Jamani hebu tafakari kwa nini Kikwete hakuwa na furaha jana na kwa nini sherehe hazikuwa na shamrashamra. Jadili
Sababu ya kwanza ni kuwa anajua watanzania wana imani ndogo na yeye na umati ule hajui ni asilimia ngapi walikuja kwa kumdhihaki tu au wana mapenzi ya kweli naye. Anajua watanzania wanaelewa mchezo mchafu ulifanyika na hivyo alikuwa na 'guilty conscience'.
Pili, ameporomoka sana umaarufu wake ndani ya miaka mitano ya uongozi wake. Mwaka 2005 watu wengi walikuwa na matarajio makubwa toka kwake. Performance Threshold waliiweka juu sana wakiamini ni mchapa-kazi na hivyo atafanya makuu. matokeo yake ameshindwa hata kukaribia pale walipotazamia, maskini afadhali angekuwa si popular wakati ule (bado najiuliza kwa nini alikuwa so popular kiasi cha mtu kusema atamchagua yeye ukimuuliza sababu hana zaidi ya kusema nampenda tu JK!!).
Anajua jamii ya wasomi haimuungi mkono, mtaji wake mkubwa umekuwa ni wale 'wasioelewa zaidi mambo' tuseme asilimia kubwa bado ni 'wajinga' na kwa kuwa anaelewa ujinga huondoka mtu akielimishwa, basi ana wasiwasi na hatima ya CCM wajinga wakielimika. Kushuka toka 84% mwaka 2005 hadi 61% mwaka huu lazima imnyime raha.
Mwisho ni ahadi alizotoa kwenye ilani na zile za free-style, ambazo hata yeye anajua hawezi kuzitekeleza. Na kwa kuwa anajua watanzania wanaelimika kwa kasi, aatkuwa anaulizwa juu ya utekelezaji wa ahadi hizo miaka yote mitano kila akifanya ziara za ndani ya nchi...labda aamue kufanya ziara za nje ya nchi (kama kawaida yake) na za ndani awaachie waziri mkuu na mawaziri wengine.
Kama msafara wake ulipigwa mawe Mbeya hapo nyuma, sasa hivi anahofia matukio ya namna hiyo kutokea zaidi mahali pengi nchini.
Kama alikuwa hana furaha, basi naamini hizo ni miongoni mwa sababu zilizopelekea hali hiyo.
MUNGU ibariki Tanzania!