Kwanini kinywaji cha Mbege Kinaonjwa kwanza kabla ya kupewa mteja

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Nimepita sehemu mtu kanunua mbege ila kabla hajaanza kunywa akamwambia muuzaji aonje kwanza(Ria), kwanini Mbege tu na sio Bia sijawai ona mhudumu kafungua bia na mteja kumwambia Onja.

Kwanini Mbege?

Wataalamu wa Mila mtujuze hapa.
 
Nadhani hiyo ilikuwa ni nembo ya upendo kwa wana kaskazini so haina nia mbaya kama unavyotaka kutuaminisha mkuu
 
Nimepita sehemu mtu kanunua mbege ila kabla hajaanza kunywa akamwambia muuzaji aonje kwanza(Ria), kwanini Mbege tu na sio Bia sijawai ona mhudumu kafungua bia na mteja kumwambia Onja.

Kwanini Mbege?

Wataalamu wa Mila mtujuze hapa.

Kipindi cha nyuma, Wachaga walikuwa wanauana sana kwa sumu kwenye vinywaji na vyakula, hivyo ndio huo utaratibu ukawepo kuwa muuzaji lazima anywe kidogo ili kuthibitisha kuwa hiyo pombe ni salama
 
Sio mbege tu. Ni karibu pombe zote za kienyeji(zinazokuja wazi) Na hio ni uthibitisho kuwa mama muuza hajaweka kitu kibaya. Hata kwetu wanafanya hivo hivo
 
Back
Top Bottom