Shupavu sana na asiyeogopa mtu!

c.Kiongozi Mwajibikaji na asiyeogopa kufanya maamuzi magumu hata kama yatamuuza

Kujiuzulu kwake kutoka katika Wadhfa wake wa Uwaziri Mkuu kufuatia Kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond inachukuliwa na wengi kama kuhusika kwake katika Saga hilo.Napenda kuwakumbusha Watanzania wenzangu kwamba Waziri Mkuu ndiye mtendaii Mkuu wa Shughuli za Serikali na mtekelezaji wa Maagizo ya Baraza la Mawaziri ambacho kimsingi ndicho chombo kikubwa cha Utendaji wa serikali (Govt. Machine) na hivyo kama kuna Kosa linafanyika basi Linatosha kuiangusha Serikali nzima so katika SAGA ile ilibidi Serikali Nzima akiwa ni Pamoja na Rais wajiuzuru lakini EL akubali mwenyewe kwa ajili ya kulinda heshima ya Chama chake na Serikali, huu ni mfano mzuri wa kuigwa kwa Waafrika wote.

Siku zote tatizo letu waafrika ni kukosa kuwajibika pale inapobainika uzembe umefanyika,ukweli umebaki kuwa wazi mpake leo hii NCHI IPO GIZANI migao ya Umeme inaendele kama kawaida na dada wa Richmond ambaye ni Dowans Mitambo yake inawashwa na tumerudi pale pale!! Mimi nasema kwa kosa la Richmond,Serikali nzima ilikuwa imeanguka.

d.Mfuatiliaji na asiyechoka kufuatilia kero za na hakai ofisini kungoja taarifa
Wakati wa janga la Njaa lilisababishwa na ukame kwa msimu wa mwaka 2007/08 ni huyu EL alikuwa akishirikiana na Wakuu wa Wilaya zote zenye njaa na wakati mwingine alishiriki yeye mwenyewe kupita nyumba kwa nyumba kusimamia zoezi la ugawaji wa chakula kwenye Familia zenye njaa ili kuhakikisha kwamba azma ya serikali ya kwamba hakuna mwananchi atakayekufa kwa njaa inatimizwa ni huyu huyu EL.


Mtu hawezi kukosa mapungufu hata siku moja,nakubali ana mapungufu yake lakini EL ni embe dodo lililoiva tayari kuvunwa na Watanzania Mwaka ukifika 2015.


Nawaleteeni EL

Nakupongeza sana kwa kuwa na ujasiri wa kutoa ukweli uliopo. Serikali ndiyo ilikosea kwenye sakata lile na laiti Mh. Lowasa angekuwa hana mapenzi na chama na serikali yake mpaka sasa hivi angekuwa ameshatoa siri nzito iliyojiri ambayo ndiyo ilipelekea yeye kuhukumiwa. Mantiki hii ni sawa na ile ya kubeba dhambi kwa ajili ya wengine!!

Mpaka sasa hivi si chama cha siasa au maadui wa Lowasa wanaoweza kusimama na kueleza ufisadi wa Lowasa, kinachoendelea sasa ni majungu na roho mbaya pamoja na tabia ya watanzania kufuata mkumbo bila kufanya utafiti wa kutosha, ndiyo maana ni rahisi sana kumwitia mwizi mtu yeyote na wananchi wakatoka bila kuuliza kaiba nini bali wao watatoka na kumchoma moto.

Kama Lowasa angekuwa na hatia mpaka sasa hivi angeshafikishwa mahakamani kujibu tuhuma. Vyombo vya usalama vimeshakiri wazi kuwa hakuna tuhuma zinazomkabili ndiyo maana hawawezi kumfikisha mahakamani.

Kama Lowasa angekuwa ni mbaya kiasi hicho wakati wa mkutano wa rais na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam asingemtetea kiasi kile kuwa hakuwa na kosa

kama Lowasa angekuwa na hatia rais wakati wa kampeni asingemnyanua mkono na kuutangazia umma kuwa Lowasa ni mtu safi, ndiyo maana nilishangaa sana rais kugekuka na kuanza kutoa hoja za kujivua gamba, watajivuaje gamba wakati alishawanyanyua mikono kwenye kampeni kuwa ni watu safi akiwemo Lowasa?

Kama Lowasa ni mbaya mbona alipewa kura na watu wake kiasi kile?

Kama Lowasa ni mbaya mbona amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa moja ya kamati nyeti za mambo ya usalama?

Lowasa angekuwa dini nyingine asingeandamwa hivi. Hii ni hofu ya urais.

Polleni sana wana JF mnao mchukia MH. Lowasa bila kufanya utafiti ila nawahakikishia kwenye hili Mungu ataonekana.
 
