Kwanini Kagame anachukiwa sana humu JF?

Kagame 'hapendwi' kwa sababu anaendesha nchi kwa mkono wa chuma.. Binadamu ni kiumbe asiyependa bughudha. Anapenda kubembelezwa.

Hata hivyo hana tofauti na Mungu anayetawala wanadamu kupitia hofu.. Inaaminika, ili uweze kummiliki mwanadamu afanye unayoyataka, mjaze hofu kwanza. Ndiyo mbinu wanayotumia hata majambazi, wachawi, majini, wakubwa kwa wadogo, wanyama mwituni n.k. HOFU.

Kuhusu wananchi wake kumpenda kunaweza kusababishwa na mambo mawili;

1. INTIMIDATION / HOFU (nimeshaifafanua hapo juu)
2. STOCKHOLM SYNDROME *(Ugonjwa wa watu kuwapenda watesi wao).
- Ufahamu vizuri zaidi ugonjwa huu >> What is Stockholm syndrome?

Kimsingi, Kagame ana nia njema ya kukuza uchumi na maendeleo ya nchi yake. Anataka nafasi ya S.Africa na Nigeria. Au tuseme anatamani Rwanda iwe kama Israel. Taifa dogo lenye uchumi mkubwa, elimu kubwa, nguvu kubwa na kadhalika.

Mpo hapo?
 
Back
Top Bottom