Kwanini Kikwete alikataa kumleta Ballali?

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,756
22,015
Thread yangu niliyoianzisha hapa ikapigwa vita sana na kuhamishwa...Ile iliyokuwa ikisema.."Kikwete akataa Ballali Asiletwe"
Sasa tumeshagundua kuwa that was the case...Ila tunabaki na fununu tu huku Ballali mwenyewe ikisemekana kuwa keshakufa!

Thread hii inawakaribisha wale wote ambao sasa wanaamini kuwa Kikwete ni kweli hakutaka Ballali aje, na pia wale wote ambao tunajiuliza ni sababu gani hasa iliyomfanya asitake Ballali kuletwa na kuhojiwa licha ya kwamba ni wazi kuwa alikuwa ndio shahidi na mtuhumiwa wa kwanza na ndio maana akafutwa kazi.

Na pia kulazimishiwa na wamarekani ili amuhitaji lakini akagoma! Wamarekani waliona kuwa Ballali ni mtuhumiwa lakini yeye hakuona hivyo!
Pia tunajiuliza kuwa ripoti hiyo itakuwa ni ripoti ya aina gani ambayo haijajumuisha mahojiano tunayoyajua sisi dhidi ya kamati na Ballali.

Pia kwa wale ambao wana maoni yao binafsi kuwa sasa Tanzania iwe na mwelekeo gani baada ya mambo haya na ni nini cha kufanya ili kuweza kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa Mtanzania.
 
Hii hapa ni linki ya wale wote wenye kutaka kuona jinsi ambavyo mpambano huu ulianza kitambo hapa jf!Kongoli hapo upate uhondo wakati huo haijapelekwa kwenye "Vibweka vya wakubwa" Celebrity forum"

Kikwete Akataa Balali Asiletwe!
 
Jibu nafikiri tumelipata. Mara BALALI AMEKUFA BOSTON, AMEKUFA DC, MASHINE ZILITOLEWA, NO DRIP ZILIKWISHA, ATAZIKWA DC, NO MWILI UTACHOMWA, NI NDUGU TU WATAMUONA, HAKUNA PICHA WALA VIDEO, HATUJUI ALIPO, TUTAMLETA TZ HAI AU MAUTI na MENGINE MENGI.

Muda wa kudanganya WATANZANIA UMEKWISHA AU UNAFIKIA UKINGONI. Hawa watu wamelipotezea TAIFA letu RASILIMALI, NGUVU NA WAKATI kwa uovu wa matumbo yao.
NO more of this S##T under our watch.

Natoa pongezi kwa tume ya Rais ya kuchunguza EPA kwa kujaribu kutumwagia mchanga machoni. Wanaweza kufanikiwa for the time being lakini nashukuru MUNGU kwa ugunduzi wa kamera kwenye cell phone, camera za kawaida, Mtandao wa JF, YOUTUBE, na mitandao mengine. Watu wataumbuka hapa na sijui watajichimbia wapi.

Time will tell ...........
 
Balozi wa Marekani nchini, Bw. Mark Green amesema kuwa serikali ya nchi yake haijaombwa na Serikali ya Tanzania kumrudisha nchini aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Daudi Balali.

Alisema kwa kiasi kikubwa, hatua kama hizo zitategemea maamuzi yatakayochukuliwa na Serikali ya Tanzania kuhusiana na jambo hilo.

Hata hivyo, alisema wao wako tayari kumsaidia Rais Jakaya Kikwete kushughulikia ombi litakalofanikisha utekelezaji wa azma hiyo kama ipo.

Bw. Green alikuwa akijibu maswali ya wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake ambapo aliwaita kuzungumzia ujio wa Rais George Bush nchini mwezi ujao.

Alipoulizwa mahali alipo hivi sasa Dk. Balali huko Marekani, Balozi huyo alijibu kwamba hajui na kuongeza kwamba sheria za Marekani hazimruhusu kutangaza nyendo na mahali walipo watu wanaoishi Marekani.

