Kwanini Kikwete Hakuwa na Furaha kwenye Kuapishwa?

mudushi

Senior Member
Oct 19, 2010
151
84
Jamani hebu tafakari kwa nini Kikwete hakuwa na furaha jana na kwa nini sherehe hazikuwa na shamrashamra. Jadili
 
Furaha inapimwaje? kwa kuchekacheka au kununa? i think kama kweli hakua na furaha basi ni kwasababu hakupata pongezi toka kwa mshkaji wake waliegonga nae gahawa, Obama
 
Yale matokeo ni Tathimini ya utendaji kazi wake ndo maana hakua na furaha. Hata ungekua wewe kutoka 84% hadi 61.17%. Kwamba juhudi zote alizozifanya kwa miaka mitano hakuna alicho gain kutoka kwa watanzania
 
Furaha inapimwaje? kwa kuchekacheka au kununa? i think kama kweli hakua na furaha basi ni kwasababu hakupata pongezi toka kwa mshkaji wake waliegonga nae gahawa, Obama

Unaweza kujua kama mtu kafurahi au hapana kwa kuangalia body language yake!! Jakaya body language yake ilikuwa inaonesha unyonge!! Angeshinda kwa halali ungeliona lile SMILE lake ambalo jana halikuwepo!!
 
Jamani hebu tafakari kwa nini Kikwete hakuwa na furaha jana na kwa nini sherehe hazikuwa na shamrashamra. Jadili

wewe unafanya mchezo na miahadi aliyotoa isiyotekelezeka?...hata hivyo namtakia kila la kheri ....
 
Jamani hebu tafakari kwa nini Kikwete hakuwa na furaha jana na kwa nini sherehe hazikuwa na shamrashamra. Jadili

ahadi kedekede alizotoa kwenye kampeni ziishaanza kumtafuna na kumnyima raha na ukichanganya na ukwapuzi wa kura aliofanya then anakuwa na ile kitu........guility conscious
 
mh na nyie......kwani mbona zipo sababu nyingi za mtu kukosa furaha labda alikuwa .... si mnajua mzee wetu mtu wa kudondoka kwenye majukwaa haaaaaaaaaaaaaa
 
Niliiposti hii kwa kichwa cha habari ambacho hakikuvutia ila mnaweza kuangali tathmini hii inaweza kuwapa picha ni nini kinachoweza kumpa raisi hofu na mashaka.

Total Population in Tanzania: about 35 M
Eligible population for voting: estimates from NBS projections 47% of the population about 16 Million above the age of 18.
Those who registered for voting: About 20 Million (NEC, 2010)! (against NBS projections on eligibel voters, those who are above 18 years of age)
Voted: About 9M
The elected president votes: About 5 M = 25% of all registered voters
= 32% of all eligible voters

Source: Own calculations from NEC website: The National Electrol Commission of Tanzania - Homepage [online] and from the NBS Tanzania
[online]
 
Jamani hebu tafakari kwa nini Kikwete hakuwa na furaha jana na kwa nini sherehe hazikuwa na shamrashamra. Jadili

Sababu ya kwanza ni kuwa anajua watanzania wana imani ndogo na yeye na umati ule hajui ni asilimia ngapi walikuja kwa kumdhihaki tu au wana mapenzi ya kweli naye. Anajua watanzania wanaelewa mchezo mchafu ulifanyika na hivyo alikuwa na 'guilty conscience'.

Pili, ameporomoka sana umaarufu wake ndani ya miaka mitano ya uongozi wake. Mwaka 2005 watu wengi walikuwa na matarajio makubwa toka kwake. Performance Threshold waliiweka juu sana wakiamini ni mchapa-kazi na hivyo atafanya makuu. matokeo yake ameshindwa hata kukaribia pale walipotazamia, maskini afadhali angekuwa si popular wakati ule (bado najiuliza kwa nini alikuwa so popular kiasi cha mtu kusema atamchagua yeye ukimuuliza sababu hana zaidi ya kusema nampenda tu JK!!).

