Kwanini kila uchaguzi wa CHADEMA ukikaribia, CCM na wenzenu huleta hoja ya ubadhirifu wa hela?

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Wakati Freeman Aikaeli Mbowe⁩ anachukua nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Taifa kutoka kwa mzee Bob Nyanga Makani, alikuta kuna Wabunge wa 5 na Madiwani wasiozidi 75 nchi nzima. Wabunge wasioweza hata kujaza sebule yenu hapo.

Leo tukielekea kwenye uchaguzi mkuu mwingine wa ndani wa CHADEMA, Mwezi Desemba, 2019 CHADEMA kuna Wabunge zaidi ya 65 madiwani zadi ya 1500 nchi yote, halmashauri za kutosha na wanaunda kambi ya upinzani bungeni (KUB)

Hivyo ni vyema wewe "kijana - baro baro" wa leo mwenye kuendeshwa na "mihemko" kutambua haya mafaniko makubwa kabla ya kusema "Mbowe ameiua CHADEMA", inawezekana hujui hata CHADEMA imefikaje hapa ilipo leo, sio miujiza, ni STRATEGIES!

Kuna Vijana wa leo, labda kwa mihemko na juhudi za kutumika hawajui nguvu iliyotumika, jasho lililomwagika hadi kuifanya leo CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani. Wanadhani ni kitu rahisi kama kucheza 'BIKO na TATU MZUKA'

Hatusemi kwamba Freeman Mbowe ni malaika, kwamba hakuna dosari na makosa kwenye uongozi wake, hapana, isipokuwa jasho, damu na machozi yake yamemwagika kwa ajili ya CHADEMA, tuhuma zenu zinapaswa kuwa 'Valid' wakati wa kumkosoa, tuhuma za JINAI zithibitishwe!

Freeman Aikaeli Mbowe ni mwenyekiti halali wa CHADEMA, na ataondoka madarakani siku wanachama wa CHADEMA wakisema "imetosha" kupitia mkutano mkuu, sio kwa sababu "Kuna kelele za CCM na mapandikizi" huko nje za "Mbowe ondoka! Mbowe ondoka!"

Mzee Bob Makani alikuwa na kadi namba Tatu ya CHADEMA, kadi namba Mbili ilikuwa ya Mzee Brown Ngilulupi na kadi namba moja ya Mzee Edwin Mtei, hawakukosea kamwe kumuona Freeman Mbowe na kumkabidhi CHADEMA ambayo ameifanya kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Mwisho, kimsingi, CHADEMA imebarikiwa kuwa na mwenyekiti kama Freeman Mbowe, wengine tuliopata fursa ya kufanya nae kazi au kukutana nae, tunajivunia sana, he's a man and a-half! Stay blessed Chairman!

estamos juntos en esto, presidente!

#MMM, Martin Maranja Masese
 
Mbinu ya kishamba isiyolipa na ambayo haijawahi kufanikiwa , nadhani ccm wangeendelea na ile mbinu yao ya mauaji na utekaji tu , lakini hii ya majungu wanapoteza muda tu
 
Well I wouldn’ know much about it not being a member of CDM or any political party for that matter but it seems to me that Mr Mbowe has not only done very well, he has also held up excellently under the prevailing conditions. No doubt he is an astitute, tough, resilient and resourceful politician. A political survivor wilful enough to withstand the persecutions that always follows visionarys of his calibre as well as the inevitable mudslinging without minding his personal losses. As an impartial observer I think with the support of his party,he might get the Tanzanian opposition somewhere.
 
Back
Top Bottom