Kwanini kila ajali ya basi la mohamed inahusisha kupasuka tairi?

Jamani,
Tatizo kubwa la mabasi hayo kwa uzoefu wangu ni mwendo mkali nu kua na inexperienced drivers si mnajua wabongo kwa kupenda cheap laboureres? SUMATRA, TRAFFIC MPO?
 
Pole kwa wafiwa.
Naamini sisi JF tunaweza (wanaosafiri kipindi hikikutoka dar to mikoani) kuendesha uchunguzi na kuja kubandika hapa matokeo yake. Tuyachunguze mabasi ya mikoani kama yanafuata ratiba na kama yanapita checkpoint ontime. pia wakati wa kuchimba dawa shuka uangalie tairi za gari kama kashata zake zipo au zimelika hata kidogo.
Then tuangalie speed za dereva anapokaribia miji midogo maana wanakatiza kana kwamba wanafukuzwa na shetani nyuma. Baada ya hapo leta ripoti hapa jukwaani. endapo wahusika (najua wanasoma humu) hawatafungua macho yao na kutafuta suluhisho basi tujue wamelogwa.

Tusikae na kulaumu tujitahidi kuchukua hatua hata kama ni ndogo lakini ni hatua
 
huyo jamaa anatakiwa afuatiliwe kwa umakini sana na kila ajali lazima gari lake lipasuke tairi na kugongana na lingine si mnakumbuka ajali iliyopita aligongana na dereva wa coka cola?halafu wanasema hakuwa mwendo mkali embu angalia gari ilivyoharibika mbele na coastal aliyogongana nayo ndio haitamaniki kabisa!!mimi nadhani ifike wakati hata habiria tusiwaonee aibu madereva mara tunapoona anakwenda mwendo mkali tusisite kumweleza kwani tukikaa kimya matokeo yake ndio haya tunapoteza watu wasio na hatia!mbona makampuni ya dar express,kilimanjaro nk hawapati ajali kihivyo?tunamuomba tajiri wa muhamed akae chini na kufikiri ni njia gani anazotakiwa kuzifuata ili kuepuka hili hii kweli inakera sana na ni aibu!na amwogope na mungu pia kwa kuwa makini na magari yake kwakweli haipendezi na inauma sana!
 
Mi nadhani tatizo ni elimu kuhusu matairi, naambatanisha hapa hii document pengine itawasaidia wengi kamam ilivyonielimisha mimi.

, nisaidieni jinsi ya kuattach file hapa maana naona imenishinda
 
kwa nijuavyo mimi mabasi haya yamejengwa kwa bodi ngumu na chesisi nzito sana kiasai matairi yanshindwa kuhimiri uzito yanaobeba,na ndio maana utaona matairi yote yaliyopasuka kwenye ajari hizo ni ya mbele kunakokuwa na mzigo mkubwa na tairi ni mbili tu[moja kila upande]
 
Unapokuwa na serikali ya kizembe, uvundo wake hushuka hadi ngazi za chini.

Mampuni ya mabasi yanapolimbikiza ajali bila serikali kuu (Waziri, Rais) kuingilia kuangalia ni nini hasa vyanzo vyake na jinsi ya kurekebisha, basi tusishangae zikiendelea kujirudia na wahusika wakitoa sababu mchwara huku watu wakiendelea kupoteza maisha.

Wakati wa kumlaumu Mohamed Trans n.k., umeshapita. Lawama sasa zielekezwe serikalini, Mawaziri husika na Rais JK mwenyewe kwa kushindwa kulinda usalama wa raia wake.
 
Kama ni imani za kishirikina hili liko dhahiri na wazi kabisa.
Kila ajali inayohusisha mabasi ya mohamed, utasikia tairi lilipasuka.
Kila mwaka wanauwa watu wengi mno ambao wamefanya kosa kubwa moja la kuiamini mohamed trans na kuwalipa nauli ili wafike kwao.
Jamani hawa mohamed hawajifunzi kutokana na makosa, kwanini wasitafute matairi imara na madhubuti ambayo wasafirishaji wengine wamekuwa wakiyatumia?

Kama wewe ni mtu mzima ningependa kujua umri wako na elimu uliyo nayo.
 
Kama ni imani za kishirikina hili liko dhahiri na wazi kabisa.
Kila ajali inayohusisha mabasi ya mohamed, utasikia tairi lilipasuka.
Kila mwaka wanauwa watu wengi mno ambao wamefanya kosa kubwa moja la kuiamini mohamed trans na kuwalipa nauli ili wafike kwao.
Jamani hawa mohamed hawajifunzi kutokana na makosa, kwanini wasitafute matairi imara na madhubuti ambayo wasafirishaji wengine wamekuwa wakiyatumia?
kama kweli ni ushirikiana waambie watafute matairi ya chuma,alafu utasikia nayo yamepasuka ndio utaujua ukweli,kwani ni ajali ngapi zinahusisha kupasuka tairi,au ndio kujisaidia ajisaidie kuku,akijisaidia bata kaendesha?
 
Do sijui watakubali nirudishe tiketi yao kwani nimekata kusafiri kesho na hilo limeniogofya:(
wewe kama ni wa ajali ni wa ajali tuu,hata usiposafiri unaweza dondokewa na ukuta na ahadi ikatimia,kwani ni abiria wangapi wameshasafiri na mabasi ya kampuni hii pasipo pata ajali,au unataka kusema kila siku yanaajalika?ulipokata tiketi hukujua kuwa ni mohamed trans ndio ulilokata?
 
Kama ni imani za kishirikina hili liko dhahiri na wazi kabisa.
Kila ajali inayohusisha mabasi ya mohamed, utasikia tairi lilipasuka.
Kila mwaka wanauwa watu wengi mno ambao wamefanya kosa kubwa moja la kuiamini mohamed trans na kuwalipa nauli ili wafike kwao.
Jamani hawa mohamed hawajifunzi kutokana na makosa, kwanini wasitafute matairi imara na madhubuti ambayo wasafirishaji wengine wamekuwa wakiyatumia?

Hapa ni Swala moja tu la kukimbia huduma za hili basi mpaka Wakose wateja!
 
Kama ni imani za kishirikina hili liko dhahiri na wazi kabisa.
Kila ajali inayohusisha mabasi ya mohamed, utasikia tairi lilipasuka.
Kila mwaka wanauwa watu wengi mno ambao wamefanya kosa kubwa moja la kuiamini mohamed trans na kuwalipa nauli ili wafike kwao.
Jamani hawa mohamed hawajifunzi kutokana na makosa, kwanini wasitafute matairi imara na madhubuti ambayo wasafirishaji wengine wamekuwa wakiyatumia?
siri hiyo wanaijua wenyewe...
 
Siamini ushirikina,lakini kuna madai kuwa kuanguka kwa magari hayo na kuchinja watu ni njia ya kutambikia ,udaku wa mitaani ni kuwa likianguka moja na kuua anaingiza matatu mapyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
pia ebu tazama tiketi za mabasi hayo zina alama ya madini(dhahabu) kuna uhusiano gani na hilo walio karibu MD TRS COMPANY watupe data
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom