Watu wengi wamekuwa hawafahamu nini wanahitaji maishani mwao, wengi hata kufikiria kuwa hawatoweza kuishi bila kazi au ajira. wanacho sahau ni kuwa ajira ni derived demand ila wao wanahitaji kipato ili kuendesha maisha yao na kipato sio lazima uajiriwe.
Chanzo: ChapishaBlog
1. Utakua na kipato kidogo ambacho ni lazima ukifanyie kazi.
Pindi utakapo chagua maisha ya kuajiriwa, kipato chako kitakua kikitegemea mshahara tu. Wengi wenu mna dhana kuwa kuna manuva na madili mengine ofisini mtayafanya ili kuongeza kipato, na je yasipokuwepo?.
LAbda kutakua na overtime allowances lakini ni lazima ufanye kazi kwa muda mrefu ikibidi hadi usiku, na kushangaza zaidi hakuna atakaejali nguvu na juhudi zako kwani si unalipwa.
Je ushawahi kufikiria njia tofauti ya kuingiza kipato hata kama haupo kazini, ukiwa unapata breakfast, safarini au mapumzikoni lakini pesa bado zikawa zina flow kwenye kampuni yako mwenyewe.
Fikiria kujiajiri na uanze kutengeneza kipato chako mwenyewe bila masharti wala bughza za kuamka alfajiri kuwahi ofisini.
2. Utakosa ujuzi wa mambo mengi maishani mwako.
Wengi mnafikiria kuwa ukiajiriwa utapata experience si ndiyo, basi wacha nikujuze kitu ndugu, pale ni unapata uzoefu juu ya ile kazi tu na sio ujuzi wa maisha kiujumla wake.
Maisha yako yatakua kama robot na ya upweke sana, wangapi mmewasikia waki jitetea kwamba natamani kufanya kitu Fulani ila nimebanwa na kazi za ofisini. Au kwa wadhifa Fulani wa ofisi si ruhusiwi kufanya mambo Fulani, au kwa hadhi yangu yangu siweza kwenda maeneo Fulani.
3. Utaishi maisha kama mfugo kwa boss wako.
Kuajiriwa kwa hivi sasa ni sawa na kuwa mfugo Fulani ndani ya ofisi (No offence), na ni kwa kuwa mfugo mwema tu ndipo utadumu ofisini.
Kwa nafananisha kuajiriwa ni kama mfugo?, Maisha yako yote utakapo kua kazini utakua ukipongezwa tu pale unapo mfurahisha boss wako (Mfugaji wako) maana yeye ndiye anayekuweka mjini.
4. Kuajiriwa ni kunufaisha wengine badala yako.
Wafanya kazi kwa sasa naweza kusema ndio walipa kodi wazuri na wakubwa, wafanya kazi wengi hawakwepi kodi. Kodi ya kila aina amewekewa mfanya kazi kwa sababu ni rahisi kuipata kutokana inalipwa moja kwa moja na mwajiri wake.
Hadi kodi ya pango la ofisi ambapo mfanya kazi anakaa kufanya kazi zake zinalipwa na mfanya kazi mwenyewe.
Umeshawahi kujiuliza hizo pesa za kulipia kodi ya pango kwenye magorofa mazuri ya mjini zinatoka wapi?, Jibu ni zinatoka ofisini baada ya wewe kuzizalisha.
Wawekezaji kwa maana ya ma-investors pia wana lipwa kutokana na juhudi na uchapa kazi wako. Mara tatu ya utakachokua ukilipwa kitakua kinakwenda kwa wawekezaji na wewe kulipwa kiduchu ya kilichobaki. Mjinga si ndio wewe?
5. Kuchagua ajira ni kuchagua njia ya mashaka sana.
Waajiriwa wengi na hata wewe mmekua mkifikiria kuwa kuajiriwa ndio njia salama ya kupata kipato cha uhakika pasipo wasiwasi wowote. Dhana hii imejenga mmiongoni mwa watu wengi sana kuwa mwisho wa mwezi utafika hela itaingia.
Waajiriwa wengi wanaona wako very secured wakati wakiwa kazini kitu ambacho sio kweli, unawezaje kuhisi uko sehemu salama wakati vyanzo vyako vyote vya mapata vinatokana na seheme moja tu?!
Boss anaweza kuzuia chanzo chako cha kipato just kwa kusema maneno mawili tu Kazi basi. Pindi uwambiwapo maneno haya ina maana, housing, transport, meal allowances and other per DMs ndio basi, kwishneh.
Pind utapo amua kufanya na shughuli zako mwenyewe ndipo utakapo kua na vyanzo mbalimbali vya wewe kujipatia kipato hata kama njia moja imebuma basi unageukia upande au kwenye bidhaa ya pili, ni kama tu dukani kwa mangi wapo watakao kopa lakini wapo watakao toa cash, hivi vikidoda vile vinanunuliwa habari ndio hiyo.
