Vision yao ni ufisadisiasa na proganda zinatuangusha.!!!
Viongozi wetu hawana vision.!!!
Sio kwamba wanapenda sifa, wanastahili sifa, ccm wakisema hatutaki tuwe kama majirani zetu mwaka 2007 walivyo twangana ni cheap politics ambazo zinaelekeza to the negative side, ukiangalia positive ni nyingi zaidi e.g, katiba mpya, barabara za mjini nairobi, data infrastructure kama uliyotolea mfano, vita ya alshabab somalia, usafiri wa reli, barabara na anga unaboreshwa kila siku etc..kwa nini wasiwe na mkonga mmoja kama wa kwetu?
kuwa na mikonga 5 maana yake nini ?
sisi tuko wengi zaidi lakini nashangaa hatuna spidi kama hawa jamaa
Kenya plans to land 5th undersea cable | balancingact-africa.com
Nazdas
kusema kuwa matatizo tuliyonayo leo yamesababishwa na nyerere unakuwa unakosea.
Kwanza kipindi cha nyerere kulikuwa na viwanda vingi sana ambavyo waliofuata walishindwa kuviendeleza.
Kipindi cha nyerere thaman ya shiling ya tanzania ilikuwa iko juu tofauti na sasa.
Tatizo la tz sio nyerere bali ni ubinafsi wa viongozi wetu walioshindwa kuendeleza msingi mzuri alioacha nyerere. Viwanda walivyobinafsisha vingi havifanyi kazi. Wameingia mikatabaa ya kifisadi tu, watu wananunua mashirika ya umma halafu wanang'oa mashine wanauza kiwanda wanafufunga. Nyerere aliweza kujenga reli ya tazara lakini mpaka leo waliomfuatia wameshindwa kujenga reli nyingine mpya na zilizokuwepo wanaziua
Nyerere kikwazo ameshakufa,waliohai wamefanya nini cha maana??au ndio tabia za kiswahili kutafuta mchawi uku tunacheza bao muda wote..
Ok kama Kambarage alifanya madudu. Haya tueleze waliofuatia nao wamefanya nini kama sio madudu zaidi ya Kambarage?
Hawa viongozi wetu kwa kweli ni mzigo wa misumari tumebebeshwa..Inafika mahali mtu unakuwa not proud to be Tanzanian..Unaona aibu kwa kweli..
Nyerere kikwazo ameshakufa,waliohai wamefanya nini cha maana??au ndio tabia za kiswahili kutafuta mchawi uku tunacheza bao muda wote..
Unajifanya mgeni na nji hii...hujui kuwa kila mwanya wa mtu kujitoa umebana??rushwa hadi kanisani/misikitini......Unadhani ni rahisi kama unavotaka nikuamini??Labda nikuuliza hiyo misumali umebebeshwa na nani? Halafu, kuhusu swala la kuwa sijui proud kuwa Mtanzania, usilikuze sana, hata wewe unaweza kufanya mambo mengi kama wewe pia yakakufanya ukawa proud, acahana na mabo ya Tanzania usiongelee kwa ujumla anza na wewe, Je umefanya nini, kukufanya uwe proud?
Siasa hizi mie siziwezi!
Nakubali kabisa kwamba tangu Nyerere aondoke basi ufisadi umekuwa maradufu lakini kunitaka nitaje hao waliofuata wamefanya nini(from african political point of view, u mean hawajafanya chochote!) ni kutaka kuniangiza kwenye siasa zisizo na tija kwangu!! Hata hivyo, ukweli bado utabaki pale pale, hatua kubwa ilipigwa na Kenya imetokana na msingi wa kiuchumi ambao uliwekwa na Kenyatta; sana sana, yule ambae alimfuatia(Moi) ndo alitaka kuuharibu. Ukweli bado utabaki pale pale, kwamba hata hayo machache yanayofanyika sasa yalitakiwa yawe yameshafanyika miongo kadhaa iliyopita.
Unajifanya mgeni na nji hii...hujui kuwa kila mwanya wa mtu kujitoa umebana??rushwa hadi kanisani/misikitini......Unadhani ni rahisi kama unavotaka nikuamini??
unaonekana umekata tamaa sana na maisha ya Tanzania, pole sana, lakini hata kwingineko pia sio rahisi hivyo, hiyo ndio bahati mbaya yenyewe, hivyo hatuna jinsi bali kuendelea kupambana tu, lakini bado naamini ukijituma sana bila kuchoka na kulalamika sana utafanikiwa tu, mimi ni mfano hai na wapo wengi tu kama mimi ambao tumeanzia sifuri 0 mpaka sasa tuna tunauwezo wa kumiliki kitu na kuendesha maisha yetu ndani ya Tanzania hii hii!