Kwanini kwenye sherehe chakula kinawekwa mwisho?

Kwanini kwenye sherehe chakula kinawekwa mwisho?

BABA SANIAH

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2013
Posts
4,777
Reaction score
6,267
waungwana nauliza tu.katika sherehe nyingi mambo ya nyam nyam,
maakuli
ulaji
misosi
hua inawekwa mwisho,hivi ni kanuni,sheria,au utaratibu tu,na kwa nini ufanane,kwa nini chakula kisiwekwe mwanzo.
hebu tujuzane angalau kidogo wadau wa jamii forum.
 
waungwana nauliza tu.katika sherehe nyingi mambo ya nyam nyam,
maakuli
ulaji
misosi
hua inawekwa mwisho,hivi ni kanuni,sheria,au utaratibu tu,na kwa nini ufanane,kwa nini chakula kisiwekwe mwanzo.
hebu tujuzane angalau kidogo wadau wa jamii forum.
Nishakula nimeshiba nikae nasubiri nini sasa?
 
kwani tunafuata kula au lile tukio,kama kula tunakula kila siku waungwana,cha maana lile tukio,kwa mfano harusi tunatakiwa tule then tusheherekee,au vipi wadau
 
50℅ hadi 60℅ watu kwenye sherehe huwa mnafuata msosi.
Sasa pata picha watu wakishashiba nini kitaendelea.


Harafu sijui why tu msosi wa kwenye sherehe unakuwa mtamu kuliko kuliko wa nyumbani na kwingineko.

Mti wenye matunda.
 
Tembelea kwanza ofisi za NIDA wewe utakua sio mtanzania
 
espy ,wewe ukila tu unasepa eeh
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kabisa mkuu, bahati mbaya huwa kinakuwa mwishoni. Kuna wakati huwa nasepa hata kabla ya msosi nakuwa nimekunywa maji yangu tu maana nakuwa nimechoka alafu mambo mengi yasiyo ma msingi.
 
Jamaaa umeamua utoe jibu lenye ukakasi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimeona tunaulizwa maswali ya kitoto, yaani utadhani huyu mwenyewe kawahi kufanya hasara hiyo ya kuandaa msosi kwa watu then sherehe. Kwa kifupi tunasema tunaenda shughulini na siyo tunaenda hotelini/mgahawani.
 
Wenzetu wa Kenya hula kwanza ndipo ratiba nyingine zinafuata.

Ni utamaduni mbovu tu tuliojijengea coz kama ni kula ningeweza kaa mahali nikala kwa gharama ndogo kuliko hata ninayotumia kwenye sherehe.

Nadhani sababu ni kwakuwa tunaalika watu wengi ambao hata si wa karibu yatu. Imagine unafunga ndoa ukaalika marafiki na ndugu zako wachache wa karibu sana, wanaweza kula mwanzo na kuondoka kweli? Zaidi itafanya wawe karibu, wachangamfu, wenye furaha na kila mmoja kuiona sherehe ni yake.

Haya mambo ya kuwapa kadi watu wakuchangashie, wanampa yoyote wanayemjua ndio yanafanya sherehe zikose ustaarabu. Kama ni harusi wanakuja watu hawawajui hata maharusi...kazi kupiga kelele tu na kufanya vituko.
 
Back
Top Bottom