6. Maisha yako sehemukubwa yatakua ni utumwa na kunyenyekea.
Utumwa wa kujitakia, ndio kuingia kwenye ajira ni kuingia kwenye utumwa wa kujitakia mwenyewe kwa hiyari yako.
kwani utakua ni mzee wa ndio boss. Siku zote utakazokua kibaruani wewe utakua ni ndio boss, sawa mkuu, kweli muheshimiwa hata kama unaona vitu haviko sahihi.
Na ole wako ikatokea siku moja ukaenda kinyume na vile (slave master) boss wako anavyotaka ndipo utakapotambua dhahiri kuwa wewe ni mtumwa wake kwani utatakiwa kuomba misamaha kwa kila aina ya style. Muda mwingine unaweza hadi ukapewa kitu kinachoitwa karipio kali.
Lakini hiyo itakua tofauti na pale utakapoamua kufanya shughuli zako binafsi, pindi ukoseapo na kwenda njia isiyo sahihi ukigundua una turn back na kutafuta wapi ulipokosea ili usonge mbele. Ni tofautini na ofisini ambapo utatakiwa kusema nisamehe Boss.
7. Ukikubali kuajiriwa, umekubali maisha ya kuwa ombaomba.
Kwanza ningependa utambue kwa takwimu zisizo rasmi wafanya kazi wengi ndio wana ongoza kwa consumer loans, hata ukija mtaani kwenye daftari la mangi wakopaji wengi utakuta ni wafanyakazi.
Endapo utaamua kuajiriwa basi tambua kwamba pindi utakapo hitaji kuongeza kipato (mshahara) chako basi inabidi uwanze kuomba na kumbembeleza kwa boss hadi akuelewe, and guess what inabidi umuelezee boss shida zako hadi akuelewe. Haahah!.
Kumbuka pindi utakapoajiriwa sio wewe utakae kuwa ukiamua ulipwe kiasi gani bali ni boss wako au mmiliki wa kampuni, ndio mwenye last say. Utumwa gani huo!
8. Ajira hupunguza ujamaa na ushiriikiano ndani yako.
Nadhani utakua na fikra kwamba pindi unapokua kwenye ajira au upatapo kazi ndi utakua na chance ya kutengeneza marafiki wapya, kujuana na watu kutengeneza channels za michongo na connections mbalimbali.
Kama una fikra hizo basi tambua you are wrong my friend, kwani ofisin utaruhusiwa au kujiruhusu ku share ideas only na watu wa level yako watu walewale ambao mko katika field mmoja tu.
Ukiwa muhasibu hutopata nafasi ya kuwa na urafiki na wafanya usafi hata kama mnapandaga gari moja kuja ofisini. Boss (Master) wako atakusha ngaa kukuona unaongea na mfagiaji.
Ishu hapa ni kwamba una hitaji kuji socialize na watu wa kila aina iwe unafahamu au hufahamu namaanisha hata wale walio tofauti na wewe.
9. Kupungua kwa uhuru binafsi
Pindi uwapo kazini, kampuni itabidi iwajibike ku didimimza uhuru wako binafsi. Wengi mtabisha mkidhani kwamba mko huru kufanya chochote unachotaka ofisini lakini kumbe nyuma ya pazia ni kuwa mmeshaiva katika nguzo zote za utiifu.
Cha kwanza kabisa wanachofanya ni kuwapa sera ndefu na ngumu ya kampuni ili uendane nayo. Ni katika sera za kampuni mtu hulazimishwa kufikiria, kuvaa (dress code) muda mwingine hadi kuongea kama kama shirika linavyotaka.
Katika kipengele cha mfanyakazi bora au mtiifu ni Yule tu atakae weza kwendana na sera za kampuni lakini si kwa matakwa yake bali ni woga wa kuwajibishwa at the end.
Sera na kanuni hizo kwa watu waliopevuka na wasiopenda kuajiriwa kwao huziona kama kandamizi na michosho.
Kanuni kuu ni tumia akili uungwana, fanya upendacho, furahia maisha
10. Ni maandalizi ya kuwa muwoga wa maisha.
Kama unafahamu wafanyakazi wengi ndio watu wanaongoza kwa malalamiko juu ya ofisi na makampuni wanayoyatumikia. Lakini bado wame ngangana tu ndani ya ofisi kama sio woga wa maisha ni nini?
Unafanya kazi sehemu ambapo unashindwa hata kuthubutu kumwambia boss kuwa wewe ni lofa pale anapozingua au kucheza na maslahi yako muhimu alafu unajifanya wewe sio muoga, ohh man unajidanganya.
Popote pale utakapokua ukifanya kazi utakua ukizungwa na makundi ya waoga wenzako, na utakua ukishirikiana nao hadi pale utakapo asili njia hiyo ya maisha. Bado muda unao na hujachelewa kama unataka kubadili mawazo muda ndio huu, maisha ni yako uamuzi ni wako badilika sasa.
Bado unataka kazi?
Sitafuti kazi CC: Niki Wa Pili
Chanzo: ChapishaBlog