Kwanini Kagame anachukiwa sana humu JF?

Mtanzania amchukie Kagame kwa lipi, wanaomchukia Kagame ni wanyarwanda waliopo Uganda, Kenya, na hapa Tanzania ambao ni members wa JF. Nasema kwa uhakika, wanyarwanda wengi waliopo Kenya wanamchukia sana Kagame and wish him dead kwa jinsi alivyoua watu kwenye genocide back in 1994.
 
Rwanda haina umoja bali watu wanaishi kwa uwoga, kama ambavyo mnatengenezwa wabongo sasa hivi.
Hizo laptop project sio serikali ni wahisani ndio walifanya hiyo kutokana na hali iliyopitia.
Vitu ulivyosema ni vyote wazungu ndio wahisani.
 
Kagame ni
Nimepitia threads nyingi Sana na comments za watu zinazomhusu Paul kagàme, nimesikitika Sana kwa njisi ambavyo watu hawamupendi kagàme , ninaomba tufanye uchunguzi na comments bila chuki binafsi

Angalieni , katika inchi za Afrika au duniani kote , Ni raisi gani amefanikiwa katika kuiletea maendeleo inchi yake ?

Amewaunganisha wanyarwanda wote , makabira ya Rwanda yote ni wamoja na wanampenda Sana kagàme , hiii Ni kupitia kampeni yake iliyoitwa SOTE NI WANYARWANDA.. na Sasa umoja na mshikamano vinaonekana

Amaefanikisha kumaliza rushwa katika inchi yake , ambapo inchi nyingine zimeshindwa kabisa ..

Elimu Ni Bora kuliko inchi yoyote , mfano kila mtoto ana laptop yake , pia kuonesha ubora wake wa elimu , Tanzania imeazima wataalamu wa IT kutoka rwanda

Anatengeneza ndege zisizotumia rubani maalufu Kama DRONES , na ndizo zinatumika kusambaza madawa inchini

Amewagawia wanyarwanda Ngombe na kuwajengea nyumba nzuri

Ameitangaza rwanda kupitia timu ya kubwa ya England ya ARSENAL kupitia VISIT RWANDA, Leo kila mtu duniani anaulizia RWANDA , watalii wanaongezeka kila kukicha ((nitawaletea takwimu )

Kwakweli Mimi siyo mnyarwanda ila nimependa uongozi wa huyu mjeshi , Ni uongozi unaotakiwa kuigwa na watawala wengine , na tukipata kiongozi wa hivi hata akitawala milele ni sawa tu ..

Angalia Burundi , imepitia matatizo sawa na RWANDA , lakin kimaendeleo na usalama bado iko nyuma Sana , hii Ni kwasababu ya kiongozi mubovu

Nawaomba watanzania wenzangu , tuache chuki binafsi juu ya Paul Kagàme , acha achape kazi kwa ajili ya watu wake ,

Anawaoenda watu wake na watu wake wanampenda Sana , Ni wachahe Sana mainterahamwe ndio hawampendi ,

Kiongozi Bora hawezi kukaa kimya akiona watu wake wanauawa , Ni kiongozi mpumbavu Sana anayeweza kuona watu wake wananyanyaswa na akakaa kimya ..!!

KAGAME ni kiongozi wa watu , na ingewezekana tungefanya awe rais wa Afrika ,

Acheni chuki za kipuuzi
kagame ni mwizi mkubwa ...bepari linalo changia kuifanya Congo ishindwe kuwa mahala salama pakuishi ....so tukiwa wapenda haki tunaanzaje kumpenda mtu kama huyo
 
Mnyarwanda gani anaridhika na kagame, Kama hujawahi kufika Kigali kaa kimya mkuu, wale watu wanaishi Kama wako Utumwani, kumzungumzia kagame kwa zuri au Baya Ni kujipalia makaa ya Moto muda wowote unakula risasi hadharani...
Kwani wewe unaridhika na rais wetu wa sasa? Hata marekani kuna wengi hawampendi Trump lakini mambo yanakwenda.
Mwenye macho haambiwa tazama. Rwanda na Burundi zilikuwa zinakaribiana sana kimaendeleo. Jee hivi sasa unaweza kuzifananisha?
Mimi binafsi ni muumini wa demokrasia lakini siyo demokrasia ya kimagharibi. Kimila nchi za kiafrika hazina haja ya kufundishwa demokrasia za wale ambao miaka hamsini iliyopita walituona kama ngedere na walipolazimika kutuacha ndipo hapo walipomwaga sumu ya kuweka vikaragozi wao na pale walipoona kuna manufaa kwao walitengeneza mizengwe iliyoleta maafa makubwa afrika.
Asilimia 90 ya migogoro yote ya afrika imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hao waumini wakubwa wa demokrasia.

Rwanda ilistahili kabisa kuwa na aina rais kama Kagame. Vita yake kubwa ilikuwa kwa vijana kufyekelea mbali uhutu na utusi na kuleta uzalendo. Kutokana na uchanga wa demokrasia nchini humo kuna wakubwa wengi hawapendi hali ya hivi sasa. Ile conduit ya kupitisha madini upande wa mashariki imezibwa. Hivyo choko choko lazima ziwepo.
 
Waulize wakongo wakwambie mabaya yake manake umeandika porojo nyingi sana za pauka pakawa. Wazungu pia wanajua Tanzania ni nchi yenye amani, raia wake waaminifu, wakarimu, wanapendana, hawana chuki..bla bla...Njoo Tz uone! Kagame hakusikika sana midomoni mwetu miaka ya nyuma na watu wengi hatukutaka kuju ishue zake. Alipo tuekea huyu mnyarwanda wake atuongoze ndio chuki ikaanza, mwambie amchukue huyu mnyarwanda wake ampe hata uenyekiti wa mtaa huko kigali.
Usipende kujidhalilisha na kuidhalilisha nchi yako mbele ya kanchi ka ajabu kama Rwanda kwa sababu ya cheap politics.
 
Mbona Burundi Ina saiz Kama ya Rwanda lakin bado wako nyuma ,

Alafu mkuu , inchi yetu ya tz kwa ukubwa wake na rasrimali zake zote tulizonazo , kimaendeleo ilitakiwa tuwe Kama marekani
Wewe si Mtanzania.
 
Kweli kabisa , hizi Ni chuki tu binafsi na wivu uliopitiliza , nashangaa sioni wakimutukana Nkurunziza au kumukosoa kwa Mambo yake , why always kagàme and rwanda ?

Waiache Rwanda , wao mbona hawaiongelei tz Kama ss tunavyoiongelea ??
Wanyarwanda munapenda kujisifia, lakini maskini wa kutupwa na watu dhaifu sana.
 
Huyu jamaa ni myarwanda tena ni mtusi.
Kiswahili sio cha mtanzania wala mkenya.

Kagame namkubali sana tena sana ila kuna mambo hapo yameongezwa chumvi na mleta mada.

Kagame ni mtu wa maendeleo na ni mdau mzuri wa kutekeleza masuala ya uhuru wa biashara na ajira kwa wakazi wa nchi zote za EAC.

Nakumbuka kipindi cha mwisho cha JK Rwanda walikuwa wanatoa ufadhili wa elimu ya masters na kuendelea kwenye mambo ya ICT kupitia tawi la chuo kikuu cha kimarekani kinachoitwa The Carnigie Melon University lililopo Rwanda.

Ufadhili zaidi ya $10,000 kwa mwanafunzi yeyote toka nchi za EAC, fedha hizo ni toka serikali ya Rwanda au tuseme walipa kodi wa Rwanda.

Raisi gani EAC aliwahi kufanya utu na undugu kama huo? Labda mzee Nyerere (R.I.P), nasema tena labda..

Kipindi hicho hicho mwana EAC yeyote mwenye sifa alikuwa anaruhusiwa kufanya kazi Rwanda bila usumbufu kama Mnyarwanda tu.

Chuki zingine dhidi ya Kagame ni za kupandikizwa na watu wanaodhania kushindwa kwao kisiasa au kiuchumi ni sababu ya Rwanda hasa Kagame.
Na wewe ni walewale.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom