Kwanini Kamati? Mabadiliko makubwa ni muhimu katika mfumo wa haki nchini

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,260
Mojawapo ya mabadiliko makubwa tunayohitaji katika nchi hii ni kuziondolea nguvu ya kuhukumu utitiri wa kamati zinazotoa adhabu kwenye masuala mengi ya nchii hii, mfano katika habari, uchaguzi na bunge.

Mahakama ndizo zinapaswa kutoa hukumu kwa kila jambo lenye kuhitaji hukumu za kisheria. Haipaswi kamati zitoe hukumu halafu ziwaambie wasioridhika wanaweza kwenda mahakamani,huko ni kutanguliza mkokoteni mbele badala ya punda anayeuvuta.

Kamati ziwie zinafungua mashtaka tu mahakamani na mahakimu au majaji ndio watoe uamuzi wa haki. Hii ni kwa kuzingatia kwamaba wengi wa watu wanaotoa hukumu katika hizo kamati hawana hata taaluma au weledi wowote wa kisheria hivyo ni vigumu kwao kutenda haki kwa walalamikaji au walalamikiwa.
 
Wakati wa kupitisha sheria kwa nini huwa mnatoka nje?
 
Nadhani wameweka huu utaratibu ili kupunguza misongamano mahakamani..
 
Njia nyepesi ya kupunguza msongamano mahakamani ni kufanya upelelezi na kukamata badala ya kukamata na kufanya upelelezi kesi zikiwa mahakamani.

Nadhani tumpe Tundu Lissu uongozi ili arekebishe haya mambo..

Maana huyu Wa sasa alishakiri kuwa hashauriki..
 
Back
Top Bottom