Kwanini lakini, why?

Abdulhalim

Platinum Member
Jul 20, 2007
17,193
3,011
Let see..

Nna swali MUHIMU. Linaeza kuonekana la kijinga..lakini hio haliondoi validity yake.

and the question is,,.

WHY DO WE CHOOSE COMPETITION OVER COLLABORATION?

Chukulia mfano wa uchaguzi unaokuja wa 2010. Kwanini watu wana-confine akili zao na resources kwenye ku-compete? Kwa 'hao' manguli wanaodhani wanahitaji kutuongoza kuelekea kwenye promise land, kaa ideas zao kweli ni pure, naive, zenye zeal ya kuendeleza nchi kiukweli, kwanini basi at least, hawasikizani wao kwa wao na kushirikiana? hata humo ndani kwenye 'magenge' yao wanayoita vyama vya siasa hawasikizani, how can we take them serious kwamba hawana ajenga nyingine zaidi ya zile wanazohubiri?

Mchango wako tafwadhaal.
 
Katika Game Theory, game yoyote ambayo players wana-dominant strategies, outcome siku zote itakuwa non cooperation, kwa mfano ni game ya Prisoners Dillema (PD) au Tragedy of the Commons. Hii conclusion inahusisha politcal games pia ambazo zinakuwa driven na self interest za players. Hivyo usitahajabu kabisa kuona hakuna cooperation but rather competition, na chamsingi zaidi ni players kuwa na best strategies angaist their opponents inorder to maximize their payoffs. Ni vizuri kujua pia kwamba hizi competition siyo lazima ziwe effective bali zinahusisha "non credible threats" ambazo players wakiwa smart zinaweza zisisaidie sana, na matokeo yake cooperation ikawa ni njia bora yakupata matokeo mazuri.
 
Viongozi waliishia kwa Mwinyi!
Wanaofuata sasa ni washindania maslahi, na hawawezi kukaa meza moja wakashauriana-period!
 
Mchango mzuri,

Swali lilikuwa ni kwanini watu watake ku-compete? WHY?

Ukweli ni kwamba competition is based on UBINAFSI, na ukishakubali ubinafsi sidhani tena kama kunakuwa na NIA NJEMA KWA WOTE. Huu ndio msingi wa thread hii. Sasa chukua mfano wa SIASA, kaa msukumo haswa wa kugombea unatokana na UBINAFSI tunaezaje kukaa kitako kutegemea matokeo mazuri ya kumnufaisha kila mtu ? How?

Yaani ni sawa na mtu anayetaka kwenda vitani, lakini anaanza kujipiga risasi mguuni.. Je atashinda vita huyu? Sidhani.
 
Viongozi waliishia kwa Mwinyi!
Wanaofuata sasa ni washindania maslahi, na hawawezi kukaa meza moja wakashauriana-period!

Kama hawawezi kukaa meza moja wenyewe kwa wenyewe huko kwenye 'magenge' yao ya kihalifu wanayoyaita 'vyama vya siasa', tunaezaje kuwaamini hawa watu ? Kutoelewana wenyewe huko ndani ni dalili kwamba wanapunjana kwenye ulafi wao.

Na zaidi najiuliza hivi ni nani hasa ktk dunia hii ya sasa inayo-demand PESA MBELE KAMA TAI, aneweza kufanya siasa bila kuwa na njia nyingine ya kupata mkate wake wa kila siku na pengine hata kunufaika kuliko wananchi wengine wenye ajira rasmi zenye kueleweka (profession)? Mfumo uliopo unapalilia UBINAFSI, na ukasharuhusu UBINAFSI huezi tena ukazuia MBINU CHAFU, maana nia njema hutoweka.
 
Sasa chukua mfano wa SIASA, kaa msukumo haswa wa kugombea unatokana na UBINAFSI tunaezaje kukaa kitako kutegemea matokeo mazuri ya kumnufaisha kila mtu ? How?

Hili wazo linanikumbusha kadhia fulani fulani. Kuna majimbo fulani fulani ya kisiasa ambayo wananchi wake walichagua wawakilishi wa upinzani, matokeo yake yale majimbo 'yaliadabishwa' kwa kutokupelekewa huduma fulani fulani ukilinganisha na majimbo jirani yalikuwa yamechagua wawakilishi wa chama twawala. Sasa ushindani unaenda kuleta kinyongo na kama nilivosema NIA NJEMA inatoweka na jamii kutaabika.

Back
Top Bottom