Balozi wa Marekani nchini, Bw. Mark Green amesema kuwa serikali ya nchi yake haijaombwa na Serikali ya Tanzania kumrudisha nchini aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Daudi Balali.
Alisema kwa kiasi kikubwa, hatua kama hizo zitategemea maamuzi yatakayochukuliwa na Serikali ya Tanzania kuhusiana na jambo hilo.
Hata hivyo, alisema wao wako tayari kumsaidia Rais Jakaya Kikwete kushughulikia ombi litakalofanikisha utekelezaji wa azma hiyo kama ipo.
Bw. Green alikuwa akijibu maswali ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake ambapo aliwaita kuzungumzia ujio wa Rais George Bush nchini mwezi ujao.
Alipoulizwa mahali alipo hivi sasa Dk. Balali huko Marekani, Balozi huyo alijibu kwamba hajui na kuongeza kwamba sheria za Marekani hazimruhusu kutangaza nyendo na mahali walipo watu wanaoishi Marekani.
Kuhusu uwezekano wa kurudishwa nchini fedha zinazodaiwa kuchotwa BoT endapo sehemu yake imehifadhiwa kwenye mabenki ya Marekani, alisema kwa kuzingatia sheria za nchini mwake, fedha kama hizo zitafuatiliwa na hata kama zilipitia katika mkondo wa benki za Marekani.
Alisema suala la kurudishwa kwa fedha (kama zipo), kama ilivyo katika kumrejesha Balali, kwa kiasi kikubwa pia litategemea maamuzi ya Serikali ya Tanzania.
Aidha, kuhusu habari zilizozagaa kuwa Dk. Balali alipatiwa uraia wa Marekani kwa njia ya Green Card, alisema kuwa mtu yeyote anayeomba viza maana yake siyo raia wa Marekani na kwamba Balali aliomba viza miaka miwili iliyopita kwa wadhifa aliokuwa nao kama Gavana wa BoT.
Alisema, juhudi za Rais Kikwete kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa ni miongoni mwa mambo ambayo Rais Bush atayazungumzia akiwa nchini.
Tanzania ni miongoni mwa nchi tano za Afrika ambazo zitatembelewa na Rais George Bush wa Marekani mwezi ujao. Nchi zingine ni Rwanda, Benin, Ghana na Liberia.
- SOURCE: Nipashe
Jamani Watanzania;Balali haji hai hapa.Hapa dili linasukwa kati ya JK na Mr Bush kwa exchange ya mali za watanzania ili kuhakikisha Balali anarudishwa maiti.Balali yeye anafikiri yuko salama mikononi mwa Marekani.Wakishahakikisha wamemtwanga sumu ndo JK atajifanya kuomba Balali arudishwe.Sasa anabuy time kuhahkisha wamempata Balali anayejifanya amejificha.
Balali ndugu yangu huna guarantee ya kuishi zaidi ya kumwaga ukweli sasa.Hii issue ni mbaya kuliko sisi tunavyoijua ubaya wake:Mkuu wa kaya anashikwa ugoni,yatakuwa mambo ya Mfalme Daudi na Mke wa jemadari wake(Abigairi)
Tom karibu jamvini,
Uchunguzi wa fedha za EPA ulishaanza siku nyingi na tunaambiwa wapo ambao wamerudisha fedha. Mpaka wakati huu marehemu Balali kama mtendaji mkuu ktk BOT alipaswa kuwa ameshahojiwa na timu ya Mwanasheria Mkuu na wenzake ili kufanikisha uchunguzi wao. Kusema marehemu alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa saa 24 wakati hata Hospitali aliyokuwa anatibiwa Serikali haiijui ni mchezo wa kitoto,utayajuaje mgonjwa yuko mahututi wakati hujui hata alipo?
JK kama alikuwa anadhamira ya kweli ya kumrudisha ahojiwe,angekubali offer ya US kumrudisha na wao ndio wangesema hayo ya kuwa yuko chini ya uangalizi wa madaktari saa 24 ngojeni kwanza.
Ukweli una baki palepale kuwa kulikuwa na sababu za kutotaka maelezo ya marehemu Balali yapatikane kwa uwazi.
Hivi Tanzania si nchi inayoendeshwa kisheria? Kama ni nchi inayoendeshwa kisheria basi mamlaka ya kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote hayapo mikononi mwa rais.
Thread yangu niliyoianzisha hapa ikapigwa vita sana na kuhamishwa...Ile iliyokuwa ikisema.."Kikwete akataa Ballali Asiletwe"
Sasa tumeshagundua kuwa that was the case...Ila tunabaki na fununu tu huku Ballali mwenyewe keshakufa!
Thread hii inawakaribisha wale wote ambao sasa wanaamini kuwa Kikwete ni kweli hakutaka Ballali aje,na pia wale wote ambao tunajiuliza ni sababu gani hasa iliyomfanya asitake Ballali kuletwa na kuhojiwa licha ya kwamba ni wazi kuwa alikuwa ndio shahidi na mtuhumiwa wa kwanza na ndio maana akafutwa kazi.
Na pia kulazimishiwa na wamarekani ili amuhitaji lakini akagoma!Wamarekani waliona kuwa Ballali ni mtuhumiwa lakini yeye hakuona hivyo!
Pia tunajiuliza kuwa ripoti hiyo ambayo haijajumuisha mahojiano tunayoyajua sisi dhidi ya kamati na Ballali.
Pia kwa wale ambao wana maoni yao binafsi kuwa sasa Tanzania iwe na mwelekeo gani baada ya mambo haya na ni nini cha kufanya ili kuweza kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa Mtanzania.
BALALI RESIGNATION LETTER

)Quote:
Originally Posted by Nyangumi
Jamani Watanzania;Balali haji hai hapa.Hapa dili linasukwa kati ya JK na Mr Bush kwa exchange ya mali za watanzania ili kuhakikisha Balali anarudishwa maiti.Balali yeye anafikiri yuko salama mikononi mwa Marekani.Wakishahakikisha wamemtwanga sumu ndo JK atajifanya kuomba Balali arudishwe.Sasa anabuy time kuhahkisha wamempata Balali anayejifanya amejificha.
Balali ndugu yangu huna guarantee ya kuishi zaidi ya kumwaga ukweli sasa.Hii issue ni mbaya kuliko sisi tunavyoijua ubaya wake:Mkuu wa kaya anashikwa ugoni,yatakuwa mambo ya Mfalme Daudi na Mke wa jemadari wake(Abigairi