Indume
Member
- Apr 11, 2011
- 81
- 37
Kitabulisho cha Taifa kilichoanza kutolewa hivi majuzi na mkuu wa nchi kina lengo la kumtambulisha raia na kusaidia mamlaka mbalimbali kujua uhalali wa shughuli zako na mchango wako katika pato la Taifa.
Kulingana na jinsi kinavyosomeka, imeonekana kuwa waandaaji ambao ni serikali hii isiyokuwa makini wamekurupuka kabisa kuandaa vitambulisho vyenye sifa ya U-taifa.
Kwanza, kuna mkanganyiko wa matumizi ya lugha iliyotumika. Kwa kiswahili kuna sehemu inasomeka "Majina ya kati" lakini kwa tafsiri waliyoiwekwa wao kwa kiingereza ni "Middle name" badala ya middle names.
Pili, Kitambulisho hiki cha uraia kinasomeka kuwa kitafikia muda wake au mwisho wa matumizi yake ni mwaka 2023 (Expiring date is 2023), ikiwa na maana kuwa ifikapo mwaka 2023 uraia wako wa kuitwa wewe ni Mtanzania utakoma.
Swali langu ni kuwa inakuwaje kama kweli mimi ni mtanzania na nimepewa uraia kwa nini uraia wangu una expiring date??
Kwa maana ingine basi mwaka 2024 watanzania wote akiwemo na mkuu wa nchi hawatakuwa raia wa TZ, ina maana serikali na vyombo vyake vitaachia ngazi.
Kwa maeneo hayo, inaonekana mamlaka zilizojihusisha na kushughulikia mchakato wa kuandaa vitambulisho vya Taifa either hawakujua cha kufanya au wamekurupuka na kushinndwa kabisa kutengeneza vitambulisho vyenye hadhi ya Kitaifa.
Ombi langu ni kuwa ni afadhali Passport ziendelee kutumika kuliko kutumia hivyo vitambulisho vya taifa, na ikiwezekana viandaliwe vitambulisho vingine vyenye hadhi ya kitaifa kwa kuwatumia wataalamu makini.
Thanks.