Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2015

Kwanini Lowassa anafaa kuwa Rais wa Tanzania 2015

ZIPOMPAPOMPA, kama Lowassa ni rafiki yako wa kweli hebu muulize na aseme ukweli toka moyoni mwake, ni kitu gani kinachomfanya alazimishe kupata madaraka? Tatizo lenu nyie hamumshauri vizuri huyu mzee, munachoangalia ni "mrungura" tu, mukiishavuta basi. Kama unakiri kuwa hata ukimwita mtoto wa darasa la 4 na ukamuuliza Fisadi ni nani atakwambia Edward Lowassa, je, maneno haya huwa munamwambia? Na kwa uelewa huo, je unaona bado ana nafasi ya kuongoza Taifa hili?
 
Waulize walioko Keko kama wote kweli ni wakosaji.

Lowasa alishindwa kujitetea mwenyewe Bungeni miaka iliyopita, leo hii ndo unajitokeza kuuliza ubaya wake!

Mushaurini arudi AICC, kwani mpaka arudi kuwa waziri mkuu?

Pamoja na huo uchapakazi hata huko AICC hafai
 
WATANZANIA WENZANGU HEBU TUACHE USHABIKI HALAFU TURUDI KATIKA UKWELI NA UWAZI,
KAMA NI KUCHAFULIWA NA KUONEWA MHESHIMIWA EDWARD LOWASA AMEONEWA NA KUCHAFULIWA SANA,
LAKINI NAPENDA KUULIZA, JE NI KWELI MZIGO WOTE WA UFISADI NA UBAYA WOTE UNAOTENDEKA TANZANIA LOWASA NDIO TOP OF ALL???
LEO HII KILA UNAPOPITA, HATA UKIMUITA MTOTO WA DARASA LA 4 UKAMUULIZA UNAMJUA FISADI, ATAKUAMBIA LOWASA.

BINAFSI NAKUMBUKA JINSI AMBAVYO ALISIMAMIA KIDETE SUALA LA UANZISHWAJI WA SHULE ZA SEKONDARI KILA KATA, JAPO HAZIKUPATA MAFANIKIO MAKUBWA BUT KWA KIASI KIKUBWA LIMEPUNGUZA WIMBI LA VIBAKA NA MATEJA KWANI VIJANA WETU WANAOMALIZA LA SABA WANAINGIA SEKONDARI KWA WINGI.

VILE VILE NAKUMBUKA KABISA KWAMBA NAMBA MUHIMU ILIYOPIGIA DEBE UANZISHWAJI WA CHUO CHA DODOMA NI HUYU HUYU LOWASA.

JE UNAWEZA UKAMLINGANISHA EDWARD LOWASA NA MIZENGO PINDA? PINDA ALIRUDISHA GARI ALIYONUNULIWA ILI AONEKANE NI KWELI NI MTOTO WA MKULIMA, LAKINI HAPO HAPO TUNAAMBIA ANAENDA JIMBONI NA MSAFARA WA MAGARI 50.

NAKUMBUKA NIDHAMU YA KAZI ENZI ZA LOWASA, JAMAA UKISIKIA ANATEMBELEA WIZARA FULANI, LAZIMA WATU WAWEKE ADABU KWA SABABU WANAJUA HATAKI MCHEZO KATIKA KAZI.

SASA NAULIZA JE NI LOWASA ANASTAHILI KUHUKUMIWA KILA KONA KWAMBA YEYE NI FISADI? KWA NINI VIONGOZI WENGINE KAMA KIKWETE, MKAPA, MSABAHA, KARAMAGI ETC, HAWASHIKIWI BANGO KAMA ANAVYOSHIKIWA LOWASA?

KIPINDI KILE ALISEMA BUNGENI "TATIZO NI UWAZIRI MKUU" JE NA SASA TUSEME "TATIZO NI URAISI" ???

!!!tafakari!!! :A S 114:
Hapo kwenye red napingana na wewe kuwa secondary za kata zimepunguza wezi..coz wale walioenda hizo shule ndo hao 99% wamefel na wapo mtaani..what are they going to do?
 
