Kwanini kila kitu tunatolea mfano Kenya?

gagonza

JF-Expert Member
Oct 18, 2009
309
98
kumekuwa na kawida watu wengi hata viongozi kila wana chosema wanafananisha na kenya,je hakuna nchi nyingine ya kutolea mfano? pili sisi hatuna vitu ambavyo wakenya wanaweza kujifunza kutoka kwetu?
 
Wakenya wanatakiwa kijifunza mambo mengi ya msingi toka TZA e.g kuishi kwa amani kati ya watu wa dini mbali mbali, + kutokuwa na ukabila, etc
Ila na sie tujifunze! hasa hili moja ambalo kwa sasa hakuna nchi yeyote afrika au ulimwenguni ninayoijua mie ambayo ina katika nzuri kama Kenya.tena inafanya kazi. Cheki jinsi walivyo itumia, kuwaengua majaji wabovu,kupata jaji mkuu competent, + viongozi wengine wengi, na sasa wako wanaitumia kupata New Polisi Chief.

The way you choose,identify your leaders will determine what you will get out of them. For us tanzania we have more than enough examples on this topic.
 
kumekuwa na kawida watu wengi hata viongozi kila wana chosema wanafananisha na kenya,je hakuna nchi nyingine ya kutolea mfano? pili sisi hatuna vitu ambavyo wakenya wanaweza kujifunza kutoka kwetu?
Ndugu yangu, wengi wetu hatujielewi. Mtu ana passport imegongwa muhuri wa kenya tu wala hakuna hata Mauritius au Morocco japo, unadhani atajipatia ujiko kwa kujionyesha ametembea kwa nchi gani? Ni kutokujithamini na kutofahamu kuwa hapa kwetu tumewahudumia hao wakenya, waganda, wazambia, malawi, mozambique, Zaire, Burundi, Rwanda , Angola na South Africa. Ndiyo maana huwa sielewi mtu anukuwa inferior kisa kamuona msouth au mkenya ambaye nchi yake ulijengwa na wazungu na sasa inagawanyika wakati sisi watanganyika tunaijenga wenyewe kwa mikono yetu bila shida. Taraibu tutafika wao ndiyo wamejaa hapa kutwa kucha kung'ang'ania madada zetu ili wapate uraia. Yani ningekuwa mwana$mke wa kitanzania mimi, wangenikoma!
 
Watanzania wengi wana akili za kuazima,ni mpaka hapo watakapoanza kutumia akili zao ndio watakapojitambaua.
 
Tunatolea mfano wa Kenya kwa sababu ni nchi iliyo karibu na sisi na ni rahissi kwa mtanzania kufika au kujua taarifa zake.Kenya ni nchi jirani ambayo licha ya kuwa na mazingira kama ya kwetu kwa kiasi fulani bado wamepiga hatua kuliko sisi.Ni nchi jirani inayotuzidi kiuchumi licha ya sisi kuwa na utajiri wa maliasili kuliko wao.Huwezi kutolea mfano nchi za mbali wakati mfano wa karibu na unaoeleweka upo.Wana Mombasa,tuna Dar lakini bado tunajikongoja.Wana Lamu,tuna Tanga,wenzetu wanajenga bandari kubwa huko sisi Tanga imebaki porojo na makabrasha makabatini.china ana historia ndefu na sisi kuliko Kenya lakini kampuni zao zote zinaweka makao makuu yao Nairobi na kuingia mikataba mikubwa na serikali ya Kenya...Wenzetu kwa ushapu wao wanapata mega deals kutoka world bank na ADB kuendeleza miundo mbinu yao.Angalia Highway ya Thika wanayoitambia ni juhudi za ushapu wao huku sisi miradi yetu mikubwa kama hilo daraja la Kigamboni ikichukua miongo mitatu,reli ya Dar-Kigali haisikiki tena...ni mambo mengi sana ambayo tulifaa tuwe mbele yao lakini ndio hivyo tunabaki kuwaita nyang'au zaidi ya hapo hatuna usemi.
 
Watanzania wengi wana akili za kuazima,ni mpaka hapo watakapoanza kutumia akili zao ndio watakapojitambaua.

Hili la Watanzania wengi wana akili za kuazima halijakaa vizuri. Unaposema wengi unamaanisha "Majority" ie. Zaidi ya 50% ya Watanzania wanatumia akili za kuazima. Sikubaliani na wewe. Ukisema baadhi ya Watanzania ni sawa.
 
kumekuwa na kawida watu wengi hata viongozi kila wana chosema wanafananisha na kenya,je hakuna nchi nyingine ya kutolea mfano? pili sisi hatuna vitu ambavyo wakenya wanaweza kujifunza kutoka kwetu?
nadhani ni kwa sababu ya jinsi hawa jamaa wanavyotuangalia sisi. Hebu chukulia hii scanario ya karibuni alafu ujipe jibu!

Embakasi MP Ferdinand Waititu has apologised for urging the eviction of the Maasai from his constituency. The MP said his remarks targeted night watchmen, many of them, from Tanzania, who also happen to be Maasai. He said the blanket condemnation caught on tape was a “slip of the tongue”.

Source: nation.co.ke
 
Tukatae tukubali ila ukweli unabaki kuwa hawa jamaa wametupita kwa vingi na hata tunapofanya nao kazi utaona kabisa the level of seriousness, aggressiveness na akili ya serving for future investments. On top ukiacha Nigeria na South Africa ndio the leading fast growing economy in Africa...Tutafakari na kuchukua hatua!
 
Tunatolea mfano wa Kenya kwa sababu ni nchi iliyo karibu na sisi na ni rahissi kwa mtanzania kufika au kujua taarifa zake.Kenya ni nchi jirani ambayo licha ya kuwa na mazingira kama ya kwetu kwa kiasi fulani bado wamepiga hatua kuliko sisi.Ni nchi jirani inayotuzidi kiuchumi licha ya sisi kuwa na utajiri wa maliasili kuliko wao.Huwezi kutolea mfano nchi za mbali wakati mfano wa karibu na unaoeleweka upo.Wana Mombasa,tuna Dar lakini bado tunajikongoja.Wana Lamu,tuna Tanga,wenzetu wanajenga bandari kubwa huko sisi Tanga imebaki porojo na makabrasha makabatini.china ana historia ndefu na sisi kuliko Kenya lakini kampuni zao zote zinaweka makao makuu yao Nairobi na kuingia mikataba mikubwa na serikali ya Kenya...Wenzetu kwa ushapu wao wanapata mega deals kutoka world bank na ADB kuendeleza miundo mbinu yao.Angalia Highway ya Thika wanayoitambia ni juhudi za ushapu wao huku sisi miradi yetu mikubwa kama hilo daraja la Kigamboni ikichukua miongo mitatu,reli ya Dar-Kigali haisikiki tena...ni mambo mengi sana ambayo tulifaa tuwe mbele yao lakini ndio hivyo tunabaki kuwaita nyang'au zaidi ya hapo hatuna usemi.

well said ! I luv u !
 
kumekuwa na kawida watu wengi hata viongozi kila wana chosema wanafananisha na kenya,je hakuna nchi nyingine ya kutolea mfano? pili sisi hatuna vitu ambavyo wakenya wanaweza kujifunza kutoka kwetu?

Kwasababu Mlima Kilimanjaro uko Kenya. Au?
 
There is alot that Tanzanians can learn from Kenyans and vice-versa but we are like China and India, so keen to put each other down.
 
sasa cc watanganyika tumeshugulika na ufisadi tuu hata leo pia ikiwa wazanzibar watakuwa kivyao basi tutatolea mfano wao kwani tunajuwa walivyo
tuwache kulala watanganyika wakati umefika sisiem kuondoka
 
Kuna hadithi moja ya zamani kwa ufupi inasema hivi. Siku moja kipofu alifunuliwa macho kimiujiza, kitu alichokiona kwanza ilikuwa punda, halafu macho yakafumbwa. Kwa hiyo yule kipofu kila anachoambiwa au kusifiwa anauliza "kama punda?". Akiambiwa kuna gari kubwa limepita, yeye anauliza "Kama punda?" nk, Hivi ndivyo ilivyo kwa ndugu zangu wadanganyika, kila kitu kama Kenya? kila kitu kulinganisha na Kenya, hao ni kama vipofu. Hata hao wenzetu wa Kenya kuna mambo ya Tz ambayo wana yasifia na kuyaona mazuri. Kadhalika hata watu toka sehemu nyingine duniani kuna mambo yetu ambayo wanayapenda na wangependa yafanywe ktk nchi zao. Nimeeleweka sina sababu ya kutoa mfano, labda wanajamvi wengine wanisaidie.
 
Tusidanganyane kwa kupakana mafuta,picha wanaionyesha viongozi wetu,wasomi wetu na maneno wanayoongea ndani na nje ya nchi ni reflection of what we are as a whole country,watanzania tumekuwa watu wa kuthamini wazungu,kusifia vya wenzetu na hata kujishusha thamani mbele ya wageni.Mara ngapi tumesikia viongozi wetu na hata vijana wasomi wakilikataa shirikisho la Afrika Mashariki kisa wakenya watapora ajira zao? Hao wakenya wengine mbona wamesoma na wengine wanasoma kwenye vyuo vyetu!!!

Back
Top Bottom