Kwanini Kamati ya Maadili ya Bunge haiwashughulikii hawa watu?

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,394
12,978
Hapo nyuma tumeona jinsi Kamati ya Maadili ya Bunge ilivyokuwa na nguvu. Baadhi ya Wahanga wake ni Pascal Mayalla, Zitto, CAG aliyepita, Gwajima na wengine wengi. Hapo nyuma tuliona jinsi watu walivyoitwa kwa mkwara, kuadhibiwa na kuonywa.

Ninachoshangaa ni jinsi Spika anavyoshambuliwa especially na wana CCM wenzake kwa kauli yake kuhusu deni la taifa. Kuna wengine wametoa kauli za dharau na kushusha hadhi na cheo cha Spika na yeye binafsi. Nimeona video ya Mwenyekiti wa CCM Njombe na Singida na wanaojiita muungano wa akina mama wa Vyama vya siasa... Kwa kweli inaleta maswali mengi. Huo ujadili wanatoa wapi?

Swali langu la msingi, Je Spika na Kamati yake ya Maadili wataitumia ile nguvu yao kuwapa hawa watu somo au watavumilia hii dhihaka inavyoendelea kuelekeza kwa Mkuu wa Mhimili.
 
Back
Top Bottom