Huwezi kumfananisha Edward Lowassa MWIZI na Mizengo Pinda MWADILIFU. Ndugu yangu ZIPOMPAPOMPA hebu jitokeze kidogo utujibu maswali yetu ili tukupe undani wa UCHAFU wa LOWASSA. Baada ya kutoka kwa Mch. Joshua wa Nigeria, LOWASSA ameonekana bungeni akisalimiana na kila mtu, nina wasi wasi kwa kasi ile atasalimia mpaka kivuri. Hizi ni dalili za kuchanganyikiwa zaidi maana sasa ameonesha wazi kuwa hawaamini viongozi wa dhehebu lake na akaamua kwenda kuombewa Nigeria. Kila mtu mwenye uelewa anajua sifa kubwa ya Nigeria ktk matumizi ya nguvu za giza. Bila aibu mwanaume huyu alitua huko kwa maombezi.
 
Kama taifa na kama tunadhamira ya kweli ya kupambana na ukali wa maisha basi inabidi kufanya jambo moja tu - tuchane kabisa na hii tabia ya ku-recycle viongozi. Leo wezi, kesho victim, kesho kutwa wapambanaji! Tanzania hakuna watu wengine wa kutuongeza? Personally ningetaka kufunga hii chapter ya 'walewale' .

You are very right!
 
Mbona unatulazimisha kumkubali? kwani wewe ndiye mlileta - Amini watanzania wa sasa ni wajanja, waache wanajua wanachokisema- don't school us plz
 
Mwanae Lowassa amenukuliwa mara kadhaa akidai kuwa wao wameikamata "media house" hapa nchini, lakini mbona wanashindwa kumsafisha Lowassa kama kweli amechafuliwa kwa kuonewa na kwamba yeye ni msafi? Tunachokiona sasa hivi ni kuchafuliwa kwa viongozi wengine kwa gharama za kumsafisha Lowassa. Mpango huo hautafanikiwa kwani ndio munazidi kuwapandisha ktk nafasi ya juu hao munaodhani munawachafua.
Hivi wewe ZIPOMPAPOMPA unaamini kuwa ukimshauri LOWASSA kwenda kufanya mkutano wa hadhara pale Jangwani atakubali kufanya hivyo? Unaweza kubuni nini kitakachotokea? Hebu jaribuni muone.
 
Ndugu zangu,

Tanzania ya leo haistahili mjadala kama huu; tuna watu wengi na tuna fursa ya kuanza ukurasa mpya na kuvaa nguo mpya kwanini tunapenda kurudia nguo kuukuu? We must give a chance to a positve turning point for our country. Let us look forward and talk the future of this nation. Lowassa is a very old story we have to close this chapter and move forward we are not being fair to our beloved Tanzania. Chadema wanaongoza mapambano ya kuikomboa hii nchi kwenye mikono ya watu kama akina lowassa(Mafisadi), kwanini tusiwaunge mkono na tuachane na unafiki wa CCM wa kujivua magamba. Watanzania hautuwezi tukawa ni watu wa kusubiri CCM wajivue magamba enough is enough! Tuna nafasi ya kusonga bila CCM. Lazima ifike mahali CCM waadhibiwe kwa matendo yao. Miaka 50 ya uhuru watu wanalala gizani eti umeme ni wa mgao; we dont deserve this!
 
Kwa hakika Lowasa anastahili kuongoza nchi hii. Juhudi na bidii yake wenyewe mliona kwa kipindi kidogo sana alichokaa katika nafasi ya waziri mkuu. wale wote wanaobeza mfano wa hizo shule za kata hakika wanakosea kuwa ni za kifisadi. Angalia maandalizi hayo yanavyokuja kuwa sambamba na walimu wanaomaliza mafunzo yao, tayari kufundisha mwnafunzi awapo darasani !!!!! Je walioingia baada wameongeza nini tofauti na hizo walizozikuta. Je hujashuhudia Tbc ikirusha kipindi kinachoonyesha wanafunzi wanaokaa nje (uwanjani kufanya mitihani asubuhi kabla jua halijachomoza sana kwa sababu ya ukosefu wa madarasa ya kutosha, tena katika mji mkuu wa nchi hii wanapokutanika wabunge wote wanaolipwa mapesa kibao toka katika kodi za walala hoi ????????????????? Namuunga mkono Lowasa. Jipe moyo mkuu.
 