Anajua jamii ya wasomi haimuungi mkono, mtaji wake mkubwa umekuwa ni wale 'wasioelewa zaidi mambo' tuseme asilimia kubwa bado ni 'wajinga' na kwa kuwa anaelewa ujinga huondoka mtu akielimishwa, basi ana wasiwasi na hatima ya CCM wajinga wakielimika. Kushuka toka 84% mwaka 2005 hadi 61% mwaka huu lazima imnyime raha.

Mwisho ni ahadi alizotoa kwenye ilani na zile za free-style, ambazo hata yeye anajua hawezi kuzitekeleza. Na kwa kuwa anajua watanzania wanaelimika kwa kasi, aatkuwa anaulizwa juu ya utekelezaji wa ahadi hizo miaka yote mitano kila akifanya ziara za ndani ya nchi...labda aamue kufanya ziara za nje ya nchi (kama kawaida yake) na za ndani awaachie waziri mkuu na mawaziri wengine.

Kama msafara wake ulipigwa mawe Mbeya hapo nyuma, sasa hivi anahofia matukio ya namna hiyo kutokea zaidi mahali pengi nchini.

Kama alikuwa hana furaha, basi naamini hizo ni miongoni mwa sababu zilizopelekea hali hiyo.

MUNGU ibariki Tanzania!
 
nafikiri anajua ya kuwa, mwaka huu bunge lake limekuwa la moto kuliko tangu tumepata uhuru, hivyo atakuwa na kazi nzito kiasi kwamba anauona uprezo mgumu sana kipindi hiki. kama vipi ajiuzuru basi...
 
Jamani hebu tafakari kwa nini Kikwete hakuwa na furaha jana na kwa nini sherehe hazikuwa na shamrashamra. Jadili

wacheni majungu JK alikuwa bomba ameapa kwa kujiamini zaidi kuliko ilivyokuwa 2005! mwaka 2005 nilikuwa uwanjani na jana pia! hata katika hafla alikuwa anatabsamu yake ya kawaida! tafuteni jengine...! amesema ' Yaliyopita sindwele tugange yajayo..!
 
Kwa hizo 61% alizopata amefeli sema hamna vigezo vya maana vinavyotumika kutathmini, hata ingekuwa wewe semister ya kwanza chuoni ulipata 82% kwenye uchumi ambayo ni B+, ukarelax na kudhani ndo ushamaliza chuo,matokeo ya semister ya pili unaambulia 61% ambayo ni E sawa na falure u have to do supplementery (kwa chuo nilichosoma) lazima upokee hayo matokeo kwa maskitiko makubwa ukizingatia ulikuwa unaibia kwenye mitihani, ina maana hata 61% sio ya kwako, wewe marks zako za halali ni F yaani falure na unadisco immediately, hii ndio sawa na JK mwaka huu, sema kalazimisha kubaki chuoni ngija tuone kama msuli atauweza au atendeleza usanii.:doh: JK amka.
 
Ww ungepata mtihani average 61% ungefanya graduu? LAbda kama ndo wa kwanza kusoma kijijini kwenu.
 
Ule umati ulikuwa umetokea mikoa ya jirani kwani Dar jamaa hakubaliki. Kuna taarifa zilizothibitishwa kuwa kuna msg ilitaka watu watoke mikoa ya moro na kwingineko wakiwa na sare za chama ili wajaze uwanja. Kwani kwa dar peke yake tungeweza ona rangi za viti.
 
Ni %41 kikwete 2010 na sio 61...kama unavodai hata yeye anajua ndo maana roho ikawa inamsuta akawa anaficha uso akijua dhahiri kuwa watu kama sisi tunaojua tutamuangaliaje usoni...hiyo ndo fact.....
 
Amedrop sana alafu kwa upande mwingine ukichangia na uchakachuaji basi dhamira yake inamsuta
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom