Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,498
- 37,792
Naomba msaada wa ufafanuzi toka Kwa Watanzania wenzangu. Tangu Jana majira ya saa 6:10 usiku kuna Watanzania wameanzisha nyuzi humu JF na mitandao mingine kuonyesha jinsi walivyo na kinyongo Kwa timu ya Taifa kutoa Sare na Algeria na hivyo kufuzu Fainali za AFCON.
NINI kiko nyuma ya chuki na makasiriko haya maana si kawaida Mtoto wa Mtu kufaulu mtihani halafu mzazi wake akanuna. Huwa nasikia kuna wazazi wanachukia watoto wao kufaulu pale wanapokuwa wamepanga kuwaozesha au kama ni wa kiume kuwatumia kuchunga mifugo. Lakini pia wazazi wengine huwa wanachukia sababu ya kuwa na uwezo mdogo kiuchumi.
Sasa hii Hali ya baadhi ya mashabiki àmbao hawachangii hata 100/= kugharamia timu kuchukia mafanikio ya timu ya Taifa Lao inatokana na Nini?