ZIPOMPAPOMPA, kama Lowassa ni rafiki yako wa kweli hebu muulize na aseme ukweli toka moyoni mwake, ni kitu gani kinachomfanya alazimishe kupata madaraka? Tatizo lenu nyie hamumshauri vizuri huyu mzee, munachoangalia ni "mrungura" tu, mukiishavuta basi. Kama unakiri kuwa hata ukimwita mtoto wa darasa la 4 na ukamuuliza Fisadi ni nani atakwambia Edward Lowassa, je, maneno haya huwa munamwambia? Na kwa uelewa huo, je unaona bado ana nafasi ya kuongoza Taifa hili?

Mkuu nimekuvulia kofia. Umempa somo ambalo kama kweli anampenda Lowassa atamueleza ili asiendelee kuunguza fedha zake (japo hana uchungu nazo). Sasa kama hata watoto wadogo wanaona kwamba ufisadi na Lowassa ni synonimous, hii habari ya kwamba anachagulika na anastahili kuwa rais anaitoa wapi. Au ataua kizazi chote ili kije kipya? Halafu atawahi uchaguzi wa 2015? Huyu baba limemchwea na sasa zimebaki hasira tu na juhudi tasa za wapambe wake kuingia humu na kila thread za kumsifia na kuchafua wenzake. Wapambe wamegeuka kuwa stick za kupimia oil ya gari!
 
Huwezi kumfananisha Edward Lowassa MWIZI na Mizengo Pinda MWADILIFU. Ndugu yangu ZIPOMPAPOMPA hebu jitokeze kidogo utujibu maswali yetu ili tukupe undani wa UCHAFU wa LOWASSA. Baada ya kutoka kwa Mch. Joshua wa Nigeria, LOWASSA ameonekana bungeni akisalimiana na kila mtu, nina wasi wasi kwa kasi ile atasalimia mpaka kivuri. Hizi ni dalili za kuchanganyikiwa zaidi maana sasa ameonesha wazi kuwa hawaamini viongozi wa dhehebu lake na akaamua kwenda kuombewa Nigeria. Kila mtu mwenye uelewa anajua sifa kubwa ya Nigeria ktk matumizi ya nguvu za giza. Bila aibu mwanaume huyu alitua huko kwa maombezi.

Ukiona mtu anafanya importation ya uchawi ili kujaribu kushinda urais, hapo ujue kwamba wachawi wa ndani wamejaribu lakini hali ya "mgonjwa" imezidi kuwa mbaya na mgonjwa katoka wodini kwenda ICU. Lakini la kujiuliza ni je, hivi mpaka unatumia nguvu za giza, huko ikulu umeweka nini? On a very serious note: Kama Lowassa atagombea urais, basi mimi pamoja na kutoipenda Chadema, niko tayari kuwaunga mkono hata kama watamsimamisha dreva wa Mbowe kuwa mgombea maana najua siyo MWIZI!
 
Mwanae Lowassa amenukuliwa mara kadhaa akidai kuwa wao wameikamata "media house" hapa nchini, lakini mbona wanashindwa kumsafisha Lowassa kama kweli amechafuliwa kwa kuonewa na kwamba yeye ni msafi? Tunachokiona sasa hivi ni kuchafuliwa kwa viongozi wengine kwa gharama za kumsafisha Lowassa. Mpango huo hautafanikiwa kwani ndio munazidi kuwapandisha ktk nafasi ya juu hao munaodhani munawachafua.
Hivi wewe ZIPOMPAPOMPA unaamini kuwa ukimshauri LOWASSA kwenda kufanya mkutano wa hadhara pale Jangwani atakubali kufanya hivyo? Unaweza kubuni nini kitakachotokea? Hebu jaribuni muone.

Mimi najua kitakachotokea. Atarudi akiwa na POP na aiwa hana nguo ya ndani maana wananchi watakuwa wamesogezewa mwizi wao karibu. Hizo media house ni New Habari Corporation na Tanzania Daima? Nani anayasoma hayo majarida ya udaku?
 
Maisha waswahili wanasema ishi na watu vizuri watakutumikia (kwa maana nyengine utakuwa kiongozi wao), kinyume cha msemo huu ni kwamba ishi na watu vibaya watukuchukia. Washabiki wa Lowassa mwambieni akagombee Monduli kwengineko wananchi watampiga mawe kwani ameacha makovu tangu baba wa taifa alipompiga chini asigombee akisema hafai kuongoza nchi. Mtu gani kila anapoongoza watu wanakutuhumu wewe ni fisadi ingelikuwa kikundi cha watu wachache tungelisema wanachuki binafsi but sio watu wote. Kuanzia AICC hadi uwaziri mkuu ukimuuliza kila aliyefanya nae kazi husema jamaa ni fisadi. Ndio faida yake hiyo atafute urais sayari nyengine (Neptune au Pluto) na sio Duniani especially Tanzania kwani wananchi watamtandika na mawe hasa waislamu!!!!
 
*Asema chokochoko zimetokana na kujivua gamba
Na Debora Sanja, Dodoma



MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, amesema hawezi kujiuzulu nafasi hiyo hadi uchaguzi wa chama utakapofanyika mwaka 2014.

Alisema kauli zilizotolewa hivi karibuni za kumtaka ajiuzulu ni kauli za wanachama wachache zinazoongozwa na viongozi wanaoleta fujo kutokana na kutakiwa kujivua gamba ndani ya chama hicho.

Alisema mara baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu mwaka jana, TLP iliunda tume ya kuchunguza kwa nini chama hicho hakikufanya vizuri katika uchaguzi huo. Chama hicho kilipata kiti kimoja tu cha ubunge katika Jimbo la Vunjo. Mrema ndiye aliyepata kiti hicho.

Alisema tume ya watu watano iliyoongozwa na Alhaji Hamad Mkadam ilitoa mapendekezo katika kikao cha Uongozi wa Juu wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya chama hicho.

"Katika kikao hicho kilichofanyika Mei 23, 2011, sekretarieti ilipokea mapendekezo hayo ambayo miongoni mwayo ilikuwa ni chama kutoendelea na shughuli yoyote hadi viongozi waliosababisha TLP kufanya vibaya katika uchaguzi mkuu wajivue gamba.

"Mtu wa kwanza aliyetuhumiwa alikuwa Katibu Mkuu, Meja Jesse Makundi, ambaye alikubali ku-resign (kujiuzulu) na aliandika barua yake Mei 25, mwaka huu.

"Hiyo ripoti haikunitaja popote, hata hivyo katika chama mimi peke yangu ndiye niliyepigania hadi nikapata ubunge, ambao pia unanifanya niwe karibu na Serikali. Hivyo siwezi kujiuzulu, kwanza nijiuzulu kwa lipi? Muda wa kujiuzulu ni wakati wa uchaguzi wa chama mwaka 2014," alisema.

Alisema mbali na wanachama, kiongozi mwingine aliyetakiwa kujiuzulu alikuwa ni Naibu Katibu Mkuu, Rajab Hamad Tao, ambaye hajajiuzulu.
Aidha, alisema TLP haina mgogoro wala mpasuko wowote na hatua yake ya kujivua gamba ni mkakati wa kukisafisha chama hicho.

Mrema alisema Halmashauri Kuu ya TLP itaitishwa Julai 9, mwaka huu ili kuzungumzia malumbano hayo ikiwa ni pamoja na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2014.

Mrema anatambulika kama bingwa wa kupambana na kuwashinda wabaya wake kwenye migogoro iliyoibuka kwenye vyama kadhaa alivyopitia.
Akiwa NCCR-Mageuzi, alipambana na kundi lililotaka kumng'oa hadi akalishinda. Hali kama hiyo ilijitokeza tena TLP, ambako aliweza kumtimua hadi mwasisi wa chama hicho, Leo Lwekamwa.

 
Unable to change the Title...

Mrema: Sijiuzulu ng'o; Asema chokochoko zimetokana na kujivua gamba
 
Heading na content ya ndani mbona haziendani?
 
Jamani mbona huyu spika wetu anaonekana na hasira za karibu sana? Maana anakuwa kama presha inapanda wakati akitokea mbunge kuomba mwongozo au utaratibu anakuwa kama anataka kupiga mayowe... Hivi home kwake inakuwaje huyu mama?
 
sijui hata kama akiwepo watoto/wajukuu zake wanashika hata remote kuangalia tv...
 
Back
Top Bottom