Kuhusu uwezekano wa kurudishwa nchini fedha zinazodaiwa kuchotwa BoT endapo sehemu yake imehifadhiwa kwenye mabenki ya Marekani, alisema kwa kuzingatia sheria za nchini mwake, fedha kama hizo zitafuatiliwa na hata kama zilipitia katika mkondo wa benki za Marekani.

Alisema suala la kurudishwa kwa fedha (kama zipo), kama ilivyo katika kumrejesha Balali, kwa kiasi kikubwa pia litategemea maamuzi ya Serikali ya Tanzania.

Aidha, kuhusu habari zilizozagaa kuwa Dk. Balali alipatiwa uraia wa Marekani kwa njia ya Green Card, alisema kuwa mtu yeyote anayeomba viza maana yake siyo raia wa Marekani na kwamba Balali aliomba viza miaka miwili iliyopita kwa wadhifa aliokuwa nao kama Gavana wa BoT.

Alisema, juhudi za Rais Kikwete kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa ni miongoni mwa mambo ambayo Rais Bush atayazungumzia akiwa nchini.

Tanzania ni miongoni mwa nchi tano za Afrika ambazo zitatembelewa na Rais George Bush wa Marekani mwezi ujao. Nchi zingine ni Rwanda, Benin, Ghana na Liberia.

  • SOURCE: Nipashe

Why ndugu zangu..Why???

Kwanini Kikwete alikataa kumleta Ballali na sasa anasema ni mapenzi ya Mungu yeye Kufa!

Why?

Kwamba hata wamarekani walikuwa wakimlazimishia Ballali lakini kwa ufukara wetu wa mawazo tukasema tumuamini Muungwana...Wakwapi wale waliokuwa wakimpa mwezi?

Ama walijua kuwa ndani ya Mwezi mabadiliko atakayoyafanya Kikwete ndio haya ya watuhumiwa kufa wakiwa huru na hivyo kesi kwisha?

Watanzania kweli hatutakuwa na upungufu wa akili kama tukiirudisha CCM madarakani?
 
Kwa sababu aliona ni heri atetee mafisadi waliomuingiza Ikulu kifisadi fisadi kuliko kutetea maslahi ya Watanzania.

Inasemekana wamemtisha kwamba akiwagusa tu basi wataibua mizengwe ya kifisadi yote iliyofanyika hadi yeye akaibuka kama mgombea wa chama cha mafisadi.

Sasa njemba acha iogope maana ina wasi wasi kwamba hata awamu moja inaweza isimalize kama watayaanika hadharani yaliyojiri pale Dodoma.

Kama utakumbuka alimwambia waziri mmoja wa kutoka katika nchi za wafadhili kwamba shilingi 133 billioni zilizokupuliwa BoT na zile nyingine shilingi 155 bilioni (ambazo hadi hii leo hazijachunguzwa na zilichukuliwa na Meremeta) ni pesa za Watanzania na hazikuwa za wafadhili.

Kwa maana nyingine fedha zetu ni halali kuliwa na mafisadi.
 
Mushi Hongera sana. Nakupa hongera kwa sababu katika ile thread uliyoianzisha January mwaka huu asilimia kubwa ya wachangiaji walikupiga vita labda kutokana na kichwa cha habari, lakini ulichoandika kina ukweli.

Tangu Ballali alipoondoka nchini Kikwete kama kweli angekuwa ana nia ya kuhakikisha anahojiwa basi angeiomba serikali ya US imrudishe ili akajibu tuhuma nzito dhidi yake katika taasisi aliyokuwa anaiongoza, BoT.

Pamoja na US kutoa offer ya kumrudisha Ballali lakini Kikwete hakusema lolote kuhusiana na offer ile. Hatuhitaji Kikwete atamke hadharani kwamba alikataa Ballali kurudishwa nchini, lakini vitendo vyake vinaashiria hivyo. Kwa mantiki hiyo basi hoja yako ilikuwa na ukweli.

