Kwanini kulinganisha jezi ya Simba na Yanga?

Kwanini kulinganisha jezi ya Simba na Yanga?

888I

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
445
Reaction score
553
Vilabu vinazindua jezi nzuri.Swali ninalojiuliza ni kwanini vyomba vya habari mtandaoni, wanahabari mtandaoni na watu wengine mtandaoni wanalinganisha jezi za timu mbili tofauti wakihoji Jezi Gani Kali ? 😳 Huwa na maana Gani ?

Binafsi nafikiri Haina mantiki yoyote kwani Azam mashabiki wake watanunua jezi za timu yake na kadhalika kwa kila shabiki wa timu nyingine.Ni nadra sana kukuta shabiki wa Simba hajanunua jezi kwasababu shabiki wa Yanga amesema jezi ya Simba ni Mbaya na si nzuri ya ya Yanga.

Kwa wanahabari kuna kitu kinaitwa 5W+H lakini sikuhizi tunaongeza kile Cha SO WHAT? unalinganisha ili Nini kitokee ? Nafikiri tunapaswa kutoa habari na kupokea maoni kuliko kuanzisha mjadala wa namna hiyo ama weka vigezo ama vipimo vya jezi nzuri ama Bora inatakiwa kuwa vipi Kisha mashabiki watakwenda kupima jezi za timu zao.
 
Wenzako wako kwenye marketing braza Ile ni biashara lazima ipigwe promo Kila upande maana mtu kutoa 45000 sio rahisi
 
Watu wa Simba na Yanga Wana maisha Yao Tabia zao Mila zao na desturi tamaduni zao tofauti kabisa na wananchi wengine wa tanzania.

Wewe waache TU,
 
Back
Top Bottom