Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,944
- 51,083
Taifa huendelezwa na watu wake kwa kutumia maarifa waliyo nayo pamoja na Juhudi ya kufanyakazi kiubunifu kwa kuongozwa na sera za kisiasa zinazoeleweka. Mwalimu aliwahi kusema kwamba ili tuendelee tunahitaji vitu vinne, watu, Ardhi, Siasa safi na uongozi bora.
Kwa hali yoyote ile "Maendeleo" tuliyonayo inawezekana kabisa hayalingani na miaka ya Uhuru wa nchi yetu pamoja na idadi ya watu iliyopo. Ukitaka kuona ni kwa kiwango gani tuna umaskini angalia kiwango cha huduma za kijamii zinazotolewa kwa watanzania.
Ukiangalia miundombinu ya Afya, Elimu,Usafiri na usafirishaji,sayansi na teknolojia pamoja na mifumo ya kuendeshea mambo yetu jinsi ilivyo, bila ya shaka kuna ishara kwamba kama taifa bado tupo nyuma kimaendeleo.
Kama taifa tatizo letu ni lipi hadi hatua za maendeleo tunazozipiga inakuwa kama vile tunatembea kwa mwendo wa Konokono?