Halafu katika kupitia thread ile haraka haraka nikakutana na hii toka kwa mwenzetu Nyangumi aliyoituma January 30, 2008 basi nikabaki mdomo wazi.

Jamani Watanzania;Balali haji hai hapa.Hapa dili linasukwa kati ya JK na Mr Bush kwa exchange ya mali za watanzania ili kuhakikisha Balali anarudishwa maiti.Balali yeye anafikiri yuko salama mikononi mwa Marekani.Wakishahakikisha wamemtwanga sumu ndo JK atajifanya kuomba Balali arudishwe.Sasa anabuy time kuhahkisha wamempata Balali anayejifanya amejificha.

Balali ndugu yangu huna guarantee ya kuishi zaidi ya kumwaga ukweli sasa.Hii issue ni mbaya kuliko sisi tunavyoijua ubaya wake:Mkuu wa kaya anashikwa ugoni,yatakuwa mambo ya Mfalme Daudi na Mke wa jemadari wake(Abigairi)
 
Ila nimekubali mafisadi ni soo babake... duuuu! Yaani unaambiwa wamemfanyia plastic sugery Balali na kumshauri abaki Marekani maisha yake yote yaliyobaki , then wakaishauri familia yake zitangaze msiba na waseme watazika kulekule marekani... na hairuhusiwi mtu wa nje ya wanafamilia kuhudhuria kwa kuwa mtashtukia kwamba anayezikwa ni maiti iliyonunuliwa mortuary ya hukohuko majuu na kuvikwa sura ya balali.

Then baada ya hapo wabongo mnaletewa picha za mazishi kama vile kafariki kweli..... loooo kama hamjashtukia hilo mmeliwa!!!! Poleni eeeee wabongo wenzangu kwa kulishwa mchanga wa macho!!!!!!

Mafisadi Hureeeeeeeee! Mkapa, Chenge, Mgonja, Mramba, Kikwete, Lowasa, na wengine wote naona mna-toast glass za wine tu kushangilia dili kutimia... Mna akili fyetu nyie !!!!
 
Halafu tangu lini Kikwete amekuwa Daktari ? Jee yeye ndiye aliyeufanyia Autospy mwili wa Balali mpaka aseme ilikuwa natural death .Mimi nadhani there is more to this story that what we have been told .
 
Tusiwe wepese wa kujumuisha mambo. Hakuna ushahidi kwamba JK alikataa kumrudisha Marehemu Balali.
Alichokifanya JK kwa nafasi yake ni kutengua uteuzi wa marehemu kutokana na udhaifu aliounyesha katika kuidhinisha fedha za EPA.

Hilo ndilo lililokuwa jukumu lake la msingi baada ya taarifa ya wakaguzi kukabidhiwa kwake. Sasa kwa kuwa mengine ilikuwa ni lazima yafuate mkondo wa kisheria kwa kuzingatia kuwa nchi inaendeshwa kwa misingi ya utawala wa sheria,ilibidi auunde tume kuchunguza makampuni yaliyotajwa na repoti ya wakaguzi kuhusika kuchukua fedha za EPA.

Sasa kamati ilishaanza kazi,JK hakuwa na haja tena ya kuingilia majukumu ya kamati.Alichokuwa anasubiri ni kamati kukabidhi repoti kwake. Ni upotoshaki mkubwa kwamba Marekani ilishamuona Balali kama shahidi mkuu. Marekani ni taifa linalozingatia haki na sheria kwa kila raia. Sio rahisi kuropoka vitu wasivyokuwa na uhakika navyo mpaka mamlaka zinazohusika kisheria zithibitihse.