Kama nilivyowahi kusema Lowassa akisimama kwa nafasi ya urais nitampa kura yangu. Haijalishi yupo CCM au kwenye Chama kingine.
Kinachofanywa na CCM kwa sasa ni kujaribu kumchafua Lowassa ili hata akiamua kwenda Chama kingine aonekane hafai na hili Lowassa anafahamu fika na ndiyo maana ametulia kimya.
Nampenda sana Lowassa sio kwa sura yake bali ni kwa utendaji wake na uwezo wa kufanya maamuzi magumu ilimradi tua ajue kuwa ni ya haki.
  1. Alifanya maamuzi ya kutoa maji Lake Victoria licha ya kelele za Misri na majirani
  2. Aliusitisha mkataba wa kinyonyaji wa City Water
  3. Alisimamia kikamilifu sera ya shule ya sekondari kwa kila kata. Kwa mara ya kwanza katika nchi yetu ndiyo tumenza kusikia katika awamu yake idadi ya watoto waliofaulu. Zamani hizi tarakimu hazitolewi bali zilikuwa zinatolewa za watoto waliochaguliwa na wengi walikuwa watoto wa walimu na viongozi. Watoto wa wakulima wa kawaida ni wachache sana na shule zilikuwa zinaweza kuadhibiwa kwa watoto kutochaguliwa kwa muda mrefu hata miaka saba. Kwa sasa nafasi za shule ni nyingi wakati mwingine kuliko watoto waliofaulu katika baadhi ya kata. Falsafa hii ndiyo imeanza kuonyesha matunda ya haki kwa Wabunge wengi wa Upinzani kupita kwani wapiga kura wengi ni vijana wa shule ya sekondari na wale waliomaliza. Ninaamini kuwa std seven leaver siyo sawa kabisa na form four failure. Form four failure lazima kuna kitu amekipata shuleni hata kama ni civics lakini basic right zake anafahamu. Sera hii ya kuelimisha jamii ni nzuri sana na ndiyo itakayopelekea kumaliza enzi ya CCM katika nchi hii. Ni kwa mantiki hii nasema Lowassa anatufaa sana kama kiongozi wa nchi hii.
  4. Baada ya sera ya shule za kata kufanikiwa alikuja na sera ya Zahanati kila kata. Kabla hajatekeleza sera hii, akajiuzulu na ndiyo mwisho wa utekelezaji wa sera hii. Aliyekuja sijui hata kaja na sera gani ameisimamia je! Kwa ujumla sijaona kitu cha muhimu serikali imefanyia kazi na impact yake kuonekana baada ya Lowassa kuondoka.
  5. Ndiye aliyekuja na kutaka kutatua kero ya jam barabarani, alianza na mistari mitatu na akashughulikia upanuzi wa Ali Hassan Mwinyi Road mpaka Mwenge, Alishughulikia uboreshaji wa barabara ya Shikilanga na uboreshaji wa feeder roads nyingi za Dar na ambazo baada ya yeye kutoka kuna mengine yamesimamia hapo hapo mpaka vifusi vimejisambaza zenyewe.
  6. Alisimamia kwa ufanisi ugawaji wa chakula kwa waliokuwa wanahitaji bila kuuziwa na viongozi wadhalimu na wengi wa waliokiuka walichukuliwa hatua na wengine walifukuzwa kazi kushtakiwa na hata kufungwa.
  7. Ni kiongozi ambaye akitembelea sehemu anaangalia report za awali za sehemu hiyo na kama akifahamu kuwa ripoti inayosomwa ni ile ya wakati uliopita alidiriki kumwambia hiyo ripoti ninayo ni ya mwaka juzi nataka ripoti ya sasa. Hivyo viongozi walifanya kazi kwa kuwa wanajua kuwa akiwatembelea hataki kupambwa kwa hotuba ndefu zisizo na utekelezaji.
  8. Ni Kiongozi ambaye ameanzisha uchunguzi wa majengo mengi Dar hasa Kariakoo ambayo yako chini ya kiwango na majengo mengi pamoja na kuwa wengi wa wanasiasa ndiyo wamiliki walitakiwa kuyarekebisha. Alipojiuzulu ripoti mpaka leo ipo kwenye kabati wanasubiri maafa waunde tume nyingine.
  9. Ni Kiongozi ambaye anapenda kufanya safari za ndani za kukagua maendeleo badala ya kwenda nje ya nchi mara kwa mara. Hili lilimjenga sana na REDET walipotoa tathmini kuwa EL ni maarufu ndani ya nchi kuliko JK na Regina maarufu kuliko Salma, hapa ndipo upepo ukabadilika na hakukaa tena muda baada ya hiyo ripoti (Kumbuka Ouko na Moi).
  10. Aliweza kusimamia haki Bungeni na ni yeye aliyemwambia Sitta hakuna haja ya kujenga ofisi ya Spika Urambo kwani hana hakika kuwa kila wakati Spika atatoka Urambo au La sivyo kujenga ofisi ya Spika katika jimbo la kila Spika haitawezekana. Lakini baada ya kujiuzulu walibadilisha haraka kanuni za Bunge na ofisi ya Spika ikajengwa Urambo, hata kabla ya nyumba ya Spika kijengwa Dodoma.
  11. Katika jimbo lake amewainua sana akina mama na vijana na pia akavuta maji kutoka jimbo lingine kwa kuchimba kisima kirefu na kuwapelekea wananchi wake.
  12. Ukiwa mchapa kazi katika kundi la wavivu, utaonekana adui na hufai kabisa. Hii inawezekana ndicho kilichompata Lowassa.
  13. Kila binadamu ana madhaifu yake lakini tujue pia kuwa HATUNA MALAIKA WA KUJA KUWA VIONGOZI WETU BALI NI SISI WENYEWE BINADAMU NA KILA MMOJA ANAMAPUNGUFU YAKE LAKINI KATIKA UTENDAJI TUMEZIDIANA.
  14. LOWASSA YOU HAVE MY SUPPORT, GO FOR PRESIDENCY TO TAKE THIS GREAT COUNTRY TO GREAT HEIGHTS.
 
Njia ya lowasa kwenda ikulu nyeupee!!pe!pe!pe! Kama atakuwa tayari kutoa siri zote anazozijua za kuhujumu nchi yetu na watanzania; baada ya hapo aungame!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kwa kuwa sifa ya kiongozi yoyote yule ni ujasiri!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Tunayajua yootee!!!! Hayo, lakini sifa moja kubwa na muhimu kwa kiongozi yeyote ni ujasiri, yeye hana. Kwa maana hiyo tayari hafai!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Nanu kumbe huna habari kuwa, ndugu zake hukoo umasaini wanakufa kwa njaa. Ni vipi awashibishe majirani wakati watoto wake wanakufa na njaa. Au husikilizi redio;;;;; hawana chakula wamasai huko kwao. Uongozi mzuri huanzia nyumbani.
 
Pamoja na wote wanaoendesha siasa za kumpaka matope, bado ni kiongozi pekee mwenye kupenda watu wake. Ni mbunge pekee ktk Jamhuri hii ambaye jimbo lake linaongoza kwa kuwa na mabweni ya watoto wa kike. Anafaa kwa kweli
 
Nafikiri wakati wa kampeni za 2015 bado tusubiri wakati ukifika then ulete hizi hoja. Huu ni wakati wa kufikiri jinsi gani wananchi wa kawaida wataweza kumudu maisha yao na kuiona kesho sio nani anafaa au hafai. Mtu anaweza kufaa sasa lakini miaka miwili ijayo hafai au hafai sasa lakini baadae anafaa. ikifika wakati tutajadili hii hoja ya nani anafaa na tutatoa sifa za kiongozi safi then ww upime mwenyewe kama huyo wako anafikia hivyo vigezo.
 
Watanzania na hasa wabunge wa ccm ni manafiki sana. Lowassa anapigiwa makofi bungeni ili iweje.

Kudadadeki mimi nitasilimu kama Mkristo Lowassa atagombea Urais 2015.
 
Mkuu nakuunga mkono kabisa!
BUT NILIAMBIWA KUWA CCM WANAMWOGOPA SANA LOWASA NIMEAMINI NI KWELI!
 
EL Atikisa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania!

Juzi Ijumaa Mh EL alichangia hoja katika Bunge la Bajeti na Hotuba yake kakatizwa mara kwa mara la Makofi na Shangwe miongoni mwa Wabunge toka ameanza hadi amemaliza,hii ilikuwa udhihirisho wa wazi kwamba wa kiu na kilio cha Mamilion ya Watanzania kwa Utendaji mahili wa Kiongozi huyu shupavu kupitia kwa Wawakilishi wao ambao ni wanachi.Kwa muda wa Majuma kadhaa vyombo vya habari vimekuwa vikipamba Picha zake.


HOJA YAKE
Katika wakati huu mgumu sana unalikabili Taifa letu ni Kweli kwamba tunahitaji watu watakaofanya Maamuzi MAGUMU bila woga kuliokoa Taifa letu katika majanga yanaloikabili bila kuogopa matokeo ya maamuzi yao.Shime Viongozi wetu,Fanyeni Maamuzi MAGUMU ili mliokoe Taifa letu,hatutawalamu kwa matokeo ya maamuzi yetu bali kwa matokeo ya kutokufanya kwenu maamuzi.

Ahsante sana EL kwa Ujasiri ulioonyesha kusema wazi wazi na nina imani kwamba Mamillion ya Watanzania wako nyuma yako! na bado wanakulilia.
 
Back
Top Bottom