Kwanini kama taifa hatuendelei?

Kwanini kama taifa hatuendelei?

Mmmmmm ongezeko la watu ni opportunity kwa mfanyabiashara yeyote Maana soko la nguo za watoto, maziwa Ya watoto na baby products litakuwa kubwa mno hence kodi kubwa kwa serikali itakayoingia. Population is not a problem inategemea unatazama from which angle
mkuu tuzangumzia maendeleo ya jamii kwa ujumla,sio kila mwanajamii ataweza kutumia fursa hyo kupata kipato maana hizo biashara ulizotaja haziwezi fanywa na kila mtu
 
"it is dangerous to be right when the goverment is wrong"
-VOLTAIRE-

sent from my SM-galaxy s8+ using jamiiforums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: 30P
unsustainable economic growth
 
Taifa huendelezwa na watu wake kwa kutumia maarifa waliyo nayo pamoja na Juhudi ya kufanyakazi kiubunifu kwa kuongozwa na sera za kisiasa zinazoeleweka. Mwalimu aliwahi kusema kwamba ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, watu, Ardhi, Siasa safi na uongozi bora.

Kwa hali yoyote ile "Maendeleo" tuliyonayo inawezekana kabisa hayalingani na miaka ya Uhuru wa nchi yetu pamoja na idadi ya watu iliyopo. Ukitaka kuona ni kwa kiwango gani tuna umaskini angalia kiwango cha huduma za kijamii zinazotolewa kwa watanzania.

Ukiangalia miundombinu ya Afya, Elimu,Usafiri na usafirishaji,sayansi na teknolojia pamoja na mifumo ya kuendeshea mambo yetu jinsi ilivyo, bila ya shaka kuna ishara kwamba kama taifa bado tupo nyuma kimaendeleo.

Kama taifa tatizo letu ni lipi hadi hatua za maendeleo tunazozipiga inakuwa kama vile tunatembea kwa mwendo wa Konokono?
Ndo swali gani hili sasa,
Haujakamilisha uchunguzi halafu unatuuliza swali,
Weka ccm kando wape miaka mitano wapinzani waongoze,halafu Pima maendeleo,ukiona hatuendelei ndo uje uulize kwa nini hatuendelei,
Fikiri unawapa nchi watu ambao Leo wanasema pesa si ya umma wanaigawana,kesho wanarudi kusema ni ya uma na wanarudisha pesa hiyo serikalini,halafu hata siku haijaisha wanarudi tena kuzichukua [emoji23]

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Kama kulipa kodi hatuwezi..tunakuwa ombaomba ili kujazia kwenye kodi maendeleo yatatoka wapi..??
Vyote ulivyotaja elimu,afya,miundombinu vinahitaji hela...kama kodi hatulipi vitatoka wapi??
Nitajie nchi moja iliyoendelea ambayo watu hawalipi kodi kama Tanzania...
Kaka trust me,somalia wakipata utulivu kwa miaka mitano tu watatuzidi mbaaaaaali,

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Utasubiri Sana Kama unataka chama kikusaidie bilionea bakhresa na Reginald mengi hajawezeshwa Na chama Chochote endelea kusubiri chama utakufa lofa
Hapa nlipo wee na kuwa chichiem ila kwa ulofa umenizidi

Ova
 
Mmmmmm ongezeko la watu ni opportunity kwa mfanyabiashara yeyote Maana soko la nguo za watoto, maziwa Ya watoto na baby products litakuwa kubwa mno hence kodi kubwa kwa serikali itakayoingia. Population is not a problem inategemea unatazama from which angle
Pointless

Ova
 
Taifa huendelezwa na watu wake kwa kutumia maarifa waliyo nayo pamoja na Juhudi ya kufanyakazi kiubunifu kwa kuongozwa na sera za kisiasa zinazoeleweka. Mwalimu aliwahi kusema kwamba ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, watu, Ardhi, Siasa safi na uongozi bora.

Kwa hali yoyote ile "Maendeleo" tuliyonayo inawezekana kabisa hayalingani na miaka ya Uhuru wa nchi yetu pamoja na idadi ya watu iliyopo. Ukitaka kuona ni kwa kiwango gani tuna umaskini angalia kiwango cha huduma za kijamii zinazotolewa kwa watanzania.

Ukiangalia miundombinu ya Afya, Elimu,Usafiri na usafirishaji,sayansi na teknolojia pamoja na mifumo ya kuendeshea mambo yetu jinsi ilivyo, bila ya shaka kuna ishara kwamba kama taifa bado tupo nyuma kimaendeleo.

Kama taifa tatizo letu ni lipi hadi hatua za maendeleo tunazozipiga inakuwa kama vile tunatembea kwa mwendo wa Konokono?
La maana ni kujiuliza kwa nini Chadema hawajengi makao makuu yenye hadhi, hadi leo wako pale pale Mtaa wa Ufipa.
 
Adui nambari moja wa maendeleo ya Tanzania na Watanzania ni wahuni, wezi, majangili, watoa na wapokea rushwa wa MACCM.

Taifa huendelezwa na watu wake kwa kutumia maarifa waliyo nayo pamoja na Juhudi ya kufanyakazi kiubunifu kwa kuongozwa na sera za kisiasa zinazoeleweka. Mwalimu aliwahi kusema kwamba ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, watu, Ardhi, Siasa safi na uongozi bora.

Kwa hali yoyote ile "Maendeleo" tuliyonayo inawezekana kabisa hayalingani na miaka ya Uhuru wa nchi yetu pamoja na idadi ya watu iliyopo. Ukitaka kuona ni kwa kiwango gani tuna umaskini angalia kiwango cha huduma za kijamii zinazotolewa kwa watanzania.

Ukiangalia miundombinu ya Afya, Elimu,Usafiri na usafirishaji,sayansi na teknolojia pamoja na mifumo ya kuendeshea mambo yetu jinsi ilivyo, bila ya shaka kuna ishara kwamba kama taifa bado tupo nyuma kimaendeleo.

Kama taifa tatizo letu ni lipi hadi hatua za maendeleo tunazozipiga inakuwa kama vile tunatembea kwa mwendo wa Konokono?
 
Kwanza sijakujibu kwa kejeli lakini pia nimegundua watanzania husoma jambo tukiwa tayari na majibu yetu kichwani.

Mimi sijasema hatujaendelea bali nimesema maendeleo yetu tuliyonayo nadhani hayahakisi miaka yetu ya Uhuru pamoja na juhudi tunazofanya kulinganisha na idadi ya watu tuliyo nayo. Angalia nukuu toka kwenye bandiko langu hapo juu uone kama nimesema hatuendelei ama hatujaendelea kabisa. Swali langu ni rahisi sana, Maendeleo tuliyonayo ndiyo tunayostahili kuwa nayo?
Heading huwa ni sentesi inayoakisi maana nzima ya andiko. Maana yake kwa jinsi nilivyoelewa, kuna sehemu Fulani katika miaka hamsini ya uhuru tulitakiwa tuwe tumefika, ndiyo maana ukanijibu hivi,
Najua na kuendelea kuko kwa aina nyingi, hata hivyo Sisi tumeendelea kwenye nini? Kwa mfano kiuchumi Marekani imeendelea sana, lakini kwa utowaji wa huduma za jamii kwa wananchi, Sweden imeendelea kuliko Marekani. Sisi maendeleo yetu yapo kwenye nini?
Ndio maana nikakuuliza, wewe unatumia vigezo gani? Tumia takwimu na linganisha kati ya mataifa yaliyopata uhuru, mwaka 1961 na kuwa na population kama ya Tanzania. Pia kuwa na gdp kama ya Tanzania mwaka 1961 na sasa yamepiga hatua kubwa kuliko Tanzania.
Halafu ndiyo uulize sisi tumekosea wapi?
 
Kwanza Kobello nashukuru kwa mchango wako. Kipimo cha kwanza ni lazima tunapotaka kama taifa kujipima kama kasi ya maendeleo yetu inalingana na hapa tulipo, kwa mtizamo wangu si tu kuangalia nchi ambazo zilipata nasi Uhuru mwaka 1961 kwa sasa ziko wapi kimaendeleo kiuchumi na kijamii.

Kwa mtizamo wangu malengo ndiyo kipimo cha kwanza kuangalia kama tumefanikiwa ama la. Wewe unafahamu kwamba kupanga malengo ya maendeleo kuna vigezo vyake vya kisayansi hutumika. Huko nyuma na hata sasa huwa tunapanga mipango yetu ya maendeleo kwa miaka mitano mitano, na sasa tumeongeza na kitu kingine kinaitwa dira ya maendeleo.

Sangarara alinitahadharisha kwamba neno maendeleo ni kitu "Vague" na mimi nikamkubalia. Lakini kama taifa tunaweza kusema kwamba kwenye hili tumefanikiwa lakini katika hili hatujafanikiwa. Kuna mambo ya takwimu ambayo ni muhimu kwenye kupima maendeleo, lakini na takwimu nazo huweza kuchakachuliwa (Data manipulation) kunapokosekana uwazi.

Ukiachana na takwimu za kiujumula zinazotolewa na Benki Kuu na Idara ya Takwimu (National Bureau of statistics) takwimu zetu nyingi ni za kupika ana zinarudufiwa zile zile kwa lengo maalum. Kwa mantiki hiyo tunabakiwa na kigezo kimoja ambacho ni kuangalia kama tunapopanga mipango yetu tunafanikiwa ama la!
 
Idadi ya wasomi imeongezeka sana
miundo mbinu (usafiri,mawasiliano,utawala wa sheria n.k) imeboreshwa sana
Kidemocrasia
Kiuchumi
ni vingi sana

labda kama unataka kufananisha na mataifa mengine, lakini ukiangalia tulipokuwa 1990,1980,1970,1960,1950,1940,1930 n.k sio tulipo leo kwa mbali sana.
hizo ni fikra zilizojaa tope au mavi hivi Tanzania kuna kitu ambacho hawana ngoja nikutajiye kidogo : mito ya maji Zaidi ya 30 waziwa ya maji Zaidi ya 40 almasi, dhahabu, Shaba, chuma, tanzanite, uranium, makaa ya mawe, misitu, wanyama pori, gas, oil, ardhi ya kilimo, bahari,na kadhilika na kadhalika yaani Bongo inaweza kuilisha dunia yote lakini wapi wabongo wana akili kama zako.jini na nuksi ya nchii hii ni CCM full stop. Afya= 0 Elimu = 0 miundombinu = 0 kilimo = 0 maji = 0 umeme= 0 barabara= 0 ustawi wa jamii = 0 kila kitu ni =0 that is CCM miaka 56 ya utawala wake kila kitu ni = 0
 
Back
Top Bottom