Alishosema Balozi ni kwamba "kama wakimuhitaji" hii ni sentensi muhimu kuilielewa, sio kukurupuka tu. Ilikuwa ni maoni ya jumla,sio kwamba kwa kusema hivyo balozi alikuwa anatoa msimamo wa nchi kwamba Balali ni shahidi muhimu. Na majuzi tumesikia taarifa ya Ikulu kwamba kama serikali ingemhitaji isingekuwa shida kumpata.

Harafu tusisahau kwamba marehemu Balali alikuwa ni mgonjwa wakati huo. Alikuwa ni mgonjwa kweli kweli. Alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa masaa 24 mpaka anafariki dunia.

Sasa mtu anapohoji kwa nini JK hakumrudisha mgonjwa nyumbani kutoka kwenye uangalizi wa madaktari,nadhani mtu huyu ana matatizo ya akili kama sio kusukumwa na hisia za jazba sizokuwa na msingi wowote.

Tukumbuke JK ni kiongozi wa nchi,sio rais kilabu cha mpira.Hawezi kukurupuka kufanya maamuzi kwa kila anachokisikia kwa lengo la kuwafurahisha baadhi ya watu.Hiyo sio misingi ya utawala wa sheria.
 
Mr Tom
Tom karibu jamvini,
Uchunguzi wa fedha za EPA ulishaanza siku nyingi na tunaambiwa wapo ambao wamerudisha fedha. Mpaka wakati huu marehemu Balali kama mtendaji mkuu ktk BOT alipaswa kuwa ameshahojiwa na timu ya Mwanasheria Mkuu na wenzake ili kufanikisha uchunguzi wao. Kusema marehemu alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa saa 24 wakati hata Hospitali aliyokuwa anatibiwa Serikali haiijui ni mchezo wa kitoto,utayajuaje mgonjwa yuko mahututi wakati hujui hata alipo?
JK kama alikuwa anadhamira ya kweli ya kumrudisha ahojiwe,angekubali offer ya US kumrudisha na wao ndio wangesema hayo ya kuwa yuko chini ya uangalizi wa madaktari saa 24 ngojeni kwanza.
Ukweli una baki palepale kuwa kulikuwa na sababu za kutotaka maelezo ya marehemu Balali yapatikane kwa uwazi.
 
Last edited by a moderator:
Tom karibu jamvini,
Uchunguzi wa fedha za EPA ulishaanza siku nyingi na tunaambiwa wapo ambao wamerudisha fedha. Mpaka wakati huu marehemu Balali kama mtendaji mkuu ktk BOT alipaswa kuwa ameshahojiwa na timu ya Mwanasheria Mkuu na wenzake ili kufanikisha uchunguzi wao. Kusema marehemu alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa saa 24 wakati hata Hospitali aliyokuwa anatibiwa Serikali haiijui ni mchezo wa kitoto,utayajuaje mgonjwa yuko mahututi wakati hujui hata alipo?
JK kama alikuwa anadhamira ya kweli ya kumrudisha ahojiwe,angekubali offer ya US kumrudisha na wao ndio wangesema hayo ya kuwa yuko chini ya uangalizi wa madaktari saa 24 ngojeni kwanza.
Ukweli una baki palepale kuwa kulikuwa na sababu za kutotaka maelezo ya marehemu Balali yapatikane kwa uwazi.


Hivi Tanzania si nchi inayoendeshwa kisheria? Kama ni nchi inayoendeshwa kisheria basi mamlaka ya kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote hayapo mikononi mwa rais.
 
Kwa wale wote walioko Tanzania ama mahali popote pale duniani na wanataka tuendelee na madai ya haki then wagonge hapo chini na wajiunge na watu wengine kama...Haki Ngowi,Basila mwanukuzi,Solo Thang na wengineo..Tulioko USA tuendeleze mapambano na walioko Bongo mfanye the same...Ila mjiunge kwenye hii group niliyoianzisha huko face book
 
Hivi Tanzania si nchi inayoendeshwa kisheria? Kama ni nchi inayoendeshwa kisheria basi mamlaka ya kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote hayapo mikononi mwa rais.

Itakuwa ni sheria ya kinamna gani hiyo ambayo ilimweka Ballali kwenye kundi la wasiohitajika either kama mashahidi ama mtuhumiwa?

Haukumbuki kuwa barua iliandikwa na Mama Meghji kwa Ballali kuwa pesa ni za usalama wa taifa?

Ballali si alimwambia Mama kuwa Kikwete ndiye aliyetaka iwe hivyo kuwa barua iandikwe kutoka serikalini kuwa hizo pesa zitatumika kwa ajili ya usalama wa taifa?

Na baada ya kushtukiwa Mama si aliandika barua ya pili ili kui cancel ile ya kwanza na kusema eti Ballali alimdanganya baada ya yeye mama mwenyewe kugundua kuwa si Kikwete aliyetoa hiyo Rhuksa ya pesa kutolewa?

Sasa ili tujue kama si Kikwete aliyemwambia Ballali aruhusu hizo pesa then kwanini hakuhojiwa wala Kikwete kutaka ahojiwe?

Si ndio ule mchezo wa kinyume nyume kuanza kwenye hukumu halafu ndio uchunguzi?

Pesa kuanza kurudishwa si ndio kuanza na hukumu halafu uchunguzi si ndio baaada ya jambazi kufa?

Ndio sheria zetu hizo huh?
 
Thread yangu niliyoianzisha hapa ikapigwa vita sana na kuhamishwa...Ile iliyokuwa ikisema.."Kikwete akataa Ballali Asiletwe"
Sasa tumeshagundua kuwa that was the case...Ila tunabaki na fununu tu huku Ballali mwenyewe keshakufa!
Thread hii inawakaribisha wale wote ambao sasa wanaamini kuwa Kikwete ni kweli hakutaka Ballali aje,na pia wale wote ambao tunajiuliza ni sababu gani hasa iliyomfanya asitake Ballali kuletwa na kuhojiwa licha ya kwamba ni wazi kuwa alikuwa ndio shahidi na mtuhumiwa wa kwanza na ndio maana akafutwa kazi.
Na pia kulazimishiwa na wamarekani ili amuhitaji lakini akagoma!Wamarekani waliona kuwa Ballali ni mtuhumiwa lakini yeye hakuona hivyo!
Pia tunajiuliza kuwa ripoti hiyo ambayo haijajumuisha mahojiano tunayoyajua sisi dhidi ya kamati na Ballali.
Pia kwa wale ambao wana maoni yao binafsi kuwa sasa Tanzania iwe na mwelekeo gani baada ya mambo haya na ni nini cha kufanya ili kuweza kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa Mtanzania.

BALALI RESIGNATION LETTER
 

Attachments

  • BALALI.doc
    60 KB · Views: 91
BALALI RESIGNATION LETTER

Naomba pia tuanzie huu mjadala kwenye source yenyewe...

The core of the point...Ballali mweyewe ambaye amesubiriwa afe.

Naomba tuanzie nyuma kidogo...

Na ndio maana nimeipost ile thread ya mwanzo ya Kikwete akataa Ballali asiletwe!

Naomba pia uipitie na utajifunza mengi tuliyokuwa tukiyajadili kuhusu issue hii ya Ballali wakati huo january ambapo alikuwa mzima wa afya kabisa tena nje ya hospital..Mtaani kama sisi na labda akisoma thread hiyo!

Tuanze na ule mvutano wa barua ya Mama Meghji yenye kusema kuwa pesa zitolewe kwa niaba ya serikali kwa ajili ya usalama wa taifa...

Halafu alisema kuwa Ballali alimwambia kuwa hiyo amri ni ya Ikulu na hivyo aandike hiyo barua ili iwekwe kwenye mafaili kuwa serikali ndio iliyotoa amri pesa zitolewe kwa ajili ya usalama wa taifa.

Baada ya dalili za mambu kugundulika...Mama Meghji akaandika barua nyingine ili kuipinga ile ya kwanza!

Barua ya pili ilidai kuwa taarifa alizopewa na Ballali kuwa Kikwete ndiye aliyeoda hizo pesa zilitolewe kwa usalama wa taifa si za kweli!

Sasa ili kujua ukweli...Nani mwingine aliyestahili kuulizwa kuhusu huu mvutano wa Meghji,Kikwete na Ballali kama si Ballali mwenyewe?
 
Ooooh Kikwete What A Disgrace Are You This Was The Issues We Trusted You With 80 Percent Vote Ole Wake Agombee Tena, Mwanza Unakumbuka Yule Mganga Wake Alimgeuka Jamaa Yuko Ndani Sasa,jamaa Alikuwa Anatupa Messege,kwamba Muungwana Ni Feki.
 
Thread yangu niliyoianzisha hapa ikapigwa vita sana na kuhamishwa...Ile iliyokuwa ikisema.."Kikwete akataa Ballali Asiletwe"
Sasa tumeshagundua kuwa that was the case...Ila tunabaki na fununu tu huku Ballali mwenyewe keshakufa!
Thread hii inawakaribisha wale wote ambao sasa wanaamini kuwa Kikwete ni kweli hakutaka Ballali aje,na pia wale wote ambao tunajiuliza ni sababu gani hasa iliyomfanya asitake Ballali kuletwa na kuhojiwa licha ya kwamba ni wazi kuwa alikuwa ndio shahidi na mtuhumiwa wa kwanza na ndio maana akafutwa kazi.
Na pia kulazimishiwa na wamarekani ili amuhitaji lakini akagoma!Wamarekani waliona kuwa Ballali ni mtuhumiwa lakini yeye hakuona hivyo!
Pia tunajiuliza kuwa ripoti hiyo ambayo haijajumuisha mahojiano tunayoyajua sisi dhidi ya kamati na Ballali.
Pia kwa wale ambao wana maoni yao binafsi kuwa sasa Tanzania iwe na mwelekeo gani baada ya mambo haya na ni nini cha kufanya ili kuweza kuhakikisha kuwa haki inapatikana kwa Mtanzania.

Alikataa kumrudisha kwa sababu alifahamu fika nini kinaendelea na mwisho wake ndio huo.
 
Kama Kikwete Anaakili Timamu Asigombee Mwaka 2010 Hata Mkewe Akilia Askilize Manake Wake Zao Wana Tabia Za Kulia Wakishindwa,oohhhhh What A DisgrEcy Tukikuwa Tunampamba Kwa Wshikaji Nje Sasa Ni Uchulo Huu.
 
Quote:
Originally Posted by Nyangumi
Jamani Watanzania;Balali haji hai hapa.Hapa dili linasukwa kati ya JK na Mr Bush kwa exchange ya mali za watanzania ili kuhakikisha Balali anarudishwa maiti.Balali yeye anafikiri yuko salama mikononi mwa Marekani.Wakishahakikisha wamemtwanga sumu ndo JK atajifanya kuomba Balali arudishwe.Sasa anabuy time kuhahkisha wamempata Balali anayejifanya amejificha.

Balali ndugu yangu huna guarantee ya kuishi zaidi ya kumwaga ukweli sasa.Hii issue ni mbaya kuliko sisi tunavyoijua ubaya wake:Mkuu wa kaya anashikwa ugoni,yatakuwa mambo ya Mfalme Daudi na Mke wa jemadari wake(Abigairi
)


Unaweza kuona jinsi watu walivyokuwa wakiona mengi na kuona mbali!
Lakini kauli hiyo hapo juu yaweza kuwa ya ukweli na kama thats the case then hata maisha yetu si yamo hatarini kweli?
Kwa jinsi ninavyowasumbua hawa watu huku kila siku?
Kweli Obama asiposhinda twafwa!
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom